Ni msanii gani wa muziki Bongo ambaye tangu uanze kumsikia hujawahi muelewa kabisa?

Bongo fleva yote ya kuanzia 2010s sijawahi juielewa. Ndio maana utakuta nasikiliza zangu Jay Mo, Chid Benz, Prof Jay, Watengwa, Solo, Nature baasi
Yeah baada ya 2010 Bongo fleva imeharibika sana hakuna kinachoimbwa zaidi ya kubana pua,matusi na kukopi amapiano na nigerian beats
 
Na wale Solid Ground Family kitu cha bush party😂

Enzi zile wasanii walikua wanatoa burudani sana
 
Harmorapa nimejaribu msikiliza had kipindi p funk kamchukua ila wapiiii nkahisi labda mimi sio mwna hip hop.ila.kwa harmorapa nmechemka, sikio limekua zito.
 
Temba apa, jamaa nilikua simuelewi kabisa aisee.
Mpaka leo bado kipaji hana kabisa sijui ni ile TMK ilimbeba au ni nini.

Juma Nature, kwa jinsi alivyokua anasifiwa na media na kujizolea mashabiki lukuki ila sikuwahi muelewa.
Baadhi ya nyimbo za zamani ni kali ila za hao jamaa hapo juu sijui zilikua zinapendwa kwasababu gani. Wanaimba kama wanaongea tu kitu ambacho hata mimi naweza.
 
Aliyeimba nampenda Bibi kikongwe ni Dudubaya.
 
B2k mimi kama fan wake nitakupiga mawe
 
Ay kwa wale ambao wameanza kusikiliza bongo fleva early 2000 and before ndio utafaham. Lakin kama umeanza kusikuliza bongo fleva from 2009 kushuka nope, hutoelewa chochote
 
Ila we mzee umenichekesha sana 😂
Kwahiyo bila miwani uoni ?

Shikamoo babu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…