Ni nani alitaka kumuua Tundu Lissu?
Habari wana JF,

Hivi kati ya hawa watano tukiachana na story za kufikirika na za vijiweni ni nani hasa alihusika na shambulio la Tundu Lissu?

Binafsi nimemuelewa Tundu Lissu hataki kurudi nchini inawezekana kabisa hajui adui yake halisi ni nani.

sasa kati ya hawa mwenye maelezo ya kutosha amtoe wasiwasi Tundu Lissu ili arudi Tanzania:-

1. Vibaka au Majambazi kwa ajili ya kutaka Mali

2. Serikali ya Awamu ya tano ikiongozwa na Hayati JPM kwa ajili ya faida za kisiasa au Maendeleo ya Nchi kwamba alikuwa kikwazo

3. CHADEMA ili kuchafua Serikali kwa faida ya kisiasa au migogoro Chamani

4. WanaCCM wasiokuwa wanapenda kinachoendelea Awamu ya Tano na Uongozi wa JPM

5. Wengineyo ,kama kwa ajili ya wivu wa kimapenzi na n.k

Ni nani hasa? Ujue kwenye Siasa kuna mambo mengi unaweza aminishwa kitu kumbe ni Propaganda tu.

Unadhani ukiweka sababu kibao ndio zitafanya tuone dhalimu hahusiki?
 
Namba 3 na 4 very possible

Namba tatu kweli are you serious. Hivi unajua CHADEMA ilivyokuwa monitored usingeongea huo uongo.

Mbowe tu alipanga kujilinda na Sabaya lakini akafunguliwa kesi ya ugaidi. Ingekuwa ni CHADEMA Sirro na Moroto wasinge laza damu, Viongozi wote wangekamatwa.
 
Usihangaike number 2 hapo iko wazi kwa ushahidi wa kimazingira na mwingine:
  • Hivi amiri jeshi mkuu anasema wasaliti wanajeshi mnajua jinsi ya kudeal nao na kumalizia "he does not deserve to live". Ulitegemea ni nani alihusika?
  • Hivi matibabu ambayo ni haki yake unamsikia Spika anasema kuwa "rais amekataa kusaini fedha za matibabu" ulitegemea ni nani alihusika?
  • Hivi haki za kibunge kunyimwa kwa amri ya amiri jeshi mkuu! Ulitegemea nani alihusika na mauaji?
  • Hivi wabunge na mawaziri kupigwa marufuku kumtembelea mwenzao hospitali - Ulitegemea ni nani alihusika na mauaji?
  • Hivi watu kunyimwa kumchangia damu na hata kuvaa Tshirt za TL: Ulitegemea ni nani alihusika na mauaji?
  • Hivi Kukataa kufanya uchunguzi na kufanya vigisu za kuficha ushahidi kama vile kuondoa camera zilizochukua tukio! Kuondoa walinzi wakati wa tukio! Ni nani alihusika na attempted assassination?
Usituletee tena stori za oh Chadema, oh Vibaka; oh UVCCM.
Wauaji wapo waliokuwa waajiriwa wa Mwendakuzimu.
Wapo wanafuatilia hata uzi huu.
In the meantime let us pray justice for TL and while that devil is rotting and roasting in hell fire.
Hivi yako mangapi ambayo ulitegemea kwa kiongozi mkuu wa serikali?
Na ongeza na hili la kung'oa security camera zilizokuwa karibu na eneo la tukio
 
Kwahiyo yeye Lisu alikuwa msaliti?
 
jamaa alishaambiwa huwezi kuwa mslaiti ukasurvive 😀 😀 😀
 
Kwahiyo yeye Lisu alikuwa msaliti?

Lissu alikuwa threat kwa Magufuli ndio maana amemfanyia kila ubaya na hila Hadi kwenye uchaguzi, ila karma ya Lissu ikamshinda akafa moja kwa moja na kuacha Lissu analipwa vyote alivyopoteza.
 
Magufuri alikuwa ni shetani kwenye sura ya mwanadamu.

Kifo chake kimeokoa taifa. Hebu fikiria asingekufa leo hii tungekuwaje kama taifa?

Tumshukuru mungu
Kama ni hivyo basi mbona huyo lisu wako harudi?

Kwa hiyo huyo mungu wako ndio ameokoa taifa kwa mikodi na gharama za maisha kupanda?
 
Mbona yeye kafa sasa na Lissu anaishi. Binadamu hawezi kumpangia mwanadamu mwenzake siku za kuishi.
hakika mkuu wanadamu maisha yetu ni fumbo hadi leo siamini kama lowasa mzima au lisu alipona ila daah Mungu hapangiwii mzeee..
 
Habari wana JF,

Hivi kati ya hawa watano tukiachana na story za kufikirika na za vijiweni ni nani hasa alihusika na shambulio la Tundu Lissu?

Binafsi nimemuelewa Tundu Lissu hataki kurudi nchini inawezekana kabisa hajui adui yake halisi ni nani.

sasa kati ya hawa mwenye maelezo ya kutosha amtoe wasiwasi Tundu Lissu ili arudi Tanzania:-

1. Vibaka au Majambazi kwa ajili ya kutaka Mali

2. Serikali ya Awamu ya tano ikiongozwa na Hayati JPM kwa ajili ya faida za kisiasa au Maendeleo ya Nchi kwamba alikuwa kikwazo

3. CHADEMA ili kuchafua Serikali kwa faida ya kisiasa au migogoro Chamani

4. WanaCCM wasiokuwa wanapenda kinachoendelea Awamu ya Tano na Uongozi wa JPM

5. Wengineyo ,kama kwa ajili ya wivu wa kimapenzi na n.k

Ni nani hasa? Ujue kwenye Siasa kuna mambo mengi unaweza aminishwa kitu kumbe ni Propaganda tu.
Niwewe ulie usika
 
Lisu Kila uchwao Ahadi, Ahadi, Ahadi,

Unaelekea kuwa muongo muongo kama yule jamaa.
Mkuu

Tujiulize

Ishu ya lisu kupigwa risasi ilikuwa ya mtu Binafsi au ya system ya vipepeo wa nchi HII!!?

Kama ilikuwa ya system ni vigumu kujileta coz atamwamini Nani!!?

Madam hajamhakikishia usalama wake Binafsi kama mhanga!!

NADHANI katiba mpya itasimamia vyama vyote viwe salama kuepusha haya!!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA""!!
 
Jiwe, alichoka kusikia maneno ya kejeli ya TL kuhusu udikiteta wake uchwara - pamoja na vile alivyokuwa anawachachafya bungeni na miswaada yao na pupa isiyofuata misingi ya Katiba na Sheria za nchi. 🙂
 
Nasema "alietaka kumuua" kwa sababu ukiangalia yale matundu ya risasi upande wake wa gari utajua kuwa hawa watu hawakutaka kumtishia tu. Walidhamiria kumuua.

Niungane na Watanzania wenzangu kumuombea Tundu Lissu dua/sala ili apone kikamilifu, Amin.

Nimejiuliza maswali mengi kuhusu shambulio hili la kipekee kwa mbunge (sijui kama kulikwishatokea shambulio jingine kama hili), hapa Tanzania.

Yafuatayo ni malumbano ya kifikra ndani ya nafsi yangu kuwa ni nani hawa waliotaka Tundu Lissu afe. Maoni yako yanahusika, tafadhal.

Nimefikiria wahusika katika dhana 4. Nitazichambua hizi dhana moja moja.

Dhana zenyewe ni hizi. Washambuliaji ni:

1. Vichaa fulani tu. (Random act)

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.

3. Serikali yenyewe

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.

1. Vichaa fulani tu. (Random act)
Hii inawezekana lakini inakinzana na taarifa za kuwa Lissu alikuwa anafuatiliwa na magari kwa kipindi kirefu. Huu mpango ulisukwa na pia walijua wanaemtaka hadi kumfuata mpaka nyumbani kwake. Sidhani hii ilikuwa ni Random Act. Dhana hii ni potofu.

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.
Hii inawezekana kabisa. Wengi walimshutumu Lissu kwa kupinga sera zote za serikali (mimi nikiwa mmojawao). Kuna watu walikwenda mbali zaidi na kusema wanataka serikali iwaruhusu wamuue. Ndio maana kuna umuhimu wa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu hawa.

Katika demokrasia watu tunashambuliana vikali kwa hoja na sio kwa kuumizana au kuuana. Kama hii itathibitika, basi kuna umuhimu wa kuwapatia ulinzi wanasiasa machachari wanaoibua hisia kali.

Kuna uwezekano mkubwa dhana hii ni sahihi.

3. Serikali yenyewe
Kuna watu mitandaoni wanadhani ni serikali yenyewe ndio imeunda hii mbinu ya kumuua Lissu ili awaondolee kelele. Wengi wanasema Lissu amefichua siri nyingi za serikali kufikia kuwa tishio kwa hii serikali.

Kwa maoni yangu huu ni upuuzi. Serikali hii inakubaliwa na watanzania wengi. Hoja karibuni zote alizotoa Lissu dhidi ya serikali zinaweza kujibiwa kirahisi sana. In fact, baadhi ya shutuma za Lissu zinaipaisha serikali kwa Watanzania. Kelele za Lissu zinaweza kuwa baraka (blessing) kwa CCM ifikapo 2020. Kumuua Lissu kutajenga hisia za uonevu na kuwaonea huruma CDM ifikapo uchaguzi mkuu. Serikali haiwezi kufanya kosa hilo.

Kwa hiyo dhana hii ni potofu

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.
Hii dhana inahusisha watu wanaoichukia serikali (sio lazima wapinzani, inaweza kuwa watu wa nje) wanaotaka kumuondoa Rais Magufuli madarakani ifikapo 2020 kwa kuihusisha serikali yake na mauaji ya Lissu.

Serikali ya Magufuli imeathiri maslahi ya watu wengi sana wa ndani na wa nje. Akiendelea hivi hivi ana uhakika kabisa wa kupita ifikapo 2020. Sasa utaitoaje hii serikali madarakani ifikapo 2020. Jenga chuki kwayo.

Kama nilivyoeleza kwenye dhana namba 3, watu wakiamini kuwa serikali imemuua Lissu kinyama basi watawaonea huruma CDM na kuichukia CCM. CDM watachukua dola ifikapo 2020.

Je ni nani hawa wanaotaka kufanya unyama kama huu na kuisingizia serikali ya CCM (false-flag attack)?

Nina dhana nyingine 2 au 3 hivi (mfano, internal politics within CDM) lakini ni za pembeni sana na uwezekano wake ni karibu na sifuri. Kwa sasa hayo ndio malumbano yanayoendelea kichwani mwangu.

Please tell me I am not crazy.

==============================
Baada ya michango mingi iliyowekwa hapa kuna dhana niliyoigusia tu (Internal politics within CHADEMA) na wengi kuuliza kwa nini sikuifafanua. Hapa chini naiongeza ingawaje mwanzoni sikuipa kipaumbele.

Dhana ya 5.
Maadui wa ndani wa CHADEMA walitaka kumuua Lissu ili watimize malengo 3 yafuatayo.

1. Lissu aondoe ushindani katika uchaguzi ujao wa Uenyekiti.

2. Lissu aondoe ushindani katika uteuzi ujao wa mgombea urais ifikapo 2020.

3. Lissu atumiwe kama kafara ili kuipa CHADEMA mvuto na kuonewa huruma na kuichukia serikali katika uchaguzi wa 2020.
Sijui tindu au tundu namchukia kama nini ilikuwa zamani sio sasa kweli .
Ni mtu mmoja mnafiki mpenda madaraka na pia ni mtu ambaye akishika hii inchi weeeh tutakuwa burundi tutapigana wenyewe kwa wenyewe ni mtu mchochezi .

I HATE TUNDU SO MUCH RIGHT NOW
 
Back
Top Bottom