Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Habari wana JF,
Hivi kati ya hawa watano tukiachana na story za kufikirika na za vijiweni ni nani hasa alihusika na shambulio la Tundu Lissu?
Binafsi nimemuelewa Tundu Lissu hataki kurudi nchini inawezekana kabisa hajui adui yake halisi ni nani.
sasa kati ya hawa mwenye maelezo ya kutosha amtoe wasiwasi Tundu Lissu ili arudi Tanzania:-
1. Vibaka au Majambazi kwa ajili ya kutaka Mali
2. Serikali ya Awamu ya tano ikiongozwa na Hayati JPM kwa ajili ya faida za kisiasa au Maendeleo ya Nchi kwamba alikuwa kikwazo
3. CHADEMA ili kuchafua Serikali kwa faida ya kisiasa au migogoro Chamani
4. WanaCCM wasiokuwa wanapenda kinachoendelea Awamu ya Tano na Uongozi wa JPM
5. Wengineyo ,kama kwa ajili ya wivu wa kimapenzi na n.k
Ni nani hasa? Ujue kwenye Siasa kuna mambo mengi unaweza aminishwa kitu kumbe ni Propaganda tu.
Unadhani ukiweka sababu kibao ndio zitafanya tuone dhalimu hahusiki?