Habari za jumapili, nadhani unaelewa siku kadhaa zilizopita mheshimiwa, mwanaharakati Tundu Antipas Lissu alishambuliwa na watu wasiojulikana ,
Lakin kutokana Na watu hao kutojulikana imesababisha kila mtu kuhisi vinginevyo, tunajua kazi ya upelelezi ni ya polis Na vyombo vya dola, lakin hiyo haimuondolei mtu wa kawaida kujiuliza baadhi ya maswali juu ya kitendo Cha unyama alichofanyiwa Mr Tundu lissu,
Wengine wamehisi kuna mkono wa wakubwa, rejea swali la mtatiro kwamba kwanini serikali ihusishwe Na tukio ilo,
Lakin kwa upande wa apili wa shilling. Kuna wenye hisia tofauti Na za wale ambao wamepelekea mtatiro kuuliza swali,
Wengine wanahisi za kwamba mnyukano ndani ya chama hasa ukielekea uchaguzi ndani ya CHADEMA husababisha madhara makubwa ,
Ikumbukwe sisemi kwamba ndo sababu ya lissu kushambuliwa la hasha Ila nakuuliza kwanini dhana hiyo ijengeke miongoni mwa watanzania Na wana CHADEMA?
Pitia maoni ya mtu mmoja mchambuzi maarufu aliandika haya kwenye page yake
"Mwaka 2009 ulikuwa uchaguzi ndani ya Chadema,lakini mwaka mmoja kabla, yaani July 2008 Chacha Zakayo Wangwe alifariki ktk ajali ya gari iliyogubikwa na utata mwingi.
Mwaka 2014 ulikuwa uchaguzi ndani ya Chadema,mwaka 2013 habari zilisambaa kuwa mmoja wa vijana wa Chadema (jina linajulikana) alituhumiwa hadharani kuwa akitumwa kumuwekea Sumu Zitto Kabwe.
Mwaka 2018 ni uchaguzi mkuu ndani ya Chadema, Septemba 2017 Tundu Lissu amepatwa na tukio la kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Haya matukio hayahusiani, ila yote yametokea mwaka mmoja kabla ya mwaka wa uchaguzi ndani ya Chadema. Inavyoonekana mwaka mmoja kabla ya uchaguzi huwa siyo mwaka mzuri sana kwa viongozi wa juu wa Chadema
[HASHTAG]#GetWellSoonTunduLissu[/HASHTAG] [HASHTAG]#LetUsAllPray4Lissu[/HASHTAG] "
Hii inaleta picha kuwa pia hata mnyukano ndani ya chama unahisiwa,
Samuel