Ni nani alitaka kumuua Tundu Lissu?
Katiba ya nchi inaruhusu kutoa mawazo...
Na mm niseme tu inawezekana asilimia 83.3.
 
Hao watu wasiofahamika wanamahusiano makubwa sana na presidential race 2020 ndani ya chadema....haina ubishi lisu ameanza kumoverwhelm mamvi politically.hawezi kuwa salama.....the oldman knows who and how to play dirty

Sent using Jamii Forums mobile app
Vipi wasiojulikana kwa kuingia sehemu yenye ulinzi na kupiga risasi za kutosha then haooo mpka moro

Sent using Jamii Forums mobile app
 
If that is the case....Mamvi angemmalizia kabisa Lissu huko huko Kenya alikopelekwa maana yeye na Uhuru ni Marafiki. Njoo na lingine tena hili naona linapwaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaribio la mauaji ya Mh Tundu Lissu itaibua hisia nyingi sana.
Ni dhahiri aliyefanya jaribio hilo alikuwa na vitu viwili, haraka na hasira.

Kwa vyovyote jaribio hilo halikupangwa kwa utaalam unaohitajika katika operation kama hizo.
Na haya ni maoni yangu tu kutokana na kusoma operation nyingi kama The Jackal, katika kitabu cha The Day of the Jackal, ambayo ni hadithi ya ukweli juu ya jaribio la kumwua rais wa Ufaransa, Charles De Gaulle.

Ukifuatilia hadithi kama ile kunakuwa na mission objectives : kufanikiwa kumua aliyekusudiwa.
Katika mission yenyewe, target anatakiwa kuuwawa bila kuwepo mtafaruku, au kuacha traces za muuaji.
Na hii ni pamoja muuaji kutokomea na asionekane baada ya ku accoplish mission.

Tukirudi katika jaribio la kumuua Lissu, kwa kweli unaona waliolitekeleza ni novices-si wataalam.

Ndiyo, aliyepiga risasi alitumia bunduki aina ya SMG, Sub machine gun yenye uwezo wa kumwaga magazine ya risasi 30 au zaidi katika sekunde chache.

Kwa mtaalam pengine angetumia risasi moja tu!

Kitengo chetu cha UWT, kiko vizuri, kina utaalam na wataalam kwa kazi kama hizo.
Kwa maoni yangu hili jaribio limetekelezwa na assasins ambao sana sana wamekula hela ya mtu aliyewatuma.

Kwa kukosa utaalam na kuishia mission un-accomplished,
hiyo haiwezi kuwa kazi ya UWT, hivyo serikali.


Kimsingi pamoja na manyanyaso mengi yanayotokana na matamshi ya Lissu, hata hivyo sababu za kumwua haziko dhahiri.

Hata hivyo kwa imani niliyo nayo katika UWT, changamoto kwao ni kuwabaini hao "watu wasiojulikana" ili Idara iweze kuendeleza imani waliojijengea kwa wananchi kwa miaka mingi.

Kuwaachia polisi suala hili will be a big mistake.
 
Bila shaka wale wale watakuwa wahuni tu wenye nia ya kuichafua serikali..
Ingekuwa ni mkakati wa serikali, watu wenye uzoefu wa ujasusi lazima kungekuwa na fall back plan (plan B, C etc).
Mfano, wanajua kabisa hitmen lazima waondoke eneo la tukio ndani ya dakika kadhaa....ikitokea wameshindwa kumuuwa (wamemjeruhi), lazima kuwe na plan B...watakuwepo watu pembeni watakaozuga kama watu watakaokuja kutoa msaada...hao watamaliza kazi....hiyo ikishindikana, kutakuwa na plan C, ambayo ni hospitali...madaktari watakaopangwa kule lazima mmojawao awe mwenzao, anamaliza mchezo...hawa ni wazi hawakuwa na fallback plan..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na yule aliyemuoneshea Nape bastora nae bila shaka ata kuwa muhuni aliyelenga kuichafua serikali,hata yule alimwaga risasi km njugu mbele ya malima nae bila shaka,aliyempiga bom mwangosi hata nae muhuni tu alitaka kuichafua serikali,hata waliomteka Roma,wakamwagia nanii tindikali,na alowasema Bashe bungeni nao wahuni tu wanataka kuichafua serikali,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao watu wasiofahamika wanamahusiano makubwa sana na presidential race 2020 ndani ya chadema....haina ubishi lisu ameanza kumoverwhelm mamvi politically.hawezi kuwa salama.....the oldman knows who and how to play dirty

Sent using Jamii Forums mobile app
Km Nape mwenyewe hawezi amini huu upuuzi, ni wazi utapata wajinga wachache sana watakaokuamini.Ila watakaokuamini ni watu wa hovyo sana kuwekeza nguvu nyingi hivi.Kwa vile hao hao watu, kwa siku wanakuamini na kutakuamini km wiper inavyotembea. Kwa hili wana CCM mitaani wanakiri kuwa sasa imefikia pabaya hakuna haja tena ya uvyama.
 
Na yule aliyemuoneshea Nape bastora nae bila shaka ata kuwa muhuni aliyelenga kuichafua serikali,hata yule alimwaga risasi km njugu mbele ya malima nae bila shaka,aliyempiga bom mwangosi hata nae muhuni tu alitaka kuichafua serikali,hata waliomteka Roma,wakamwagia nanii tindikali,na alowasema Bashe bungeni nao wahuni tu wanataka kuichafua serikali,

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kwanza tunaongelea jaribio la mauaji ya mh Tundu Lissu.
Yule aliyemtolea bastola Nape, its on record Polisi wakimkana kuwa si mtu wao.
Idara nyingine hazikuwahi kumkana.
Waliomuua Mwangosi ni Polisi, mmoja alipelekwa mahakamani.

Kwa Kibanda, Ulimboka na Roma ndio hao "wasiojulikana".

Bunge ligutuke sasa na kutunga sheria kali ili vyombo vya ulinzi vidhibiti watu ndani yao wasiweze kutumiwa kiholela na wanasiasa fulani fulani na kuliletea Taifa aibu.
 
Habari za jumapili, nadhani unaelewa siku kadhaa zilizopita mheshimiwa, mwanaharakati Tundu Antipas Lissu alishambuliwa na watu wasiojulikana ,

Lakin kutokana Na watu hao kutojulikana imesababisha kila mtu kuhisi vinginevyo, tunajua kazi ya upelelezi ni ya polis Na vyombo vya dola, lakin hiyo haimuondolei mtu wa kawaida kujiuliza baadhi ya maswali juu ya kitendo Cha unyama alichofanyiwa Mr Tundu lissu,

Wengine wamehisi kuna mkono wa wakubwa, rejea swali la mtatiro kwamba kwanini serikali ihusishwe Na tukio ilo,

Lakin kwa upande wa apili wa shilling. Kuna wenye hisia tofauti Na za wale ambao wamepelekea mtatiro kuuliza swali,

Wengine wanahisi za kwamba mnyukano ndani ya chama hasa ukielekea uchaguzi ndani ya CHADEMA husababisha madhara makubwa ,

Ikumbukwe sisemi kwamba ndo sababu ya lissu kushambuliwa la hasha Ila nakuuliza kwanini dhana hiyo ijengeke miongoni mwa watanzania Na wana CHADEMA?

Pitia maoni ya mtu mmoja mchambuzi maarufu aliandika haya kwenye page yake

"Mwaka 2009 ulikuwa uchaguzi ndani ya Chadema,lakini mwaka mmoja kabla, yaani July 2008 Chacha Zakayo Wangwe alifariki ktk ajali ya gari iliyogubikwa na utata mwingi.

Mwaka 2014 ulikuwa uchaguzi ndani ya Chadema,mwaka 2013 habari zilisambaa kuwa mmoja wa vijana wa Chadema (jina linajulikana) alituhumiwa hadharani kuwa akitumwa kumuwekea Sumu Zitto Kabwe.

Mwaka 2018 ni uchaguzi mkuu ndani ya Chadema, Septemba 2017 Tundu Lissu amepatwa na tukio la kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Haya matukio hayahusiani, ila yote yametokea mwaka mmoja kabla ya mwaka wa uchaguzi ndani ya Chadema. Inavyoonekana mwaka mmoja kabla ya uchaguzi huwa siyo mwaka mzuri sana kwa viongozi wa juu wa Chadema

[HASHTAG]#GetWellSoonTunduLissu[/HASHTAG] [HASHTAG]#LetUsAllPray4Lissu[/HASHTAG] "


Hii inaleta picha kuwa pia hata mnyukano ndani ya chama unahisiwa,

Samuel
 
Back
Top Bottom