Ni nani alitaka kumuua Tundu Lissu?
ADUI WA ADUI YAKO NI RAFIKI YAKO
RAFIKI WA ADUI YAKO NI ADUI YAKO.

WAR OPPORTUNIST:
mdhuru/mchokoze/mchonganishe adui wa adui yako ili pindi wanapigana wewe ubaki kama msaidizi ili kuepuka madhara ya moja kwa moja na kufanikisha hitaji lako.
Mifano halisi:
sadam hussein v/s U.S.A. , USA ili kulinda maslahi yao (si ya Iraq) walifanikisha hilo na mpaka sasa no stability in Iraq.

Gadafi v/s U.S.A, USA ili kulinda maslahi yao (si ya libya) walifanikisha hilo kupitia kigezo cha demokrasia kupitia watu wa libya na mpaka sasa no stability in libya.

Vision:
Tanzania resources V/S Mataifa fulani (chini ya kivuli cha kampuni fulani ya uchimbaji madini)
Ili kulinda maslahi yao ( rasilimali zetu) wanaweza fanya yafuatayo:
  • Kuhakikisha kwanza wanavuruga ushirikiano wa kitaifa ili kupitia hapo watapata adui wa adui yao katika maslahi yao hivyo kuanzia hapo watamtumia adui wa adui yao kukamilisha kusudio lao wakiwa pembeni.
  • Watatumia kila hila (hata kumwaga damu) ili kuhakikisha wanatengeneza chuki baina pande mbili hizo, katika namna ya kificho kisha kumuuliza si unaona walivyowabaya?
  • Kauli pekee watu hawa fulani iliyofanikisha mission zao almost zote duniani ni kaneno DEMOKRASIA.
Tutafakari kwa kina na tuchambue kwa kina ili kukwepa kuangukia sehemu isiyo sahihi kifikra dhidi ya kilichomtokea ndugu yetu lissu.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Mbariki Rais wetu, Mungu mponye Tundu Antiphas Lissu.
Ni mtazamo wangu.
Habari ya Lissu iachiwe wapelelezi...kubuni huku hakusaidii
 
ADUI WA ADUI YAKO NI RAFIKI YAKO
RAFIKI WA ADUI YAKO NI ADUI YAKO.

WAR OPPORTUNIST:
mdhuru/mchokoze/mchonganishe adui wa adui yako ili pindi wanapigana wewe ubaki kama msaidizi ili kuepuka madhara ya moja kwa moja na kufanikisha hitaji lako.
Mifano halisi:
sadam hussein v/s U.S.A. , USA ili kulinda maslahi yao (si ya Iraq) walifanikisha hilo na mpaka sasa no stability in Iraq.

Gadafi v/s U.S.A, USA ili kulinda maslahi yao (si ya libya) walifanikisha hilo kupitia kigezo cha demokrasia kupitia watu wa libya na mpaka sasa no stability in libya.

Vision:
Tanzania resources V/S Mataifa fulani (chini ya kivuli cha kampuni fulani ya uchimbaji madini)
Ili kulinda maslahi yao ( rasilimali zetu) wanaweza fanya yafuatayo:
  • Kuhakikisha kwanza wanavuruga ushirikiano wa kitaifa ili kupitia hapo watapata adui wa adui yao katika maslahi yao hivyo kuanzia hapo watamtumia adui wa adui yao kukamilisha kusudio lao wakiwa pembeni.
  • Watatumia kila hila (hata kumwaga damu) ili kuhakikisha wanatengeneza chuki baina pande mbili hizo, katika namna ya kificho kisha kumuuliza si unaona walivyowabaya?
  • Kauli pekee watu hawa fulani iliyofanikisha mission zao almost zote duniani ni kaneno DEMOKRASIA.
Tutafakari kwa kina na tuchambue kwa kina ili kukwepa kuangukia sehemu isiyo sahihi kifikra dhidi ya kilichomtokea ndugu yetu lissu.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Mbariki Rais wetu, Mungu mponye Tundu Antiphas Lissu.
Ni mtazamo wangu.
Kwamba Lisu ndiye adui?
 
Ndiyo shida ya uongo unasahau juzi ulisema nini.
Kila ukija unakuja na mapya na wahandishi sijui ni kwa sababu ya kuhongwa wanashindwa kuhoji
Waandishi hata usiwalaumu maana nao wanaogopa kukutana na watu wasio julikana
 
UCHAGUZI WA KENYA, RISASI ZA LISSU NA MATIBABU MJINI NAIROBI.


Nataka nieleze ambavyo Dereva wa Mh. Tundu Lissu anavyoweza kuwa alichangia ama kwa uzembe tukio la Risasi kwa Lissu kufanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Nikweli kwamba watu wetu wengi wanapenda kusifiwa tu na kushabikia hivyo hawapendi kuelezwa ukweli.
So far hizi ni hisia zangu ambazo si lazima zifuatwe wala kuaminiwa. Matusi niliyoyapokea tangu jana facebook na whatsup yametosha kunisaidia kufikiri namna nyingine ambayo inaweza kuwa ilisaidia tukio lile kukamilika. Kama una hasira usisome!!

Unakumbuka kuwa Uchaguzi Mkuu wa Kenya ulibatirishwa na Jaji wa Mahakama Kuu ya huko na kuamriwa kurudiwa tena ndani ya Siku 60?? (Zingatia).

Unakumbuka kuwa Lissu alipigwa Risasi siku mbili baada ya tarehe Mpya ya Uchaguzi kutangazwa na siku moja baada ya Uhuru Kenyatta kufungua Kampeni zake huko Kenya?? (Zingatia).

Unakumbuka kuwa Chama kikuu cha Upinzani hapa Nchini kilitangaza nia ya kumuunga mkono Uhuru Kenyetta ktk mbio zake za Urais na Vijana wao hapa ndio wapiga debe wakubwa wa Kenyatta?? (Zingatia).

Unakumbuka kuwa ktk Uchaguzi wa Tanzania kuna Viongozi wakubwa wawili wa Kisiasa walifariki vivyo hivyo Kenya ktk uchaguzi wa awali wamefariki Viongozi wawili wanaohusiana na IT ya Tume ya Uchaguzi?? (Zingatia).

Je umewahi kusikia kuwa Rais wa Tanzania na Mgombea Urais wa Kenya kupitia muungano wa NASA Raila Odinga ni marafiki wakubwa hata kabla ya Rais wa Tanzania kuwa Rais na kwamba hiyo ndio sababu iliopelekea Chadema kuukacha upinzani na kuungana na Uhuru Kenyatta??? (Zingatia).

Uliwahi kusikia kuwa Raila Odinga anatumia jina la Magufuli ktk kampeni zake na kwamba akichaguliwa ataongoza Kenya kama Magufuli anavyoongoza Tanzania na kwamba hiyo inamsaidia sana kuukaribia Urais wa Kenya?? (Zingatia).

Je wajua kuwa Lowassa alikwenda Kenya kumfanyia Kampeni Kenyatta lkn pia baada ya Lissu kupigwa Risasi Lowassa hajasema lolote hadi sasa??

Je wajua kuwa Tundu Lissu alipopigwa risasi alikimbizwa Hospital ya Dodoma akiwa hoi, akahudumiwa hapo, akapata pumzi kisha ikaonekana kuwa Tanzania hakuna usalama hivyo sasa anapata matibabu Nairobi Kenya??? (Zingatia).

Kama umeyakumbuka mambo yote hayo kwa ukamilifu, sasa tutafakari kwa pamoja.

Ametokea mtu mmoja mlevi tilalila akasema kuwa'
"Kwa kuwa Lissu alikua mkosoaji mkubwa wa Serikali ya JPM (wote tunajua), na kwa kuwa Chama chake kinamuunga mkono Uhuru Kenyatta, na kwa kuwa ni lazima Uhuru Kenyatta ashinde, kwa hivyo uliandaliwa utaratibu wa kumshoot intetionally Lissu, aumizwe kisha akatibiwe Kenya na wakati wote wa matibabu (kumbuka ndio wakati wa Kampeni pia Kenya) itazungumzwa kuwa Lissu ameumizwa na Serikali ya JPM kwa sababu alimwita Dicteta Uchwara halafu wakati wote huu Rais Uhuru Kenyatta atahusishwa kwa karibu kama mtu anaetoa support ya ulinzi wa Tundu Lissu.

Homework:

Unganisha matukio yote halafu unipinge kwamba kwa Lissu kwenda kutibiwa Kenya Serikali ya Tanzania na jina la Rais Magufuli litakua halijachafuliwa na hivyo kumpunguzia nguvu Raila Odinga ktk Kampeni zake. Why not Rwanda, ok, acha Rwada. Why not Uganda ama hata South Afrika if the case ni Usalama??

Unganisha matukio hayo halafu unipinge kwamba kwa kufanikiwa huko Uhuru Kenyatta atakua hajatengenezewa kura za nyingi za huruma mbele ya macho ya Wakenya, na Raila amedhoofishwa kwa sababu hawezi tena kusema nitaiongoza Kenya kama Magufuli anavyoiongoza Tanzania. Enhe!! Tell me!!

Unganisha matukio hayo kisha unambie kuwa ukimya wa Lowassa hauna tafsiri yoyote ktk hili, kwamba tukio hili halina madhara yoyote ktk Uchaguzi wa kenya wa Oct 17 on the favor of Uhuru Kenyatta.

Kumbuka, kabla ya kupinga kwa lolote jiulize sababu za Lissu kwenda kutibiwa Nairobi. Am not so stupidy! Usiseme sababu za kiusalama. Usalama haiwezi kuwa na msingi wowote kwa sababu waliompokea akiwa mahutihuti Dodoma ni Watanzania na Hospital ile ni ya Serikali kwa hiyo wangeweza kufanya lolote even before Mbowe kufika. So far thietre Madakta huwa wanaingia pekee na mgonjwa.
Anyway, akili ni nywele kila mtu ana zake."TAFAKARI"
[HASHTAG]#SipendagiKudanganywaKijingaMimi[/HASHTAG] [HASHTAG]#skata[/HASHTAG] mtata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ok, kama ndiyo usemavyo....?
Kwa nini Serikali na vyombo vyake vya usalama visiwatie nguvuni hao unaowasema? Yani adui aingie nchini na kupiga mtu risasi afu Serikali isimtie nguvuni?

Roma mkatoliki alitekwa na kuteswa kisha anapatikana na serikali ikatuakikishia kulishuhulikia Hilo swala, lakini mpaka leo hatujui limeishia wapi!!!

Hivi kweli upo serious on what you have written?

Cha kumshukuru Mungu ni kwamba Tundu Lissu bado anapumua na soon hili giza litaisha na mwanga mkali utatanda juu ya Nchi ya Tanzania na kila mwenye Akili na macho ataona yote ambayo yamejificha kwa sasa hatuyaoni
 
Habari za jumapili, nadhani unaelewa siku kadhaa zilizopita mheshimiwa, mwanaharakati Tundu Antipas Lissu alishambuliwa na watu wasiojulikana ,

Lakin kutokana Na watu hao kutojulikana imesababisha kila mtu kuhisi vinginevyo, tunajua kazi ya upelelezi ni ya polis Na vyombo vya dola, lakin hiyo haimuondolei mtu wa kawaida kujiuliza baadhi ya maswali juu ya kitendo Cha unyama alichofanyiwa Mr Tundu lissu,

Wengine wamehisi kuna mkono wa wakubwa, rejea swali la mtatiro kwamba kwanini serikali ihusishwe Na tukio ilo,

Lakin kwa upande wa apili wa shilling. Kuna wenye hisia tofauti Na za wale ambao wamepelekea mtatiro kuuliza swali,

Wengine wanahisi za kwamba mnyukano ndani ya chama hasa ukielekea uchaguzi ndani ya CHADEMA husababisha madhara makubwa ,

Ikumbukwe sisemi kwamba ndo sababu ya lissu kushambuliwa la hasha Ila nakuuliza kwanini dhana hiyo ijengeke miongoni mwa watanzania Na wana CHADEMA?

Pitia maoni ya mtu mmoja mchambuzi maarufu aliandika haya kwenye page yake

"Mwaka 2009 ulikuwa uchaguzi ndani ya Chadema,lakini mwaka mmoja kabla, yaani July 2008 Chacha Zakayo Wangwe alifariki ktk ajali ya gari iliyogubikwa na utata mwingi.

Mwaka 2014 ulikuwa uchaguzi ndani ya Chadema,mwaka 2013 habari zilisambaa kuwa mmoja wa vijana wa Chadema (jina linajulikana) alituhumiwa hadharani kuwa akitumwa kumuwekea Sumu Zitto Kabwe.

Mwaka 2018 ni uchaguzi mkuu ndani ya Chadema, Septemba 2017 Tundu Lissu amepatwa na tukio la kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Haya matukio hayahusiani, ila yote yametokea mwaka mmoja kabla ya mwaka wa uchaguzi ndani ya Chadema. Inavyoonekana mwaka mmoja kabla ya uchaguzi huwa siyo mwaka mzuri sana kwa viongozi wa juu wa Chadema

[HASHTAG]#GetWellSoonTunduLissu[/HASHTAG] [HASHTAG]#LetUsAllPray4Lissu[/HASHTAG] "


Hii inaleta picha kuwa pia hata mnyukano ndani ya chama unahisiwa,

Samuel
Wewe ni muongo na mchawi serikali ifanye Wewe uihusishe chadema
 
Niliona dr.mipango alivokuwa anaongea inaonekana alikuwa hajajipanga.nilisikia anasema walioshiriki wakamatwe jana muda uleule jamani nauliza hadi sasa nani kakamatwa
 
Wewe ni mwehu hizo propaganda zako ni za kijuha na kishamba sana ni wajinga pekee wanaweza kuamini ujinga wako huu
Bora umeniwahi. Huyo skat na lithread lake lirefu kumbe limejaa pumba za eti unganisha! Alivyovieleza havina uhusiano hata kidogo na tukio lile. Ccm hamna wajanja humo bali kuna waganga njaa na vibaka watoa roho. Mlisema cdm wanahusika na sasa wageni kutoka nje!
Shaka kkawaumbua juu ya uhusika wenu na hata mkijazana humu kujitetea ni kazi bure.
 
Wahusika halisi umewaweka namba ya mbali,ili uanze na porojo!Kwanini 3 haijaanza?
 
Back
Top Bottom