Ni nani alitaka kumuua Tundu Lissu?
View attachment 586551

Serikali yoyote makini haiwashambulii wapinzani wake Bali huutumia upinzani kama kioo cha kujiangalia Na kujirekebisha.


Je lissu anawezaje kuwa mzembe kiasi cha kukubalia kuendeshwa Na Dereva asiyemuamini?

1. Kuna hoja kuwa kwanini Dereva wa lissu ndugu Adam hajapatwa Na risasi hata moja? Hii nitaijibu kwa mifano miwili hai.

- Hivi rais JKL alivyouwawa Dereva wake alipigwa risasi? Kwaiyo Dereva wake ndo alishiriki kumuua?

- Sheikh abood rogo aliuwawa akiwa Na baba mkwe wake ,je baba mkwe wake alipigwa risasi ? Kwaiyo baba mkwe wake alishiriki kumuua?

Hivi Dereva kupigwa risasi ndo kithibitisho kuwa hajahusika? Au Dereva kutokupigwa risasi ndo kithibitisho kuwa alihusika?

Kama Dereva anahusika baada ya wauaji kukimbia kwanini hakummaliza lissu akaamua kumkimbiza hospitali?

2. Kuna hoja kuwa baada ya Dereva kujua anafwatiliwa kwanini hakwenda sehemu yenye usalama? Hivi hoja nitaijibu kama ifwatavyo.

- Je mtaa wanaishi viongozi mbalimbali kama spika ,mawaziri,waziri Mkuu, wabunge sio sehemu salama? Kweli?

-Je ndo Mara ya kwanza kwa lissu kufwatiliwa? Hamuoni kama lissu alihisi watafwatiliwa kisha wataachwa kama ilivyo kuwa kawaida?

Kama Dereva anahusika kwanini alimzuia lissu asishuke kwenye gari baada ya kuona gari lililokuwa linawafwata bado lipo?

Ingekuwa Dereva anashirikiana nao si angemuacha lissu ashuke kwenye gari ili wauwaji wapate "clear shot"?

3. Kuna hoja kuwa kwanini baada ya lissu kwenda Nairobi Dereva kakimbia /kajificha ,Hii ni hoja dhaifu kuliko zote lakini nitaijibu

-Je mlienda nyumbani kwa Dereva wa lissu hamkumkuta ? Sasa kwanini mnasema kajificha? Mlitaka kumuona wapi?

- Je polisi walimpigia simu Dereva wa lissu aende kituoni akakataa?Kwanini mnasema kajificha/kakimbia.

mr mkiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
kilichobaki ni kila mtu afunge domo lake tusubirie alienusurika kufa apone na aje kusema lolote. Wengine wote ni tunaropoka 2. . . .kila mtu na speculation zake ambazo ni kama kubahatisha tu ila ukweli upo. Tusubirie muhusika atasema lolote 2
 
Hisia zangu zinasema, le mutuz na Murro ni hitman's bodyguards
 
Bashite ndiye muhusika mkuu hao wanajaribu kumtetea. Lakini nawaambieni mtajisafisha kote lakini mbele za Mungu hamtaweza, dua, maombi, damu iliyomwagika na vilio vya Watanzania vitawasababishia laana kubwa sana Mungu sio wa mchezo
 
Shari alilovaa bluu shati lilopigwa risasi jeupe
Bongo movie inaendelea
Stering ni mpenda kiki hormorapa
86222f0a3e96bda9267c755037d54628.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
Acha uzembe,kwa hyo hapo ulipo hujui hata kutoa huduma ya kwanza kwa mtu anaevuja damu nyingi afu unakuja kuchangia hapa
Apply pressure kwa nguo yoyote ktk jeraha linalotoka damu kwa wingi.haya kajipange upya
 
Mbona wengine wamekuwa wanaongea wao hamkusema haya!?
Mnawashwa na mnajua wanayochambua yameenda shule sanaaaaa.
Uoga wa nini!?
Tatizo bavicha na cdm yote sasa hivi inaongozwa na Mange. Akishasema yeye basi. Kila mtu ataimba wimbo wa mange.
Hata viongozi wakuu sasa hivi hutoa matamko baada ya kuhakikisha mtazamo wao unaendana na mange

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ukishakuwa unafanya vitu tofauti na mungu alivyokuumba huwa akili nayo inapotea na kuwaza upuu tu.
 
mimi nafikiri no 4 ina make sence
Rais sio mpumbavu kiasi cha kufanya jambo ambalo matokeo yake yanaonekana wazi kuwa ukifanya hivi matokeo ni vile: katika siasa kwa mbinu , nafikiri kuna uwezekano akawepo mtu pembeni ambae amefanya tukio ili tu serikali ipate lawama, na wanafanya hivo kwakua akili za waTanzania ni nyepesi sana kisomeka zilikolalia....(nafikiri ndio maana walisema tunatumia asilimia moja tu ya uwezo wetu wa akili)

Kila mtu anafahamu kuwa Rais wetu ana maadui nje na ndani ya Tanzania,kwahiyo lolote laweza tokea. Ngojeni uchunguzi au Muhusika aamke aweze kutoa majibu sahihi.
 
Haikutegemewa kwa Mwenyekiti wa Chadema Freman Mbowe akubali kirahisi kumkaribisha Waziri Mkuu ailiyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond Edward Lowassa ndani ya chama hicho kisha awe kinara wa kumpigia debe agombea urais mwaka 2015.
Duru za kisiasa zinaelelezea na kutaja bayana kuwa bila shaka yoyote nyuma ya pazia iko siri nzito ndani ya mtungi iliojificha baina ya vigogo hao wawili kwani bila nguvu za uenyekiti wa Mbowe basi Lowassa asingekuwa mgombea urais .
Majina ya vigogo wa Chadema wakiongozwa na Mbowe,Tundu Lissu, Dk Wilbroad Slaa, Abdallah Safari, John Mnyika, Godbless Lema na Halima Mdee ndiyo waliokuwa wakimpiga madongo mazito Lowassa wakati akiwa CCM huku wakimwita fisadi.
Dk Slaa ndiye aliyetaja orodha alioiita ni ya vigogo mafisadi papapa"list of shame "akidai ndani ya Serikali ya CCM akiwemo na Lowassa huku Lema naye akishangaa iweje vibaka na wezi wa kuku wamefungwa jela lakini mtu aliyeiibia serikali (yaani Lowassa) anatanua na kutambua mitaani.
Mara baada ya jina la Lowassa kukosa vigezo na sifa ndani ya CCM kwa ajili ya kuwania urais. Lowassa akaamua kuruka ukuta na kuhamia Chadema asubuhi 8 usiku akafanya majadiliano na siku iliofuata jioni yake akatangazwa ndiye mgombea wa chadema chini ya Ukawa. Mchalato huo umechukua siku mbili baada ya kujifungia kwa Mbowe na Lowassa katika mazungumzo ya faragha.
Mbowe akatoka kikaoni huku akiwa na msimamo mpya wa kisiasa ulioshangaza huku akisahau maneno yake ya awali aliyoyatoa huku akimnanga Lowasaa kwenye majukwaa ya kisiaa katika mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani.
Katika mazingira ya kushtua Mbowe akawashangaza watanzania na wana chadema aliposimama na kusema hawezi kukubali kuutupa mtaji wa mwanasiasa nguli anayeitwa Lowasa kwa kumsikiliza mwanachama au kiongozi yeyote ndani au nje ya Chadema.
Mbowe akaenda mbali zaidi na kusema yuko tayari wahame wananchama na viongozi10000 ila abaki na mtaji wa Lowassa ambao anaamini utakipa hadhi na heshima mpya chama hicho ili kizidi kujengeka kuliko kilivyokuwa. .
Mbowe bila kutarajia akajikuta akiyabeza na kuyasahau maneno yake, kuukana msimamo wake, bila aibu akawa anayaramba matapishi yake mwenyewe na kuuitia ulimi wake puani mwake .
Hata hivyo halikuwa jambo jepesi na rahisi kwa baadhi ya wanasiasa ndani ya chadema kuuafiki ujio wa Lowassa na kukubali moja kwa moja awe mgombea wa urais atakayepeperusha bendera ya chama hicho.
Miongoni mwa wanasiasa waliomkataa katakata Lowasa ni pamoja na Dk Slaa , Mnyika, Lissu , Dk Abadallah Safari na Dk Mwesiga Baregu ambao hawakuona kama kuna maana au tija yoyote kumchukua Lowassa na kumfanya mgombea sahihi wa urais .
Mbowe alipata kazi kubwa ya kuwashawishi wanasiasa waliomkataa Lowassa akiwemo Lissu ambaye hoja na msimamo wake ulionekana waziwazi hakuafiki ujio wa Lowassa .Zipo taarifa za uhakika zisemazo Lissu na Mnyika walikubali shingo upande na kuhofia chama chao kisipate mpasuko , mgawanyiko na kukitia misukosuko.
Lissu na Mnyika wakafanya kampeni za kumnadi Lowassa kama kuanua ngoma juani huku wakiwa na masikitiko lakini wakishindwa kukihama chama hicho kutokana na kukijenga kwa dhiki, shida na tabu hadi mahali alipokikuta Lowassa akavutiwa ajiunge nacho.
Dk Slaa ndiye aliyeonyesha misuli ya msimamo thabit na kukataa kuyumba mbele ya macho ya walimwengu. Akatamka bayana kuwa hakubaliani na uamuzi huo kwani licha ya kwamba kama atauridhia mpango ungempa fedheha lakini pia ungempunguzia heshima yake kama mtu aliyewahi kulitumikia kanisa .
Akajiondoa Chadema huku akitoa hoja nzito zenye mashiko akisema kwanini anaachama na siasa akiamini kutoka kwake ni hatua ya kumkimbia Lowassa kwani alishiriki kumchafua kwa nyakati tofauti hivyo hana jinsi ya kumsafisha kwa wakati huo .
Kuhama kwa Dk Slaa toka Chadema kukampa mwanya mkubwa Mwanasheria Tundu Lissu kuvivaa viatu vya Dk Slaa na kuwa nyota ndani ya chama hicho huku akiwafunika wenzake kina Lowasa , Mbowe na Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye .
Machachari ya Lissu kisiasa yakazidi kumpa nafasi zaidi .Akaanzisha kuwafuta polepole kwemye remani ya siasa za Chadem kina Lowassa , Mbowe na Sumaye .Ungetokea uchaguzi ndani chama hicho na Lissu akatamani kuwania uenyekiti, bila shaka Mbowe asingemzuia au kumshinda kwa kura.
Inaelelezwa kuwa Lissu si kwamba ana uahawishi na uwezo wa kukubalika hadi kushinda uenyekiti lakini pia hata angetaka achukue fomu ya kuwania urais , asingechomoza mwanasiasa wa kumzuia aidha iwe ni Lowassa Lawrence Masha au Sumaye.
Pia inatajwa Lissu bado ana ndoto ya kutegua na kukizika kitendawili kinachoitatiza chadema cha kuonekana chama hicho ni cha kanda ya kaskazini na uchaga badala yake anataka akipe sura mpya ili kizidi kukubalika na kuifuta hoja ya uchaga na ukanda.
Wapo wanaosema Mbowe hawezi kukubali kumpisha mwanachama yeyote awe Mwenyekiti ndani ya Chadema licha ya kushika kwake uongozi kwa vipindi viwili huku upande wa pili wa shilingi kina Lowassa, Masha, Baregu na Sumaye nao hawako tayari kumwachia Lissu usukani .
Yapo maneno na utabiri usemao kuwa kutakuwa na mchuano mkali kati ya Lissu, Mbowe , Masha , Lowassa na Sumaye mwaka 2020 aidha katika kuwabia urais huku kukitabiriwa kutokea ushindani mkubwa ikiwa Lissu, Sumaye na Profesa Baregu mmojawapo akichukua fomu ndani ya chama hicho.
Mbowe kwa wakati huu na kwa jinsi upepo wa kisiasa ulivyovurugika ndani ya Chadema, yaonyesha hana ubavvu wala nguvu tena za kisiasa kumzuia mwanasiasa yeyote kama alivyomfanyia Zitto Zuberi Kabwe hadi akachomoa kuwania uenyekiti .
Si Mbowe tu laikini pia hata Muasisi wa chama hicho Mzee Edwin Mtei naye haonekani tena kuwa na ushawishi wa kumlainisha mgombea yeyote asithubutu kuchukua fomu ya kuchuana na Mbowe kama alivyoenddsha mazungumzo ya muafaka kati ya Mbowe na Zitto.
Kumekuwa na maswali mengi yanayoulizwa bila kupatikaana majawabu tokea Lissu akumbwe na dhahma ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.Je ndoto na matarajio yake zake ndiyo yamegota ukingoni au safari yake ya kisiasa itakuwa imepigwa ngwara?
Mashariki na wafuasi wa Lissu wanazidi kumuomba mungu ampe afya njema na uzima , apone haraka kisha arudi teba ulingoni kuendeleza mapambano pia aelezee kila kitu na ukweli wa mambo ulivyo .
Sharifa Masuzu
 
Ngoja nikukumbushe. Hivi unakumbuka Zitto Kabwe, Kitila, na Mwigamba waliandaa waraka wa kutaka yafanyike maboresho ya uongozi na demokrasia ndani ya CHADEMA lakini walifukuzwa kwa madai walitaka kufanya mapinduzi ndani ya chama?

Na katika mgogoro huo wa kufifisha nyota ya Zitto ising’ae na kuwa mwenyekiti wa CHADEMA akionekana kama pandikizi la serikali ndani ya CDM, Zitto aliwahi kudai kutaka kuwekewa sumu kwenye kinywaji na Ben Saanane aliyekuwa mtu wa karibu sana wa Mbowe ambaye naye pia amepotezwa kimya kimya na wenye CHADEMA wenyewe na baadaye kuitupia lawama serikali.

Hii ni moja ya mikakati ya Mbowe kuendesha chama hicho kimafia na kidikteta ili kulinda maslahi yake ndani ya chama kwani alikuwa akikitumia chama hicho kwa mambo mbalimbali binafsi ikiwemo kukikopesha chama kwa riba kubwa. Hivyo basi watu wasishangae kuona shambulio la kufifishwa nyota ya Lissu asiendelee kung’aa ndani ya CHADEMA kwani walishafanya hivyo kwa Chacha Wangwe, Kafulila na wengineo.

Nawaza tu kwa sauti.

BenMpo
 
Pale mashabiki wa simba wanavyomshambulia Tshishimbi na mashabiki wa yanga wanavyowashambilia akina okwi,Niyo

Haya bwna watani wa jadi sie tunabaki kutizama movie
 
Back
Top Bottom