View attachment 586551
Serikali yoyote makini haiwashambulii wapinzani wake Bali huutumia upinzani kama kioo cha kujiangalia Na kujirekebisha.
Je lissu anawezaje kuwa mzembe kiasi cha kukubalia kuendeshwa Na Dereva asiyemuamini?
1. Kuna hoja kuwa kwanini Dereva wa lissu ndugu Adam hajapatwa Na risasi hata moja? Hii nitaijibu kwa mifano miwili hai.
- Hivi rais JKL alivyouwawa Dereva wake alipigwa risasi? Kwaiyo Dereva wake ndo alishiriki kumuua?
- Sheikh abood rogo aliuwawa akiwa Na baba mkwe wake ,je baba mkwe wake alipigwa risasi ? Kwaiyo baba mkwe wake alishiriki kumuua?
Hivi Dereva kupigwa risasi ndo kithibitisho kuwa hajahusika? Au Dereva kutokupigwa risasi ndo kithibitisho kuwa alihusika?
Kama Dereva anahusika baada ya wauaji kukimbia kwanini hakummaliza lissu akaamua kumkimbiza hospitali?
2. Kuna hoja kuwa baada ya Dereva kujua anafwatiliwa kwanini hakwenda sehemu yenye usalama? Hivi hoja nitaijibu kama ifwatavyo.
- Je mtaa wanaishi viongozi mbalimbali kama spika ,mawaziri,waziri Mkuu, wabunge sio sehemu salama? Kweli?
-Je ndo Mara ya kwanza kwa lissu kufwatiliwa? Hamuoni kama lissu alihisi watafwatiliwa kisha wataachwa kama ilivyo kuwa kawaida?
Kama Dereva anahusika kwanini alimzuia lissu asishuke kwenye gari baada ya kuona gari lililokuwa linawafwata bado lipo?
Ingekuwa Dereva anashirikiana nao si angemuacha lissu ashuke kwenye gari ili wauwaji wapate "clear shot"?
3. Kuna hoja kuwa kwanini baada ya lissu kwenda Nairobi Dereva kakimbia /kajificha ,Hii ni hoja dhaifu kuliko zote lakini nitaijibu
-Je mlienda nyumbani kwa Dereva wa lissu hamkumkuta ? Sasa kwanini mnasema kajificha? Mlitaka kumuona wapi?
- Je polisi walimpigia simu Dereva wa lissu aende kituoni akakataa?Kwanini mnasema kajificha/kakimbia.
mr mkiki.
Sent using
Jamii Forums mobile app