Ni nani alitaka kumuua Tundu Lissu?
Na kuhalalisha mauaji hayo hali tosha ndi ka na,mstaafu wa jeshi nae kashambuliwa,ili ionekane sio shambulizi la kisiasa,sio sirikali ndio inahusika bali wahalifu tu!!!

Viwanda vinazidi kujengwa kwa matukio ya mtutu,awamu ya V-WONDER!!!
 
Chadema from 1995-2015=fikra za mabadiliko Chadema from 2015=comedy
Hadi aibu maskini chadema mliuza chama.bavicha mnatumiwa ovyo
Lakini ukweli uko wazi chadema viongozi wake ndo mafisadi wenyewe wazee wastaafu.wengine ma dj wameuzia vijana madawa ya kulevya kwenye club zao.wametumia ujanja wa sheria kutetea waizi wa rasilimali..kwa magufuli mtakoma.na bado wale mlioficha hela nje mjiandae.fanyeni maigizo yote lakini keki ya taifa sasa inagawanywa.ile mitandao ya ufisadi chini ya mstaafu ilioutaka urais .imefeli.magabacholi mmefeli.wafanyabiashara magendo mmefeli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa mzee ..naona mnakuja na spinning doctors za kutosha.

Uongo hauleti viwanda.
 
Kama Nguvu na muda uliyotumia kuandika hayo madudu, ungetumia kufikiri na kujiimarisha kimaisha ungekuwa mbali sana.

Kama fikra zenyewe ndiyo hizi zimetekwa na mafunzo ya chipukizi basi maneno ya viwanda yatapia kama yalivyopita ya kilimo kwanza.

Tuna safari ndefu sana kuondoa funza wa ujinga kwenye ubongo wa vijana wengi waliopitia chipukizi.
 
Inawezekana wakahusika who knows, sasa ili kuthibitisha hilo na bila kumungunya maneno mmeambiwa na CDM taifa waiteni hao wapelelezi wa nje waje kusaidiana na Police wetu ili kubaini ukweli - Kama ni Lowassa ama Mbowe kahusika si itajulikana fasta tu gogoro hapa ni nini?

Pia mlishauriwa kile kipindi cha Mabomu kule Arusha, muunde tume ya kijaji kubaini mbivu na mbichi lakini hadi wa leo mmegoma kabisa
 
Those who stand the benefit of death of the Lissu. Simple and clear dont try to meander.
 
Hadi sasa shambulio la kupigwa risasi kwa Lissu, Serikali mtuhumiwa namba moja, lakini embu tujiulize maswali yafuatayo kabla ya kuinyoshea kidole Serikali. Ni mara ngapi serikali imekuwa ikimkamata Tundu Lissu na kumuachia aendelee na shughuli zake? Hivi kama ilikuwa na nia ya kumuua si ingekuwa rahisi kwa mar azote walizomkamata? Najiuliza serikali inawezaje kufanya shambulio la aibu hivyo na kujiwekea mazingira ya kujichagua mbele ya jumuiya ya kimataifa.

Shambulio lililofanywa ni shambulio la “kuteka media na wananchi kihisia” likionekana wazi lengo lake ni kuitaka Serikali ionekane mbaya mbele ya macho ya wananchi na jumuiya ya kimataifa. Hii imetufanya tusiweze kuangalia jambo hili kwa jicho la tatu. Kwa kipindi cha miaka miwili ya utawala wa Magufuli Serikali imejitengenezea maadui wengi wenye nguvu kipesa na kimadaraka, maadui hawa kwa hali ilivyo sasa wanaweza kufanya lolote kuifanya serikali ionekane mbaya tu. Wanaweza kufanya lolote ili kuhakikisha wanalipiza kisasi kwa “adui yao” ambaye tangu ameingia madarakani amekuwa akionyesha vita ya kutaka kuwaondoa wafanyabiashara, wasasiasa na vigogo waliokuwa wanajinufaisha kwa mali za Serikali.

Nashawishika kuamini shambulio la Lissu ni moja ya kisasa kwa “adui” serikali. Siku iliyopangwa kufanyika kwa shambulio hili, ilikuwa ni siku muafaka ya kufanya taarifa muhimu ya Serikali kwa umma isijadiliwe, na badala yake kuhamisha mawazo ya wananchi na vyombo vya habari kujadili shambulio la Lissu, hii ni dhahiri ilipangwa.
 
c and p

Shambulio la Mbunge Tundu Lissu henda tukaliona kubwa sana ila kama watanzania ni waungwana tujikubushe athari ya yaliyotokea kibiti.

-JUMLA YA WALIOKUFA NI ZAIDI YA AROBAINI.

-Wote walikuwa ni viongozi wa serikali na chama na 17 walikuwa ni askari polisi.

-wastani wa utegemezi kwa familia ni watu nne

_jumla ya familia zilizopoteza wapendwa wao ni zaidi ya arobaini.

-serikali ilipoteza watumishi

-zaidi ya wanawake arobaini waliachwa wajane

-zaidi ya wategemezi 160 waliachwa bila msaada. Hivyo kupelekea ugumu waaisha kwa familia hizo.

-wengine walijeruhiwa.

Matukio haya hayakupewa uzito sana na vyama vya upinzani, na kituo cha Haki za binadamu na kuoneka ni kitu kirahisi sana na hakuna hasara kwa taifa.

-Uzito wa swala la Lissu wala halifiki hata robo wa lile la kibiti.

Tukio la Lissu kushambuliwa linastua ndio ila sijona umuhimu wa kutaka hata kuingila shughuli za baadhi ya mihili kama Bunge. Vyombo vya ulinzi vinafanya kazi yake sioni haja ya baadhi ya wanasiasa kuwachanganya watanzania.

Tunathamini na kuheshimu mchango wa Lissu hapa nchini hivyo tunajali pia uhai wake. Sote tunaungana kulaani tukio lile na yote yaliyotokea Kibiti na kwingineko. Tunamuombea Lissu apate nafuu, Mungu amponye.

-press zenu hazina umuhimu kusaidi uchunguzi bali kufaidisha umati na mitandao ya kijamii. wasilisheni malalamiko yenu mahala sahihi.

mzalendo ink.


www.facebook.com/mzalendoT

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mtu aliyekaa na halmashauri yake ya kichwa kiaamua kuwa Tundu Lissu lazima auawe tena mchana kweupe kwa kupigwa Risasi zisizo na idadi, tutambue kuwa ni hatari sana kuliko ambavyo baadhi mnamchukulia.

Tusidhani kwamba huyo mtu hampendi Lissu peke yake hapa nchini au duniani. Jana alikuwa Lissu nadhani baada ya Lissu kutoweka ni Mimi au wewe.

Narudia tena huyu mtu ni hatari sana si kwa mwanaccm, cuf, ACT wazalendo wala chadema. Hakuna aliye salama

Tunaochukulia mzaha tukio hili tuendelee, but Time will tell
 
Huyu mtu aliyekaa na halmashauri yake ya kichwa kiaamua kuwa Tundu Lissu lazima auawe tena mchana kweupe kwa kupigwa Risasi zisizo na idadi, tutambue kuwa ni hatari sana kuliko ambavyo baadhi mnamchukulia.

Tusidhani kwamba huyo mtu hampendi Lissu peke yake hapa nchini au duniani. Jana alikuwa Lissu nadhani baada ya Lissu kutoweka ni Mimi au wewe.

Narudia tena huyu mtu ni hatari sana si kwa mwanaccm, cuf, ACT wazalendo wala chadema. Hakuna aliye salama

Tunaochukulia mzaha tukio hili tuendelee, but Time will tell
Mkuu tamaa ikishika mimba huzaa dhambi, na dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti......... Huyo mtu aliyefanya tukio lile siku zake zinahesabika, mark my words!!
 
Huyu mtu ni mithili ya njiti ya kiberiti huanzia nakamoto kadogoooo

Punde ataendesha mauwaji ya halaiki na kupoteza watanzania wengi wa vyama vyote hata wale wa chama chake. Anaamini hakuna mwingine zaid yake.

Hatari sana.
 
tahadhari ichukuliwe mapema tu hususani vyombo vya ulinzi na usalama visimamie vizuri secta zao kwani tunakoendea si kuzuri ukiangilia suala la Lisu lilikuwa na Mtazamo wa kisiasa lakini kadri siku zinavyozidi kwenda suala hili limeanza pata picha mpya mambo ya kiimani yameanza jitokeza hii ndio baya baya zaidi

wito vyombo vya ulinzi na usalawa fanyeni kazi yenu kiweredi zaidi msikubali kuongozwa na mtu asiyejua taluma yenu inasemeje kuhusu usalama wa inchi ,mtu na mali yake
 
Back
Top Bottom