Ni sahihi kuendelea kulea mtoto wa kusingiziwa?

Mtoto ananiwazisha sana

Nina hakika huyu mtoto anaingia kwenye maisha magumu sana

Baba mtoto mwenyewe ni Playerboy asiye na uelekeo wa kutunza mtoto

Kwenye Hii Dunia hautakiwi kuwa na huruma, hasa ukiwa Mwanaume.
Hasa huruma za kijingajinga.

Huyo mtoto anaweza asipitie hayo Maisha magumu unayoyasema,
Muache yeye na Baba yake
 
This late Popular Player PELLE aliwahi zaa na Mtumishi wake, alimkataa mtoto even after DNA kukubali bado alikataa mtoto.

Ila mwishoni hapo aligawa mirathi pia kwa wana familia aliowakataa, the lady was passed away 17 year before pelle.

What's umehakikisha mtoto siyo wako una uhuru wa kuendelea kuwa naye kwa vile umeamua hivyo

Na nyie wanawake muwe mnapunguza kusema. sema hivyo.
 
Kwenye Hii Dunia hautakiwi kuwa na huruma, hasa ukiwa Mwanaume.
Hasa huruma za kijingajinga.

Huyo mtoto anaweza asipitie hayo Maisha magumu unayoyasema,
Muache yeye na Baba yake
Baba yake yupo Huko Kusini dereva wa Daladala kazalisha sana wanawake huko

Dogo day care nimelipia 2m ada ya mwezi sijui maisha yake yatakuwaje

Mama mtu naye n mzigo tu kila unachomwanziashia kufanya kinakufa
 
Ada ya mwaka sio.mwezi
 
Wanajukwaa niwashauri wazuri sana. Hapa utapokea ushauri wa kila rangi.

Baki na msimamo wako mkuu maana ninaweza nikakuambia mtoto hana makosa fukuza mke, baki na mtoto
 
Baba yake yupo Huko Kusini dereva wa Daladala kazalisha sana wanawake huko

Dogo day care nimelipia 2m ada ya mwezi sijui maisha yake yatakuwaje

Mama mtu naye n mzigo tu kila unachomwanziashia kufanya kinakufa
Daycare gani ADA 2Mil kwa mwezi?

Daycare wakati mama yake ni Mama wa Nyumbani?
 
Baba yake yupo Huko Kusini dereva wa Daladala kazalisha sana wanawake huko

Dogo day care nimelipia 2m ada ya mwezi sijui maisha yake yatakuwaje

Mama mtu naye n mzigo tu kila unachomwanziashia kufanya kinakufa

Hayo hayakuhusu, aliyekuwa anakuhusu ni Mkeo ambaye naye kumbe hakupendi ndio maana kazaa na Mwanaume mwingine.

Kuhusu biashara, hiyo ni kawaida, hata wewe kuna biashara ukipewa kama huna uzoefu nayo inaweza kukufia hata mara Saba kila ukipewa mtaji
 
Nimegundua wife alichepuka akabeba mimba na kujifungua mtoto hafanani na mm baba yake wala mama yake

Hapa nimekaa na mtoto hadi miaka miwili imefika

Nipo njia panda nimuache wife na mtoto au niendelee kuishi nao!?
Pole sana ni heri umkute nwanamke ana mimba au ana mtoto tayali unajua moja kwa moja huyu sio wangu lkn hiyo kwako ni changamoto sana , mwanamke anaweza kuchepuka na asipate mimba, na anaweza pata mimba nje ya ndoa ila yeye asijue hii mimba nimepata nje ya ndoa,

Kwanza kabla hajachukua maamuzi yeyote hakisha kweli mtoto sio wako, eidha mwenyewe akili kwmb mtoto sio wako au ukapime , baada ya hapo wasiliana na familia yako kiundani zaid utapata mwanga, mzuli kisha chukua hatua, jambo hilo sio la kujurupuka kaka
 
Piga chini huyo, atakuletea vidonda visivyopona mpaka unaondoka hapa duniani.
 
Lazma ushtuke maana mtoto wa kwanza nafanana nae iweje huyu hata mama ake hamfanani,pili nilimnunua smartphone nikamuweke callrecoder faili nikalificha,baada ya week mbili nikajua mpaka jamaa anaongea na kuhusu mtoto wake na mpaka mama mkwe alishaambiwa.
Na ukasamehe
 
Achana nae tuu, kama ameweza kumvulia chupi mwanaume mwingine na akijua kabisa ni mke wa mtu na kamzalia mtoto achana nae tuu ni kirusi hicho, ukiendelea nae utaendelea kuumia moyo Kila siku mwisho utachukua maamuzi mabaya
 
Pole sana kwa yote Mungu akusaidie katika changamoto unayopitia.
 
Mtoto ananiwazisha sana

Nina hakika huyu mtoto anaingia kwenye maisha magumu sana

Baba mtoto mwenyewe ni Playerboy asiye na uelekeo wa kutunza mtoto
Sikuwa na mpango wa kucomment,ila baada ya ww kuandika huu utopolo, nimelazimika kucomment.

Unalalamika mtoto sio wako, at the same time unamuonea huruma as if ni yatima wakati baba na mama yake wapo.

Kitu kingine cha kijinga ulichoandika, eti baba wa mtoto ni playboy hawezi mtunza mtoto, hivi akili yako inafikiria sawa sawa au ndio upo under depression? Kwavile baba wa mtoto hana uwezo wa kutunza mtoto, vipi akitaka mtoto wa pili, upo tayari aje azae tena na mkeo, ili ww mwenye uwezo wa kutunza umtunze?

Situation kama hizo, solution huwa ni mbili tu, either upige chini mama na mtoto, au ukubali kuendelea nao. Na ukishachagua moja, basi kula buyu, life lisonge, hakuna kugeuka nyuma.

Comments zako inafikia hatua badala ya kukuonea huruma, zinatukera.
 
Japo umetumia lugha kali lakini nimekuelewa kaka asante sana

Depression inanitesa kwa sasa
 
Back
Top Bottom