Ni sahihi kwa mtoto kuona picha ya baba yake alipokuwa mtoto?

NI kweli hujui au unajitoa fahamu kwamba picha za utoto au hata za zamani zina mafunzo mengi kwa watoto wako, wajukuu na hata waliokuzidi umri? Huo siwezi kuuita mfumo dume kiuhalisia ni mfumo pori.
 
Unakuta mtoto ana miaka 15 na kuendelea kisha anakutana na picha ya utotoni ya baba yake. Baadae jioni anamuona baba anarudi nyumbani.

Hivi mnadhani huyu mtoto anaweza kuweka au kudumisha heshima kwa mzazi aliyokuwa nayo awali?
Umeona ya mzee wako nini?😂😂
 
Dah, nimeona -ve reaction ya watu humu na sijui ishu ni nini. Unajua kuna umri ukifika kuna ishu fulani zinazokuhusu ziwe na mipaka kwa kizazi kifuatacho. Mfano katika hali ya kawaida tu mwanaume mwenye miaka 70 hivi nakuendelea inabidi yeye ndiye awe mzazi aliyebakia, kwa maana ya kutoa maamuzi ya mwisho kwenye himaya yake. Sijajua kama nimeeleweka vyema

Pia natamani sana awepo mchangiaji mmoja kudadavua mada hii na kuonyesha upungufu uliojitokeza kuliko hizo duh, dah, aisee... na mengine
 
Pole sana kijana

Mimi nilifikiri umejiamini na hii mada yako kumbe umeianzisha ukitegemea positive reactions tu, najua hapo ulitegemea comments nyingi za uungwaji mkono kama "kweli kabisa" au "tena wamama ndio wanaongoza kwa kutunzatunza hayo mapicha, matokeo yake wanakuja kuwaonesha watoto wanawaharibu, sisi wababa hatunaga hayo mambo" nk, toka kwa wanaume wenzio ili uonekane mwamba

Lakini kwa bahati mbaya umekutana na negative reactions ikabidi uanze kujiquestion mwenyewe kwamba umekosea wapi, sikiliza unapoleta mada hapa jf kama kweli hiyo mada ina mantiki hautakuwa na mashaka na ulichokiandika, ila tukiona tu unaanza kujitilia mashaka mwenyewe, basi wengine tunaona huna tofauti na wale wanaoanzisha mada za kipuuzi za "kimasihara" sijui "wanawake ni viumbe hatari sana", ili tu wapate validation hasa toka kwa wanaume wenzao
 
Hujaeleweka kabisa. Unaweza tena kutuma version nyingine ya hoja yako, mkuu
 
Back
Top Bottom