Ni vigumu CHADEMA kuleta mabadiliko nchi kwa sababu ya udini

BAKWATA na Ccm ni ndugu wa karibu.
Na awamu hii BAKWATA imefanikiwa sana kuzileta taasisi nyingi za Kiislamu pamoja chini ya mwavuli wake, nafikiri ni taasisi ya Sheikh Ponda tu ndio taasisi kubwa isiyo pamoja na BAKWATA.
 
Na awamu hii BAKWATA imefanikiwa sana kuzileta taasisi nyingi za Kiislamu pamoja chini ya mwavuli wake, nafikiri ni taasisi ya Sheikh Ponda tu ndio taasisi kubwa isiyo pamoja na BAKWATA.
Mwaka 2010 Taasisi kadhaa za kiislamu ikiwemo ya Sheikh Ponda zilisimama upande wa mgombea wa Ccm dhidi ya Dr.Slaa ila ilipofika 2012 walipishana na serikali na Ponda alikamatwa na kushtakiwa kwa uchochezi huku akipigwa risasi ya bega kule Morogoro.

Kiufupi hizi Taasisi za kidini zinaweza kutumika na Ccm muda wowote kulingana na upepo ulivyo.

Kuna viongozi wa Dini ya Kikristo pia walipingana waziwazi na TEC na kuishutumu vikali kwa kufanya Siasa baada ya ule waraka wao kuhusu mkataba wa bandari.
 
Sidhani kama Mkapa alichukiwa na Waislamu wengi bila sababu, sababu za msingi zilikuwepo ila labda dini ikaongezea uzito zaidi, pia nafikiri ni hivyo hivyo kwa Samia dhidi ya Wagalatia wasiomkubali.
 
Kumbe mpaka Ponda na taasisi yake waliwahi kuwa washirika upande wa CCM!🤣🤣
Walikorofishana nini na CCM vibaya hivyo mpaka wakawa mahasimu wa kudumu?
 
Kumbe mpaka Ponda na taasisi yake waliwahi kuwa washirika upande wa CCM!🤣🤣
Walikorofishana nini na CCM vibaya hivyo mpaka wakawa mahasimu wa kudumu?
Mwaka 2012-2014 liliibuka vuguvugu la Ponda na Sheikh Ilunga (Rip) waliokuwa wanapinga 'mfumo kristo'....

.hapo ndio kina Ponda na wenzake wakakutana na Rungu la Utawala waliouunga mkono kwenye uchaguzi wa 2010.

Kuna nyuzi nyingi sana humu JF kuhusu matukio ya kipindi hicho.
 
TEC nafikiri huwa wanakuwa katika dilemma kubwa, wanapenda Demokrasia lakini wanapenda zaidi mtu wao akiwa anatawala kitini, dilemma kubwa huwa inakuja pale ambapo mtu wao anatawala huku kuna ukandamizaji kazi ya kutetea democracy inakuwa ngumu, ikitokea anayetawala sio mtu wao kazi yao ya kutetea demokrasia na kutaka mabadiliko inakuwa rahisi sana.
 
Siyo ukweli. Unapotosha. Kenya, Zambia, Malawi wote walikuwa na vyama dola kama CCM na wamevitoa. Tatizo kubwa la Tanzania ni wananachi wenyewe. Hawajitambui na elimu inaweza kuwa sababu moja kubwa. Elimu kwa maana kuwa tunayosoma ni ya kukariri na kufanya mtu asiwe na upeo wa kuona mambo.
 
Ukitoa CUF na ACT ukweli ni kwamba majority ya opposition leaders wamejuwa ni Wakristo, iwe wakati wa Mkapa, Kikwete, Magu muuaji na hata huyu Bibi Kizimkazi muuaji. Kesi ya ugaidi Mbowe alipewa na Magu hivyo kusema eti Samia anachukiwa kwa sababu ya imani yake ni uongo wa wazi na upumbavu uliokithiri.
 
Waislam huwa mnakimbilia ACT na CUF na mmeona kuwa jambo hilo ndilo linawaangusha sasa mnaibambikizia CDM udini. Mmerogwa!
 
Unataka kusema enzi za awamu ya 5 walibaki kimya?...hapana sio kweli.

Walisema sana hata humu nyuzi za nyaraka zipo.

Uliloongea linaweza kuwa kweli kwa sehemu tu hasa hapo kupenda watoto wao wa seminary wakalie kiti ila kwenye kusema watasema tu (hili lipo pande zote sio TEC tu).

Siku ikipatikana regime yenye Rais Mkristo asiye Mkatoliki (mf. Mlutheri, Anglican, Msabato n.k) nadhani hizi myth nyingi mlizonazo kuhusu TEC zitakufa.
 
Kesi ya Mbowe ya Ugaidi hakupewa na Magu, hapa unamsingizia tu Magu (Rip).
 
Mama anasema wakati wake wametoa nyaraka 8.
Kwa Magu nakumbuka walitoa kama nyaraka 2 au 3 hivi😁
 
Ni nani katika uongozi wa CHADEMA ni Muislamu kwa sasa??
Ukiachana na ulemavu wa akili ulionao!....ulemavu wa udini utakutesa sana!

CHADEMA ni zaidi ya Dini!
CHADEMA ni Imani..iliyoko mioyoni mwa watu!

Huwezi kuwatenganisha watu wenye imani na hii taasisi... wanaojitambua kwa kigezo cha udini

#TokaPepo
 
Shida sio chadema, shida ni waislamu wa pwani wanaoona wanatoka ukoo mmoja na mwamedi 😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…