Ni wakati gani unaweza au kutoweza kuchanganya dini na siasa?

Ni wakati gani unaweza au kutoweza kuchanganya dini na siasa?

Dickson Ng'hily

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2010
Posts
451
Reaction score
485
Nimekuwa nikiwaza, kimyakimya....

Hivi siasa ni nini na dini ni nini?

Hivi ni wapi dini inachanganywa na siasa na ni wapi siasa inachanganywa na dini?

Hivi majukumu ya dini ni yapi na majukumu ya siasa ni yapi?

Hivi dini inafanyikia wapi na mipaka yake ni gani?

Na siasa je, inafanyikia wapi na mipaka yake ni ipi?

Hivi kuna eneo lolote ambapo dini na siasa au siasa na dini vinakutana na kufanya kazi pamoja kwa amani?

Hivi anayeonya juu ya kuchanganya siasa na dini au dini na siasa anatakiwa kutumia platform gani?

Ninaendelea kutafakari...
 
HAIWEZEKANI KUWATENGA VIONGOZI WA KANISA NA SIASA ZA NCHI YAO!

Wapendwa Watanzania!
Limekuwa ni jambo la kawaida kwa watawala au watu walio karibu na watawala wa Tanzania wakibanwa na viongozi wa dini hasa maaskofu huanza kutoa maneno ya propaganda dhidi ya viongozi wa dini wakiwaambia 'wasichanganye dini na siasa'. Msemo huu wanautumia kama kichaka cha kujifichia wasiguswe na viongozi wa dini!

Kauli hizo zimeibuka tena kwa kishindo zaidi kuanzia mwezi Juni 2023 baada ya maaskofu kuingilia sakata la Mkataba wa Bandari. Hivi karibuni tuliikemea Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilipoitisha mkutano wa viongozi wa vyama vya siasa ili kujadili hoja ya viongozi wa dini kuonekana wakiwa na viongozi wa vyama vya siasa.

Tumeona ni wajibu wetu ili kuwaelimisha watu kuhusu suala hili kusudi wasije wakapotoshwa na wanasiasa katika suala zima la kudai haki katika taifa lao. Wanasiasa ni wajanja sana na wanajua nafasi na nguvu ya viongozi wa dini katika jamii ndio maana wanatumia nguvu ili kupotosha ukweli kuhusu nafasi ya viongozi wa dini katika ukombozi wa kifikra katika taifa.

Tunapenda kukiri kuwa hili tunaloliandika ndilo eneo ambalo sisi tuna ubobezi nalo, kwa hiyo hatubahatishi bali tunakiandika tunachokijua, tulichokisomea na kukifundisha katika ngazi za Chuo Kikuu.

Kwa upande wa Wakristo, chimbuko la dini hiyo ni mji wa Yerusalemu, Israeli ya Kale. Lakini, ni vizuri watu wakaelewa kuwa Ukristo una mizizi yake miaka 5000 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Hivyo, msingi mkubwa wa mafundisho ya Ukristo ni Biblia Takatifu yenye sehemu kuu mbili - Agano Jipya na Agano la Kale.

Dini haifanywi kwa wanyama na wala siasa pia haifanywi kwa ndege. Dini ni mfumo mzima wa maisha ambao ndani yake kuna mambo mengi. Tunaposoma au kufundisha kuhusu dini lazima tusome maisha ya jamii nzima ambayo kwanza dini ilifika kwayo. Kwa upande wa Wakristo, sisi tunasoma kuhusu jamii mbalimbali kama Misri, Syria, Ukaldayo (Babeli), Rumi, Wagiriki, Jordan, Waisraeli, Waajemi, Waarabu, Lebanon, nk.

Katika kusoma na kujifunza dini tunafundisha waumini kuishi kwa mifano ya jamii hizo ikiwa ni pamoja na kuiga mema na kuyaacha mabaya na hayo yanawezekana tu kwa kusoma kuhusu maisha yao kupitia viongozi au manabii wao.

Tunaposoma na kujifunza Biblia tunakutana na mambo yafuatayo:
1. Familia (family institutions): familia, ndoa, watoto, wajane, urithi, kifo, maziko, nafasi ya wanawake katika jamii, nk

2. Taasisi za Kiraia (Civili institutions): idadi ya watu, utumwa, taasisi ya kifalme, familia za kifalme, utawala, ajira na uchumi, kilimo, Afya na tiba, sheria na haki, mgawanyo wa muda, vipimo vya uzito, mahakama, nk.

3. Taasisi za Kijeshi (military institutions): majeshi ya Israeli, ngome za kijeshi, mbinu za kivita, siraha za kivita, vita, vita vitakatifu, nk

4. Taasisi za dini (Religious institutions): ibada, madhabahu, nyumba za ibada, uongozi wa taasisi za dini, Ofisi ya Ukuhani, Ofisi ya Walawi, sadaka, imani potofu, uchawi, utaratibu wa ibada, siku za ibada, sherehe na siku za sikukuu, nk.

Watu waliokuwa juu ya yote hayo ni viongozi wa dini na ndio waliopewa majukumu ya kuifundisha na kuionya jamii. Taasisi hizo ziliwekwa kwa ajili ya watu na kilichotofautisha ni ratiba. Wakati wa vita walipigana na wakati wa amani watu hao walifanya sherehe. Wakati wa mambo mazito ikiwemo kujua mustakabari wa nchi walikwenda kutafuta ushauri kwa viongozi wa dini. Alipotokea kiongozi mkorofi au jeuri alikemewa na viongozi wa dini au hata kutangaziwa kuondolewa madarakani na hao viongozi wa dini.

Sisi Askofu Mwamakula tunaitoa kwenu elimu hii ili msiyumbishwe ili muelewe kuwa viongozi wa dini kuingilia kati mtafaruku wa kisiasa au kiutawala ni ishara kuwa jamii yenu iko na afya!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 20 Agosti 2023; 12:35 jioni.
 
Viongozi wa Dini ni Wananchi kama Wananchi wengine wana HAKI sawa kama wananchi wengine kwanini wanapotetea Nchi ndio waonekane wanachanganya Dini na SIASA? CCM acheni Unafiki
Maaskofu ni Wananchi BANDARI ni yao pia
 
Aisee
20230820_205804.jpg
 
Nimekuwa nikiwaza, kimyakimya....

Hivi siasa ni nini na dini ni nini?

Hivi ni wapi dini inachanganywa na siasa na ni wapi siasa inachanganywa na dini...
Dini inatumikia watu kimwili na kiroho, siasa inatumikia viongozi
 
1692650257759.png
Marehemu mchungaji wa kujipachika Getrude Rwakatare alipoteuliwa kugombea ubunge wa viti maalum kwa tiketI ya CCM, tulionya kuwa CCM ilikuwa inachanganya dini na siasa. Mara akaja mchungaji na tepeli jingine la kujipachika au mchunaji aitwa Gwaijumaa. Mpaka leo ni mwishiwa wa Chama Cha Mapezi. Hapa hakuna kuchanganya dini na siasa kwa sababu dini na siasa vyote ni mali ya CCM.

Akitokea mtu ambaye ima ni kiongozi wa dini au anafungamana nayo akaikemea CCM kama walivyofanya maaskofu, utasikia hata vichwa vya panzi vikiseme msichanganye dini na siasa. Je ni wakati gani unapoweza au kutoweza kuchanganya dini na siasa? Je ni pale unapokuwa ndani au nje ya CCM?

Je, unahitaji kibali toka serikalini ambacho CCM inacho kwa sababu ndiyo inayounda serikali? Je inakuwaje rais anapoapishwa akabeba misahafu ya kidini akiombewa na viongozi wa kidini isiwe kuchanganya dini na siasa?

Je, kiongozi kiongozi wa serikali anapokwenda kuhudhuria kusimikwa au kuapishwa kwa kiongozi wa kidini siyo kuchanganya dini na siasa? Je dini na siasa siyo kitu kimoja ambacho asili yake imekichanganya? Je unaweza kuepuka kuchanganya dini na siasa hata kama nchi siyo theocracy kama Iran na Saudia?

Sijui wewe mwanangu unashaurije hapa?

1692650335496.png
 
Huu msamiati kwangu ni mgumu mno kuulewa, pengine kwa sababu elimu yangu ni ya kawaida.Hivi kwa nini? Viongozi wa kiroho huwa wanawapa nafasi ya kuongea kanisani viongozi wakubwa wa kiserikali? Je?

Kwa Mungu kuna mkubwa na mdogo au kwa Mungu pia kuna mheshimiwa na asiyekuwa mheshimiwa?.Kwa mawazo yangu mimi mbele za Mungu tuko sawa.

Kwa kuwa viongozi wa siasa wakati wanapopewa nafasi ya kuongea huwa wanaongea maneno ya dini tu ? Au wanaongea ya kisiasa?. Je Nani huwa anachanganya dini na siasa? Kati ya viongozi wa kiroho na wale wa kisiasa.
 
You can fool some people sometimes, but you can't fool all the peoples all the time

Nyie baraza wacheni kabisa kujidai mnasemea watu wote wakati hata wengi hawawajui, msilazimishe mambo, haya mnayoendeleza ni chokochoko za uvunjifu wa amani

Kikisanuka hapa hatutawaona mjueeee, Enzi ziliisha na hii ni dalili ya anguko rasmi Ngoja tuone kama kweli uhuru unazingatiwa
 
....... all peoples ......

basi sawa
You can fool some people sometimes, but you cant fool all the peoples all the time

Nyie baraza wacheni kabisa kujidai mnasemea watu wote wakati hata wengi hawawajui, msilazimishe mambo, haya mnayoendeleza ni chokochoko za uvunjifu wa amani

Kikisanuka hapa hatutawaona mjueeee,
Enzi ziliisha na hii ni dalili ya anguko rasmi
Ngoja tuone kama kweli uhuru unazingatiwa
all peoples .....

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Hivi unadhani kama sio chokochoko ni nini?
Na mmeshaambiwa msichanganye dini na siasa?
Kuendelea kuwasomea watu manatafta nini?

Sasa na wewe usichanganye dini na siasa yamesomwa kanisani yanakuhusu nini ya kanisani? Em tulia mkuu hakuna wakukiwasha kwenye hii ichi ila unatakiwa kujua mkataba ni mbovu na tumeugomea.....

wewe ukubali na ukiwa uko ulipo waambie umeukubali....
 
You can fool some people sometimes, but you cant fool all the peoples all the time

Nyie baraza wacheni kabisa kujidai mnasemea watu wote wakati hata wengi hawawajui, msilazimishe mambo, haya mnayoendeleza ni chokochoko za uvunjifu wa amani

Kikisanuka hapa hatutawaona mjueeee,
Enzi ziliisha na hii ni dalili ya anguko rasmi
Ngoja tuone kama kweli uhuru unazingatiwa
Rudisheni mlichokula!!

Usicheze na nguvu ya Umma.
 
Sasa na wewe usichanganye dini na siasa yamesomwa kanisani yanakuhusu nini ya kanisani? Em tulia mkuu hakuna wakukiwasha kwenye hii ichi ila unatakiwa kujua mkataba ni mbovu na tumeugomea.....

wewe ukubali na ukiwa uko ulipo waambie umeukubali....
Umenena kweli kiongozi. Na kama huyo mnayemwita mama yao anaweza, wamwambie awaambie TEC wasisome huo waraka makanisani.

Hiyo remote yao yenyewe inaijua nguvu ya TEC na inaiogopa.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
You can fool some people sometimes, but you cant fool all the peoples all the time

Nyie baraza wacheni kabisa kujidai mnasemea watu wote wakati hata wengi hawawajui, msilazimishe mambo, haya mnayoendeleza ni chokochoko za uvunjifu wa amani

Kikisanuka hapa hatutawaona mjueeee,
Enzi ziliisha na hii ni dalili ya anguko rasmi
Ngoja tuone kama kweli uhuru unazingatiwa
acha ujinga,baraza sio basuta.
 
Back
Top Bottom