Labda umvivu wa kusoma, wengi wamezijibu na hata serikali wameeleza lakini kwa kuwa ni agenda rasmi basi kila mbinu inatumiwa kupinga,
Tukirudi kwenye matusi ni nyie ndio mnatukana, kama huyo hapo juu anmwambia rahisi eti hela ulizokula utazitoa kupitia tundu ya mwili, hii imekaaje? Najua kwa kuwa ni mwenzenu utasema hakuna tusi hapo, nitakupa mfano wakati flani wakati wa utawala wa nyerere kuna wajumbe walidai tanganyika, sasa nyerere kwa uhodari wake akawauliza kwani moja na moja ni ngapi? Walivyomjibu ni mbili akasema basi ni serikali ya muungano na serikali ya mapinduzi zanzibar yukiweka Tanganyika itakuwa tatu,
Nadhani hapo umepata majibu ya kwanini mnsimamia upingaji wenu?
Hata kama manufaa yatarudi kwenu
Rais na aheshimiwe hata kama sio mkiristo
Kwanza umeanza kwa kunisemea kitu ambacho si sahihi.
Turudi kwenye hoja ya msingi hili swala linapingwa na makundi yafuatayo
1. Baadhi ya wanasiasa
2. Baadhi ya wanasheria
3. Wanachi wa kawaida mbalimbali
4. Baadhi ya viongozi wa dini (TEC)
Tamko la TEC halina tusi hata moja wala halisa kejeli yoyote kama ipo nioneshe. Nitafurahi endapo utanithibitishia kua kuna kiongozi wa kikristo alikosoa kwa kutukana/udini au ukanda/ukabila.
Ajabu ni kuwa TEC wametoa msimamo wao hapo ndipo mkaingiza swala la udini. Kitu ambacho TEC walitoa msimamo wao kama wanavyotoa mara kwa mara.
Hivi ndugu vifungu vya sheria unafafanua kwa kupiga story ?
Watu wanasema mkataba hauna ukomo,badala ya kuonesha kifungu kinachoonesha ukomo ili wakae kimya watu wanatukana na kutishwa.
Hoja nyingine inayolalamikiwa ni ile ya kuipa Tanzania wajibu na kuipa DP World haki. Kuwa wakitaka eneo wapewe tena bila fidia,je kuna kifungu ndani ya mkataba kinachofafanua tofauti ?
Haya uhalisia unaanza kuonekana leo hii sheria ya Nchi ya kulinda rasilimali zinataka kubadilishwa ili ziendane na mkataba. Hivi ni ipi ilipaswa kufuata mwenzake, mkataba kufuata sheria za Nchi au Sheria za Nchi kufuata mkataba ?
Ukweli ni kuwa kwenye sheria kinachokufunga ni maandishi (mkataba uliosaini) sio story za kujetetea.