Sasa hapa ndiyo umeuliza swali la msingi na ume quote kwa usahihi.
Ni kweli, Papa amesema Mashoga wabarikiwe, siyo mdoa, bali mashoga.
Lengo la kuwabariki ni kuwaweka karibu na kanisa badala ya kuwatenga. Kanisa halipaswi kuwatenga wadhambi bali linapaswa kuwakusanya ma kuwakumbatia. Maaba ya kubarikiwa.
Fundisho linasema yeyote anaweza akaomba baraka, katika utoaji wa baraka Padre anajua anachopaswa kufanya. Anawaweza akawabariki ili Mungu awaangazie waweze kuitambua kweli na kuiishi.
Je, kuna kosa kumuombea mdhambi au kumbariki mdhabi aweze kubadilika?
Ieleweke, hata iwe vipi, Padre hawezi akatoa baraka iliyo kinyume na mafundisho ya Mungu na Kanisa.
Mafundisho ya Kanisa juu ya ndoa yanajengwa katika Msingi wa Uumbaji. Ambapo Mungu alimuumbwa mwanaume, halafu akamuumba Mwanamke. Mafundisho na Sheria ya Kanisa havikuwahi kubadilishwa kuhusiana na ndoa. Hivyo basi padre hawezi akabariki ndoa ya watu wa jinsia moja. Siyo hao tu, Padre pia hawezi akabariki ndoa ambayo mwenzi ana matatizo ya akili, au ndoa ya ndugu wa damu.
Vyombo vya habari vinaruka ku report ufafanuzi unaotolewa, vyenyeww vinaenda kutengeneza taarifa ya kuonyesha kuwa Kanisa limeanza kupingana.
Nadhani nimejaribu kuelezea.