Ni wakati wa "system" kutumia mbinu zao zote kukwepa hii mitego miovu ya WEST (US) kuhusu nchi yetu.

Ni wakati wa "system" kutumia mbinu zao zote kukwepa hii mitego miovu ya WEST (US) kuhusu nchi yetu.

Wakuu kwa sasa sio siri tena kwamba wamarekani wanasukuma kete zao kwa umakini mkubwa kutimiza agenda zao ovu dhidi ya nchi yetu. Hakuna kinachotokea kwa bahati mbaya hadi sasa. Martha Karua, Boniface Mwangi na hao wanaharakati wengine wanatumika tu kwenye hii mikakati ya wamarekani. Tayari US imetoa tamko la kutaka uchunguzi ufanyike. Kwa miaka mingi Tanzania imekuwa ngumu kuingilika ila kwa hali ilivyo inabidi kazi kubwa ifanyike kukwepa hii mishale.

Kwa wale msiojua balaa la CIA nendeni mkachimbe kuhusu muungano wetu uliounda Tanzania. Huu muungano ni wa kupikwa na hao majamaa kutokana na tishio la Zanzibar kuangukia mikononi mwa wakomunisti. Pia someni kitabu cha Amos Malupenga kinachoitwa CONVERSATION WITH MEMORABLE PERSONALITIES, Page 62 - 76. Kwenye hizo page mwandishi alimhoji hayati Dr Kamoyo Mwale aliyekuwa mkuu wa idara ya usalama Zambia. Dr Mwale anasema kuwa mwisho wa ubaguzi wa rangi na kuachiwa kwa Mandela ilikuwa mipango ya CIA na sio kwamba weusi walishinda dhidi ya weupe. Ni CIA kwa maslahi yao waliamua. Lakini kabla ya Mandela kuachiwa makaburu waliweka sharti la hayati Kaunda kung'olewa madarakani kwa hofu kuwa ataungana na serikali mpya ya weusi kuwasulubu weupe. CIA kupitia Chiluba na vibaraka wengine walipiga fitina ya balaa na Kaunda akapoteza urais kupitia sanduku la kura mwaka 1991. Ikumbukwe hayati Nyerere alishang'atuka miaka 6 kabla (1985).

Dr Mwale anadai kuwa serikali ya Kaunda ni kama ilishatolewa madarakani miezi 6 kabla ya uchaguzi mkuu. Binafsi nikiangalia kinachoendelea nchini ni kama kuna watu wanatumika kumhujumu mama. Kwa mfano kulikuwa na haja gani ya kuwakamata wanaharakati na kuwapa kichapo kisha kuwatupa huko mipakani? Si wangewarudisha tu makwao kwa amani na kutoa tamko la kidiplomasia kuhusu kuwarudisha. Kilichofanyika kinamchafua mno mama badala ya kumng'arisha.

Kwa leo vyombo vyote vikubwa vya habari vya magharibi vinaandika kuhusu tamko la US. Dr Jakaya na manguli wengine wa diplomasia ingilieni kati kuhusu hawa wahuni wanaomharibia Mama kwa kupiga, kuteka na kupoteza watu. Hakuna faida yoyote kwa nchi kupitia hayo matendo ya kihuni.
Hakuna cha CIA au FBI wala MOSAD au TISS. Lissu alikamatwa kwa maagizo ya USA ? Kesi kuendeshwa online ni maagizo ya USA? Kuteka na kuuwa watu ni maagizo ya CIA. Waafrica, watawala hawataki kushindwa kwenye sanduku la kura. Wanatumia polisi na majeshi kubaki madarakani halafu mnawasingizia CIA.
 
Polisiccm na chawaccm kuonea kuteka kuua kuwabambikia kesi chadema ndiyo chanzo cha wapigania haki kuja Tanzania siyo marekani
Mimi mejibu hoja ya kuwa Marekani mewatuma akina Martha na Mwangi kuja kuharibu hali ya kisiasa.. Ndo nkasema huo ni uongo kwasababu paka hapa tulipo hakuna maslahi yao yoyote yaliyoingiliwa...
Siku tukikaziba hako kamrija kao ndo taona wanavyotumia hiyo phrase "HAKI ZA BINADAMU" kuing`oa CCM..
 
Back
Top Bottom