Ipo ile ya matonya album ya kwanza yupo yeye,bluu na mtu kama dark master- Mwanachemba ,sema mashairi yake mistari inaruka ila kuna....'chombeza,poteza,mapombe makali tunawafundisha kumeza!
 
Hivi Hawa wasanii hawajui wamekalia hela kiasi gani tu..Wakiamua kufanya tours watafunika mbaya.Hizi nyimbo zao hazichuji kabisa.

Wakiandaa matamasha ya hip hop watajaza mpaka watashangaa.Yaani siku hizi wapenzi wa ngoma kali hatuna pakwenda.Utakutana na wabana pua Mara Nyegezi nyimbo hata hazieleweki.Ujinga ujinga tu.
 
Mkuu gwankaja Hivi hii ngoma Pengo haikufanywa Mara 2 kweli? Kundi lilipovunjika Waswahili wakatoa version Yao na Wengine nimewasahau wakatoa Yao?

Zote zilikua kali sana..ubunifu wa kiwango kikubwa.
Ya Mike T ni Nyaluland...

Uko sawa Sonel ndo aliimba Posta

Pengo ya Waswahili moja ya ngoma bora sana toka kwa hawa jamaa
 
Dah, Huyu jamaa ni google ndogo aisee nimefanikiwa kupata nyimbo nyingi kutoka kwake.

Mkuu natanguliza shukrani nyingi sana kwako na mkuu KIOO aisee mmenisaidia sana wakuu.

Much respekt kwenu wakuu.

👊🏽👊🏽👊🏽
Bahati mbaya uko mbali.
Nina mizigo yote ya bongo flava tangu enzi za akina II Proud mpaka akajiita Sugu, GWM, Balozi, Mr. Paul nk. Ngoja nirushie screen shots. Sijajua utapataje hizi nyimbo
 
Ile track nadhani inaitwa Msela
 

Aiseeee, wee jamaa una hatari sana mkuu.

Natumai utakuwa ni mmoja kati ya MA-DJ waliopo kwenye radio moja kubwa sana mkuu.

Ntakuwa nakosea sana kama sitasema HESHIMA KWAKO MKUU ntakuwa ni mchoyo wa fadhila aisee.

Kwa kuanza tu kwanza naomba hiyo ngomae Mr.Prezzo G aisee. Ni hatari sana hiyo ngoma bro. Ni ya moto zaidi ya band mkuu.

Thanks a lot bro.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…