Wimbo wenyewe ni wa muda na una maneno yafuatayo;
"Siyo kusema kuwa nakupenda saana. Lakini ni nani wa kusema kuwa sikupendi.
Hayo ni maumivu ninayosikia, ninayosikia tuwapo mbali mbali.x2
Mimi naelewa kuwa ni makosa kuwa mbali mbali muda mrefu. Nikamwambia kila anaye kuhusu nikakupigia pia hata na simu."
Nimemtuma kaka Jesca akakutafute kwa marafiki zako. ..........
Nimeenda galaxy, msikitini. .....Magomeni mapipa..... kote huko sikufanikiwa kumuona dada.
Hayo ni maumivu ninayosikia, ninayosikia tuwapo mbalimbali.x2
Naomba msaada kwa anayeufahamu jina na bendi iliyouimba tafadhali
Natafuta nyimbo moja ya kibongo siijui jina lake lakn kuna video vixen mmoja anacheza balaa nyimbo ina mandhari ya nyimbo ya davido aye wapo mashambani hivi jamaa kama kafanana na matonya hivi, Anaejua jina la huu wimbo wadau nitashukuru!
Sijui kama nimekosea jukwaa ama nipo sawa. Kama nimekosea mods fanyeni makeke yenu.
Natafuta sana wimbo fulani sikumbuki uliimbwa na kwaya ipi, wala jina lake. Naomba aliye nao au anayekumbuka jina anisaidie.
Wimbo unaanza na maneno haya:
Vilio vimeenea, huzuni nayo yatanda...
Kwa ndugu zetu Albino, hawana amani...
Wawindwa kama wanyama, eti kisa mali...
Jamani sasa ndugu zangu, tumefika mbali...