Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Wimbo wa Unique sisters unaitwa "sikutaka" original version
 
Naomba kama kuna aliye na wimbo "Club 53" wa TP Orchestra Kinshasa Jazz ya marehemu Franco Luanzo Luambo Makiadi.
 
Zilipendwa flan ivi unaimbwa "ilooo ooh, ukijifanya mjanja sana, aibu imekushika, kiko wapi. ." anayefahamu waliomba plz ntajie nigugo au km unao itkua poa sn
[HASHTAG]#zilipendwa[/HASHTAG]
 
Wimbo wenyewe ni wa muda na una maneno yafuatayo;
"Siyo kusema kuwa nakupenda saana. Lakini ni nani wa kusema kuwa sikupendi.
Hayo ni maumivu ninayosikia, ninayosikia tuwapo mbali mbali.x2

Mimi naelewa kuwa ni makosa kuwa mbali mbali muda mrefu. Nikamwambia kila anaye kuhusu nikakupigia pia hata na simu."

Nimemtuma kaka Jesca akakutafute kwa marafiki zako. ..........

Nimeenda galaxy, msikitini. .....Magomeni mapipa..... kote huko sikufanikiwa kumuona dada.

Hayo ni maumivu ninayosikia, ninayosikia tuwapo mbalimbali.x2


Naomba msaada kwa anayeufahamu jina na bendi iliyouimba tafadhali
 
Natafuta wimbo Machozi Jasho na Damu wa Prof Jay, Sekuntonza wa Juwatta/Ottu Jazz Band na Ujana Maji ya Moto wa Vijana Jazz Band.
 
Kuna wimbo fulan i think ni wa kimarekani. Kwenye chorus kuna mstari unasema God is girl. Nautafuta sana.

Pia kuna wimbo JB mpiana unaitwa Binadama if am not wrong. Nao nausaka kwa muda bila mafanikio
 
Hongera sana kwa msaada wako. Mungu akubariki.

Nisaidie nyimbo hizi.
1.Bushoke_Mpenzi Christina.
2.Bushoke. Neema.
3. Papii Kocha ft. Jay dee_ Usiutupe moyo wangu.
4.Zigy dee_Enomike
 
Natafuta nyimbo moja ya kibongo siijui jina lake lakn kuna video vixen mmoja anacheza balaa nyimbo ina mandhari ya nyimbo ya davido aye wapo mashambani hivi jamaa kama kafanana na matonya hivi, Anaejua jina la huu wimbo wadau nitashukuru!
 
Habari zenu wapendwa?

Sijui kama nimekosea jukwaa ama nipo sawa. Kama nimekosea mods fanyeni makeke yenu.

Natafuta sana wimbo fulani sikumbuki uliimbwa na kwaya ipi, wala jina lake. Naomba aliye nao au anayekumbuka jina anisaidie.
Wimbo unaanza na maneno haya:

Vilio vimeenea, huzuni nayo yatanda...
Kwa ndugu zetu Albino, hawana amani...
Wawindwa kama wanyama, eti kisa mali...
Jamani sasa ndugu zangu, tumefika mbali...


Shukran.
 
Back
Top Bottom