Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Chorus inaimba ¶ ...hawatufundishi uwoga ..¶

verse .. mishe mishe ndo zilizofanya tusionane....

Ni hip hop ya Arusha mdada anaimba kiitikio, siku mbuki ni jombii kaimba au chindo .

Mwenye kuijua anijuze pls sana
Right Here - G Nako ft Chindo & Banks
 
Jamani natafuta ule wimbo unaopigwa redio Deutsche welle siku ya jumapili mchana kwenye makala ya Africa wiki hii!
Mtunzi/msanii aliyeuimba simfahamu, lakini kwa wafuatiliaji wa hiki kipindi huwa unapigwa mwanzoni na mwishoni mwa kipindi kama kibwagizo! Nakumbuka baadhi ya mashairi yake " oooooooh! Africa.... Oooooh Africa piavipambaaaa..….." Huko mbele siuwezi kuuimba vizuri hivyo Mwenye nao masaada please.
Huo wimbo unaitwa "Afrika liberté " kaimba franklin boukaka
 
Natafuta wimbo wa hipo ya zamani kidogo. Maneno ya Chorus yake ni
"Nimepita kote kutafuta life, Nikaona Bora niende Bongo huenda ikawa shwari"

Naomba anaye faham hata aliyeimba anipe Jina au wimbo wote.
cheki hapo juu
 
Aaah Joanita,
Unajua mimi ni mbeba zege tu
Miezi sita
Nataabika ili niwe na wewe tu

Huu wimbo sijui unaitwaje nimeutafuta sana. Rapa flani ana rasta na kama sikosei Pasha anaimba hiyo chorus...
Pingu Na Deso ft Me Blue- Joanita
 
Natafuta Audio ya Banana Zorro wimbo "nataka niwe na wewe mpenzi wangu kila siku ..lakini tatizo huonekanii..."
 
Kwa mwenye uhitaji wa nyimbo za zamani (1990 - 2010) za Bongo Flavor anicheki kwa namba hizi 0682277495 nitamuunga katika magroup ya maktaba ya nyimbo hizo.

Tumia no hizo kwa WHATSAPP / TELEGRAM ONLY
 
Kuna wimbo kaimba msanii wa kike japo sio wa zamani Sana ila vionjo vyake ni kama anamwimbia mpenzi wake akimsisitiza kwamba ni yeye anamfanya awe karibu yake. Sauti ya huyo msanii ni kama ya jovial ingawa nimetafuta Sana bila mafanikio. Mwenye kuufahamu huu wimbo?
 
Back
Top Bottom