Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Huu ni uzi maalum kwa MwanaJF kutoa Wimbo wake ambao amekuwa akiutafuta kwa miaka mingi, Bila ya Mafanikio. Kwa yule aliyenao anaweza kumsaidia mwenzie kwa kumtumia wimbo huo hapa.

Miaka ya 2004 Kuna familia moja ya Baba Mama na Watoto wao kama Sita walikua wanazunguka mitaa ya arusha wakiimba nyimbo za gospo na kuuza kanda (cassette) za nyimbo zao . Nilizipenda sana. Mtoto wao mmoja wa kiume ndio alikua w
anapiga kinanda (keyboard). Nyimbo zao nazikumbuka sana ila nilipoteza kanda (cassette) yao na kipindi hicho hakukuwepo na youtube. Kama kuna mdau yeyote humu ana kanda (cassette) yao aniite popote nitaifuata na nitainunua kwa bei yoyote. Mungu awabariki wakuu.!
 
Dully sykes. Dada mwajuma , it goes paraparipa papapaa paraparipaa paa..
 
Wakuu natafuta nyimbo zifuatazo
1. Wakati Umelala wa Mwana Fa, Imam Abbas na Mangustino
2. Niamini wa Banana Zorro
3. Mtumishi wako wa Mike T, Banana Zorro na Mwana Fa
Mwenye nazo aziweke na ninaomba anitag
 
Anaejua msanii au nyimbo yenyewe ya "Acha Nikupende" iliyokumika kama soundtrack kweny series ya ZAHANATI YA KIJIJI naomba anitajie! Au anielekeze namna ya kuipata
 
Kuna ule wimbo unaimbwa hivi..
🎶"Tulikutana ki mjini mjini"🎶
Halafu Kuna ule
🎶"Inama inuka eeh naangusha Moja moja Leo"🎶
Halafu Kuna ule
Unaimbwa ivi
🎶"Kama wanipenda nipe mgongo nipande unibebe mpaka kwa mama ukinifikisha ntafurahi Sanaa"🎶
 
Kuna ule wimbo unaimbwa hivi..
🎶"Tulikutana ki mjini mjini"🎶
Halafu Kuna ule
🎶"Inama inuka eeh naangusha Moja moja Leo"🎶
Halafu Kuna ule
Unaimbwa ivi
🎶"Kama wanipenda nipe mgongo nipande unibebe mpaka kwa mama ukinifikisha ntafurahi Sanaa"🎶
Huo wa inama inuka naangusha moja moja, nahisi ni twanga pepeta, enzi za Ali Choki
 
Back
Top Bottom