habari Wakuu, natafuta nyimbo hizi za kibongo za kitambo kidogo:
1. Block 41 Legendary wa Kalapina + Members wengine wa Kikosi cha Mizinga (beat yake inasikika background kwenye ile clip ya video ya show ambayo Kalapina alimshusha jukwaani Chidi Benz: "ASIYEHUSIKA NA SHOW ASHUKE" show.
2. Wimbo wa dada mmoja simfahamu kwa jina ila una maneno haya "give me some money hebu acha utoto . . . kajileta letaaaa, nasema kajileta-letaa"
3. Kuna member mmoja wa kundi la Wakali Kwanza, alifahamika kwa jina la Lil' Grey, wimbo unaitwa Jiamini tu Mi Nataka Kuwa na Wewe (sina uhakika sana na hili jina la wimbo, lakini maneno hayo yanasikika kwenye kiitikio chake)
4. Wanashangaa wa JCB kamshirikisha Nakaaya, na Jay Moe.
5. Kuna wimbo kafanya dada flani unaanza na maneno "Mara simu, mara mesejiiii . . . ni kweli kwamba sasa yatosha; ulivyoniadhibuuuu bila sababu mimi . . ."
Natanguliza shukrani kwa yeyote mwenye wimbo wowote kati ya hizo, na pongezi nyingi kwa sharings zote zilizofanyika kwenye hii thread tangu ilipoanzishwa!!!
KIOO Idimi