Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Mwenye nazo hizi nyimbo anipatie,nilikuwa nazo kuna mbweha akaformat HDD bila kuwa makini na partition.

1.Unique sisters ft Mac D - Bounce (Usiku bado mchanga)

2.Nyimbo za Mzee Makongoro (Dereva kalewa Gongo sawa hiyo na Kuleni kuku mayai nyama Samaki maziwa)

3.Crazy GK ft Fina Mango - Mama

4.Nyimbo za Marehemu komba zote alizoimba 1999 kwenye kifo cha Nyerere.

5.Patrick Balisidya - Wema hawana maisha (Sio Wa YouTube,nataka full Audio)
 
Mi natafuta za Justin kalikawe,Nyimbo za komba alizoimba kipindi cha Baba wa Taifa na wimbo fulani wa zama zile sijui mwimbaji wake labda ninukuu kipande cha maneno,usiibe ukiiba weweee utafungwa bureee
 
Mimi natafuta nyimbo mbili lakini sijui zinaitwaje na wala kaimba Nani.mmoja una kipengele kinaimbwa_ Mjini umekuja juzijuzi kwenu ulikuwa unafuga mbuzi.sikujua kuwa ni nuksi mpenzi umemkuwadia mdosi._mwingine kuna kipengele kiko hivi= Hoi hoi hoi mimi naliaa Hoi hoi hoi parapanda italia. Yaani nazitafuta sana
Suma Lee wimbo unaitwa Rafiki
Upo YouTube
 
Back
Top Bottom