Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Kuna nyimbo inasema,mshesha kakimbia na ela ya posa na hawezi kwenda police kwa kuwa hamjui....naomba jina tafadhali
 
Natafuta Wimbo wa Senzo-Rasta Wakeup.


Pia Wimbo unaitwa Kiranga..Ulikuwa katika mahadhi ya Taarabu, kundi nadhani Zanzibar Miaka ya 200s Mwanzoni.

Mashairi yake kidogo kwa kumbukumbu ya mbali:

"Anakiranga huyo
mwana huyo anakiranga,
anakiranga mpeni dawa anywe,
Apate tuliza roho anakiranga,"


Pia na Wimbo wa kundi hilo hilo..unaitwa Mageuzi kama sjakosea..

Mashairi kwa uchache kwa kumbukumbu zangu.

"Ndugu zangu wananchi tukubali mageuzi,Tusiuze nchi yetu huo sio uchaguzi,Huo Uchaguzi."


Shukranii
 
Kuna taarabu za zamani sana kama sikosei waliimba TOT

Inasema nimepata wangu fundi, amepima bila hofu, amepima kiufundi upana hata marefu.

Alafu, dereva wangu tulia hapa kwangu umetua. Ile albam ilikiwa moto miaka ya 92/93

Alafu, dereva wangu tulia hapa kwangu umetua. Ile albam ilikiwa moto miaka ya 92/93


Never say more than is necessary.:msela:
 
Natafuta wimbo wa hk alimshirikisha ester wasira unaitwa umerudia tena. Pia mwenye wimbo wa Pauline Zongo unaimbwa hv nimeshindwa kuvumiliaaa chenye mwanzooo hua na mwisho wakee
 
Wazee natafuta wimbo wenye baadhi ya maneno yafuatayo...
uwezo sina ningekujengea nyumba...
uwezo sina ningekununulia gari......
uwezo sina ningekunulia mtumbwi ukavue samaki.....
bali matatizo madogomadogo hayatonishinda... sababu jungu kuu halikosi ukoko.
Akiba yangu ya mapenzi nakupa wewe...

Naomba kujua walioimba huu wimbo angalau nijue pa kuanzia...
 
Les Wanyika _ BARUA. Video yake kila nikitafuta siipati hasa yenye ubora unaotazamika vizuri
 
Wakuu naomba wimbo flan wa taarabu uliimbwa na Mwanahela unaitwa sege sege
 
Naombeni wimbo wa mdada flani, simkumbuki jina chorus yake iko hivi

""Nitalia, nitazimia ntaposikia nimeunganishwa na jina lako""
 
nimeupata kipande huu wimbo kama unaujua au unao please do share nimeutafuta sana na hapa kuna mtu aliusikia mahali akanitumia. Ni wimbo wa gospel unaelezea yesu na wale wezi wawili pale msalabani. Kama unao au unwajua waimbaji nisaidieni nitashukuru sana.


Hivi ni dharau au ama ni nini? Yaani hakuna anayeufahamu huu wimbo kabisaaaa
 
Back
Top Bottom