Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Huu ni uzi maalum kwa MwanaJF kutoa Wimbo wake ambao amekuwa akiutafuta kwa miaka mingi, Bila ya Mafanikio. Kwa yule aliyenao anaweza kumsaidia mwenzie kwa kumtumia wimbo huo hapa.

wimbo ninaoutafuta mimi lyrics zake ni "samahani dada naomba namba yako moja tu, nataka kuongea mimi na we, nataka nikueleze jinsi gani ambavyo mi, moyo unapenda kuwa mimi na we, we dada weeeeee, unanifanya mi nakosa raha, ni we dada wewe, sababu mi nakupenda sana"
nimesahau maneno vizuri, wa zamani sana, jina sikumbuki muimbaji sikumbuki
 
wimbo ninaoutafuta mimi lyrics zake ni "samahani dada naomba namba yako moja tu, nataka kuongea mimi na we, nataka nikueleze jinsi gani ambavyo mi, moyo unapenda kuwa mimi na we, we dada weeeeee, unanifanya mi nakosa raha, ni we dada wewe, sababu mi nakupenda sana"
nimesahau maneno vizuri, wa zamani sana, jina sikumbuki muimbaji sikumbuki
Hii nyimbo ya Ngwair. Dakika moja. Iko Album ya Nge
 
Natafuta wimbo mmoja hivi naupenda sana japo sijui ameimba nani...

Jamaa analalamika sana kwamba baba yake anampiga kwa fimbo mbele ya mkewe. Anahuzunika sana kisha anauliza baba kama ulijua mimi ni mdogo sasa kwanini uliniozesha

(anachanganya na lugha fulani ya kikabila nadhani ni kisukuma na hata mahadhi ya wimbo yamekaa kisukuma)
Mwimbaji anaitwa bhudagala, wimbo nimeusahau jina..
 
Kuna ngoma flani hivi chorus kaimba Jay mo sijakusa inaitwaje nimeisaka sana..... Chorus iko hivi

"Mi nakomaa na Wala sijali vile wazushi wanavoshangaa.... Rijali lazima utoke jasho mi nakomaa nakomaa"

Pia nikipata shega tu ya darkmaster
 
Anayeufahamu wimbo unaotumika kama soundtrack kwenye tamthilia ya uzalo.....Nautafuta
 
kuna wimbo

"kila leo napofikiria, pigo gani litaacha historia, awe kiongozi awe rai, ......."

inaongelea mambo ya viongozi kufa, ya zamani.

Nipeni hii pini
 
Wakuu naombeni mtuvanisaidie kuupata wimbo wa GOSPEL wenye maneno haya" Nitalitaja taja jina laako, kila mara nitarefresh, kwenye ukuu wa mbawa zako, nitaenjoy, kwa maana umeniona"""
 
Kuna wimbo fulan wa bend hv ya zamani baadhi ya kipande chake kinaimba hv
"...... Kushindwa kutoka ahhh hapa nyumbani.. najuta eh najuta nimekosa najuta eh najuta nisamehe...
Fikiri naomba unisamehe kushindwa kutoka ahhhapa nyumbani......."
Msaada wakuu
 

Attachments

Back
Top Bottom