Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Naomba mwenye wimbo wa Mayday na Service zote za Fally Ipupa pamoja na Give me some sunshine wa Suraj Jagan & Sharman Josh.
Natanguliza shukrani!
Ingia juice mp3 utapata nymbo zote.utakuja kunishukuru.mm natafuta wimbo wa tuwaheshimu wazazi baba na mama pia wa ommy belima miondoko ya kaswida nimejaribu kutafuta bila mafanikio
 
Wakuu kwema?? Mwenye nyimbo ya Langa ft shaa inaitwa mtima nyongo nadhani please share
 
Kuna wimbo wa dini kwa mwaka 2021 au 2022 ulikuwa unapigwa katika stesheni ya redio ya Mwamposa...
Katika kiitikio ulikuwa na maneno
"Inuka sasa na uangaze, huu no wakati wako..."
Sikumbuki mistali.
Ila umeimbwa na Mwanamke
 
Natafuta wimbo......
Baba niipe Roho waako
Aniongozeee anifundiishe.....sijui nani wameimba una mahadhi ya bondeni
 
Kuna wimbo ameimba dj yusuph alieimba mbele kwa mbele,kama kuna mtu anao auweke hapa tuburudike na huyu msela wa marekani aliyeikataa bongo.
 
Hizi hapa kijana. Enjoy
Kuna radio nasikiliza nikakutana na nyimbo ya Mr ebo ikabidi nitulie nisikilize ...

Asee udongo umekula kichwa tungekuwa nacho mpaka leo daa RIP Mr ebo tungo ya hio nyimbo ya sitaki tena pombe sio ya kawaida

Ikabidi Ni search Mr ebo jamiiforum nione Kama alishaongelewa ndo nikakutana na huu uzi
 
kuna kwaito moja hivi sijui ya kisauzi corus yake kuna maneno kama "chali nnakukuna anasuu chali nakukuna ""sjui ndo hivyo 😁😁😁
 
Kuna radio nasikiliza nikakutana na nyimbo ya Mr ebo ikabidi nitulie nisikilize ...

Asee udongo umekula kichwa tungekuwa nacho mpaka leo daa RIP Mr ebo tungo ya hio nyimbo ya sitaki tena pombe sio ya kawaida

Ikabidi Ni search Mr ebo jamiiforum nione Kama alishaongelewa ndo nikakutana na huu uzi
JF ni hazina kubwa sana. Mr. Ebbo kwenye album yake ya Fahari yako aliimba mambo mengi ya msingi sana. Mungu amjalie pumziko la milele
 
Natafuta nyimbo kaimba alikiba kushirikiana na msanii simjui jina ila Ina imba hivi
"Niringe nae niacheni nichezenae awe na Mimi, wolowolo shereshere,nacheni naimba nyimbo nzuri utaipenda" jamaa anaitikia "**** kupenda Nisha mpenda sana na mtangojaaaa ooo NAI NAI"
natanguliza shukrani
 
Back
Top Bottom