Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Kuna wimbo nautafuta umeimbwa na msanii anaitwa NTOMBE ulipigwa sana enzi niko mdogo jina la wimbo siujui lakin moja ya mashairi yake unaimbwa hivi [emoji444]mwanangooo mwanangooo lekatula kilindiiii asyere mwanangooo[emoji445][emoji444]
Dah. Sijui unasaidikaje hapa
 
Mwenye nnyimbo za Dolphin posse
1.Huyu manzii
2.Sivyo alivyo
Naziomba wakuu nimezitafuta sana
Huo wimbo wa pili sijaupata, ila nimekuwekea mbili ambazo ndio nyimbo kali za wakati huo za Dolphin Pose. Usisahau kugonga like mzee
 

Attachments

Attachments

Wapendwa na mimi kuna nyimbo naitafuta ya wazungu ya zamani inahusu holiday. Watu wanatupiana makeki, mayai ila nakumbuka tu sehemu wanaimba "laa lalalalalala hey hey hey" X 2 then "I need some holi holi day, you need some holi holi holi day, she needs some holi holi day everybody needs some holi holi day"
Ok, nimekupata. Wimbo umeimbwa na Venga Boys unaitwa Uncle John from Jamaica. Huu hapa. Kama sio useme.
 

Attachments

Salamu nishamuachiaga GENTAMYCINE na ndugu zake wa Butiama akiwemo Cognizant


Ndugu zangu wapenda Burudani ya muziki hasa muziki wa Bongofleva wa miaka ya nyuma (Old skool).

Kuna wimbo unaitwa "NIPE NAFASI" umeimbwa na msanii TID akiwa amemshirikisha Fid Q,huu wimbo nimejaribu kuutafuta kwenye kila Platform ya kuuzia miziki lakini sijafanikiwa kuupata,sijaelewa shida ni nini kiukweli hadi huo wimbo kukosekana kwenye Platform hizo!.


Naomba kama kuna member yeyote ambaye anao huo wimbo au anaweza kuupata popote anisaidie kunitumia hapa maana ninaupenda sana na unanikumbusha mambo mengi sana!.

Nawasilisha!
Twende kazi
 

Attachments

Habari wakuuu kwanza nawapenda Sana
Samahani kuna wimbo nautafuta Sana halafu Sasa nimesahau aliuimba Nani
Ila kuna sehemu wanaimba hv
"I lavyuu Maria debodeboooraa ailavyuu Maria debodeboooraa...Maria debodeboooraa Maria debodeboooraa....
.....
Mwenye anaeufahamu aniambie jamani plz
Huu hapa man. Gonga like nyingi sana
 

Attachments

Back
Top Bottom