Nifahamishe kituo cha watoto yatima chenye uhitaji mkubwa sana

Mjomba hilo lina ukweli kweli au ni uzushi? Anawatesa anawatesaje? Wewe ulishawahi kushuhudia hayo mateso anayowapatia? Tunataka tuzisogeze camera zetu za Siri huko zikamnase emu tupe maelezo yaliyojitosheleza anawafanyaje hao watoto huyo sister wa Mchongo usimuite sister wa kikatoriki maana ma-sister wa kikatoriki wana nyumba zao sio nyumba za watoto yatima
 
Hili tangazo halijanikalia sawa kabisa.

Dkt. Gwajima D
He,tumefika huku ..hii ni Forum ya kijamii amabayo unaweza ukapata taarifa Kwa haraka ndani ya mida mfupi! Uzuri wa JF unapata na taarifa za upande wa pili'!
Njia aliuotumia sio.mbaya..kwani Tapeli hawezi kwenda Ustawi wa Jamii?!
 
🙏
 
He,tumefika huku ..hii ni Forum ya kijamii amabayo unaweza ukapata taarifa Kwa haraka ndani ya mida mfupi! Uzuri wa JF unapata na taarifa za upande wa pili'!
Njia aliuotumia sio.mbaya..kwani Tapeli hawezi kwenda Ustawi wa Jamii?!
Hakuna kitu kama hicho. Aende huko wizara inayohusika rasmi, itakuwa wepesi kum track akihitajika.
 
Mkuu, unamaanisha nini hasa?
Mojawapo y matakwa ya Kisheria ya mtu binafsi kuanzisha Kituo ni kuwa na uwezo wa kijiendesha! Kituo chnyehali mbaya maana yake mmiliki Hana au amekosa uwezo.Kuna watu wanaanzisha Vituo haada ya mwaka.mmoja wanaanza kuomba misaada ..eti hatuna chakula,malazi!? Hapo ujue ..mhusika aliazisha akiwa Hana uhakika wa kukiendesha .Hata hivyo inaweza kuwa na sababu za Msingi za kushindwa kiendesha ,lakini kama kuna integrity wakati wa kuanzisha ,ni nadra sana kutokea! Naongea Kwa uzoefu wa kutosha!
 
Hili tangazo halijanikalia sawa kabisa.

Wanakwenda kulizwa watu. Nahisi huu ni utapeli.

Dkt. Gwajima D
Mkuu, huna haja ya kumsumbua Mh. Waziri kwa jambo dogo kiasi hiki! Usiunderstimate JF!

Au umeisahau nguvu ya JF? Humu utapata taarifa zote: unazozitaka, unazozihitaji, zitakazokufurahisha, zitakazokukera, na hata usizozihitaji.

Kazi yako wewe ni kuchuja ujue uchukue kipi na uache kipi!
 
Any way sio mbaya!
Hayo ni mawazo yangu tena kwa sauti kubwa kabisa.

Mimi siyo muumini wa vituo vya yatima. Jisomee:

 
Huu uzi unawachangiaji wengi wa ile design ya watu wakiona mtu anakunywa bia zake kwa pesa yake mwenyewe ama anatumbua pesa zake kwa namna ajuavyo wanaanza kutoa ushauri wa ohh anatumia pesa vibaya, hizo pesa anazofanyia starehe bora angefanya uwekezaji etc. Unakuta anayekushauri hivyo hanywi bia, hafanyi starehe na hana chochote cha maana. Tuache kuwa washauri uchwara hususani mtu anapoamua kwa akili zake timamu kutumia pesa/mali zake namna aonavyo inamfaa. Mtoa mada usisikilize miluzi mingi fanya namna moyo wako utakuwa na amani.
 
Mkuu, kama kila kituo kingesubiria waanzilishi wake wawe na uwezo kwanza ndipo vianzishwe, kuna VITUO visingeanzishwa kamwe.

Nakifahamu kituo kimoja jijini Mwanza, japo Sasa kina zaidi ya miaka ishirini, lakini kilianza katika mazingira ya hali ya chini sana. Waanzilishi wake ambao walikuwa mume na mke walikianzisha wakiwa hawana karibia kila kitu. Waliianzishia kwenye nyumba waliyopewa kukaa kwa muda. Walikuwa wakikaa na watoto kwenye hiyo hiyo nyumba. Ni yeye na mke wake ndiyo waliokuwa wakifanya kila kitu, mpaka baadaye watu walipoona wanachokifanya wakavutiwa kuanza kuwasaidia.

Kwa sasa ni kituo kikubwa chenye majengo mazuri na wafanyakazi wengi, lakini kilianzia katika hali ya chini sana.
 
Wewe changia mada kwa upeo wako nami nachangia mada kwa upeo wangu.

Waziri tunamwangaisha nini na yumo humu na kajitangaza?

Vipi wewe unampangia mtu maisha yake?
 
Mkuu elewa maana ya neno wapigaji

Watu wengi waliofunguo hivyo vituo wana maslahi binafsi..

Yupo jamaa mmoja naficha code zake kwa maslahi mapana ya utu na ubinadamu.

Ila anamiliki kituo cha kulelea watoto yatima,,lakini anayoyafanya sisi ndy tunaoyajuwa..
-- pesa za misaada anayopata anafanya maendeleo yake binafsi .mfano,

*Kujenga nyumba zake binafsi,,kununuwa Magari ,,mashamba nk huku walengwa(watoto yatima) wakiambulia patupu.

-- anapewa misaada ya madawa ya hospital lakini anaishia kuuza kwenye pharmacy binafsi na pesa kufanya mambo yake.

-- Kuna wafadhili wanasomesha watoto hewa kwa mgongo wa majina ya watoto yatima.
Mfano:
Mfadhili anahitaji majina ya watoto awasomeshe shule za english medium lakini majina yanayokwenda ni ya wajukuu zake na watoto wa ndugu zake, huku mfadhili anadhani anasomesha watoto yatima kumbe anasomesha watoto ambao wazazi wao wapo na sio yatima.

Tajiri analetewa majina ya watoto ambao sio yatima anasomesha bila kujuwa watoto walengwa ambao ni yatima wanasoma KAYUMBA
-- amekuwa akiuza Michele /sukari/nk ambavyo anapewa kama misaada kwa mgongo wa yatima.

Ninaposema wapigaji namaanisha...

Serikali inapaswa iangalie kwa makini eneo hili la watoto yatima.
 
Huo ni ukweli usiopingika kwa wenye kuelewa hivyo vituo, niliwahi kundika hivi:



Tena waziri Dkt. Gwajima D afanye utafiti wa kina hivi vituo, vingine vinauza mpaka watoto kiumalaya.
 
Kabisa mkuu tena mbaya Zaidi Kuna ambao wanatumia vituo vya yatima kwa mgongo wa Dini kujipatia misaada kwa watu kumbe wanafanya kwa maslahi yao..

Hili nina ushahidi nalo [emoji817]..
 
Kabisa mkuu tena mbaya Zaidi Kuna ambao wanatumia vituo vya yatima kwa mgongo wa Dini kujipatia misaada kwa watu kumbe wanafanya kwa maslahi yao..

Hili nina ushahidi nalo [emoji817]..
Taja Jina la kituo na eneo kilipo umesema una ushahidi Sasa unaogopa nini kutaja na kuwataja wahusika?
 
Vyote hivyo vituo havifai kuwepo.


Kuwaweka binadam wenzako unawafuga kama mifugo ili uingize pesa kwa kuwategemea wao ni haramu.

Wala huna haja ya kutafuta kipi, ni vyote.
Vyote vinauza mpaka watoto kiumalaya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…