GE2025 Niffer na wengine 97 wafunguliwa mashtaka, yakiwemo ya UHAINI kufuatia maandamano ya Oktoba 29, 2025

GE2025 Niffer na wengine 97 wafunguliwa mashtaka, yakiwemo ya UHAINI kufuatia maandamano ya Oktoba 29, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Namshauri akichomoka hapa (endapo atachomoka, maana kwa sasa mahakama za bongo haziangalii vifungu vya sheria ila amri kutoka juu) afunge biashara zake Tanzania (Dar na kule Dodoma) kisha apeleke nchi zenye usalama, Kujielewa na rule of law.

Hii Tanzania ya sasa ni nchi ya kususiwa na kutelekezwa na Kila mtu mwenye akili timamu.

Kakikundi ka watu Fulani kamejipa umungu mtu, kanaamua tukiamka tunaishi vile wanataka na ikiwa kinyume wanavyotaka wanatutesa na kutuua.

Shame!
Hii nchi ukiwa na akili timamu na unajitambua unaishi maisha magumu sana.
 
Ujinga umemponza. Aliyoa tangazo Kwenye social media ya kuwa anauza barakoa ambazo ziko.suitable Kwa maandamano, zinaficha uso na zinafanya usipate athari ya mabomu. Na Kwa upofu zaidi alianzisha WhatsApp group kuratibu biashara yake huku hajui ya kuwa miongoni mwan group member ambao aliwa recruit wamo watu wa idara Maalim.
Utoto,ana miaka 26,akitoka ataiheshimu kweli serikali
 
Binti mjinga sana huyu. Alinusurika kesi ya uhujumu uchumi alivyochangisha michango kwenye janga la Kkoo. Nakumbuka hata baada ya speech ya waziri mkuu aliendelea kujigamba kwamba hajakamatwa na ana jeshi imara nyuma yake. Serikali ikatumia busara na kumwachia lakini ikaamua kumpotezea na kutomhusisha kwenye shughuli zake pamoja na za CCM. Ile kupotezewa ingemshtua kuwa serikali haimtaki na asije akajichanganya. Safari hii kajiingiza mwenyewe mtegoni. Tumuombee kabla ya miaka mitano awe ameachiwa.
 
07 November 2025
Mahakama ya Kisutu
Dar es Salaam

VIJANA WENGI WAFIKISHWA LEO MAHAKAMANI, MUWATAZAME MUONEKANO WAO, JE NI WAGENI ? JE NI NDUGU WALIOPOTEA ?


View: https://m.youtube.com/watch?v=p3lr6P8UXdQ

Hawa ndiyo wageni kutoka nje, watazameni vizuri muonekano wao, ni kama walikamatwa kutoka majumbani, walikurupushwa kutoka vijiweni karibu na makaazi yao n.k kutokana na mavazi yao wengine wamevaa bukta n.k

Wengi ni Wasichana kwa wavulana na vijana wafikishwa kwa mabasi ya mapya kabisa mahakama ya hakim mkazi mkuu kisutu jijini Dar es Salaam

Je unaweza kuwatambua, je ni mshikaji wako, mtu wa mtaani kwako, rafiki yako, alitoka kwenda kazini lakini hakurudi n.k

Mbona wote wanashuka kwenye hilo Basi bila kua hata na viatu? Wote wako peku! Au ndio kanuni ya Magereza iko hivyo?
 
Jamhuri yawapiga kesi ya Uhaini watanzania 98 kufuatilia Maandamano ya Oktoba 29, 2025.

Katika Orodha hii, yupo Mfanyabiashara maafuru Jennifer Jovin, Maarufu kama Niffer.

Kesi hizi zimepangwa kusikilizwa kwa hatua za awali kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

====

Kutokana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo, Ijumaa Novemba 07.2025, Mfanyabiahara Jenifer Jovin (Niffer) na wenzake 21 wamesomewa mashtaka matatu (3) ya uhaini

Kosa la kwanza linalowahusu washtakiwa wote 22 ambapo ni kwamba kwa pamoja wamekula njama ya kutenda kosa au kupanga uhalifu ambao ni uhaini

Kosa la pili ambalo ni la uhaini linawahusu washtakiwa 21 isipokuwa mshtakiwa mmoja pekee ambaye ni Niffer, ambapo washtakiwa walianzisha nia ya kuzuia uchaguzi Mkuu 2025, na kutishia mamlaka na wakatekeleza nia hiyo kwa kufanya vurugu zilisababisha uharibifu wa mali za umma,

Na kosa la tatu la uhaini pia linamuhusu mshtakiwa namba moja pekee ambaye ni Niffer, ambapo alihamasisha watu kuvuruga uchaguzi Mkuu 2025 na kuhamasisha umma kununua barakoa za kuzuia mabomu ya machozi kutoka dukani kwake.

View attachment 3498529

View attachment 3498525View attachment 3498526View attachment 3498527

Kuna namna huyo Niffer wenu ameropoka kwa messages na calls, na kaingia kwenye 18, kama kweli alihamasisha watu waandamane na kununua barakoa kwake, atakaa ndani sana!
 
Nimenotice wengi wana majina ya kikristo. Interesting ila labda ni coincidence tu.
 
Ujinga umemponza. Aliyoa tangazo Kwenye social media ya kuwa anauza barakoa ambazo ziko.suitable Kwa maandamano, zinaficha uso na zinafanya usipate athari ya mabomu. Na Kwa upofu zaidi alianzisha WhatsApp group kuratibu biashara yake huku hajui ya kuwa miongoni mwan group member ambao aliwa recruit wamo watu wa idara Maalim.
Kwa mahakama huru Hakuna uhaini hapa. Mshitakiwa hana kesi ya kujibu
 
Back
Top Bottom