GE2025 Niffer na wengine 97 wafunguliwa mashtaka, yakiwemo ya UHAINI kufuatia maandamano ya Oktoba 29, 2025

GE2025 Niffer na wengine 97 wafunguliwa mashtaka, yakiwemo ya UHAINI kufuatia maandamano ya Oktoba 29, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kwahiyo kuhamasisha watu wanunue barakoa ni uhaini? Basi wanaouza vilipuzi, silaha za jadi na bastola ni waahini pia maana wanahamasisha watu kuua
Mkuu Niffer alihamasisha hayo kwenye magroup yao ya whatsapp watu wakaruka na screenshot kwa Mafwele. Ni zaidi ya yale uliyoyaona kwa TV! Namuonea huruma sana huyu msichana pengine kwaajili ya umri ndo maana!!!!
 
Triump katoa saa 72 la sivyo atatupa makombora dhid ya jwccm
 
Dogo alijisahau sana,au ndo pesa zinalevya
Mpumbavu na mshenzi huyo mtoto!! Alitafuta sifa kwa nguvu sana na umaarufu bila kujua wanaomtumia watakua wamwisho kuumia!! Nililiona anguko la Niffer kitambo sana maana hakua na utulivu wa akili wala nafsi! Inawezekana pia ana ukichaa!!
 
Nimeona stakabadhi za mahakama Niffer na wengine 97 washtakiwa kwa kosa la kula njama (conspiracy to commit offence) pamoja na kosa la UHAINI.

=========
Kutokana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo, Ijumaa Novemba 07.2025, Mfanyabiahara Jenifer Jovin (Niffer) na wenzake 97 wamesomewa mashtaka matatu (3) ya uhaini

Kosa la kwanza linalowahusu washtakiwa wote 22 ambapo ni kwamba kwa pamoja wamekula njama ya kutenda kosa au kupanga uhalifu ambao ni uhaini

Kosa la pili ambalo ni la uhaini linawahusu washtakiwa 97 isipokuwa mshtakiwa mmoja pekee ambaye ni Niffer, ambapo washtakiwa walianzisha nia ya kuzuia uchaguzi Mkuu 2025, na kutishia mamlaka na wakatekeleza nia hiyo kwa kufanya vurugu zilisababisha uharibifu wa mali za umma,

Na kosa la tatu la uhaini pia linamuhusu mshtakiwa namba moja pekee ambaye ni Niffer, ambapo alihamasisha watu kuvuruga uchaguzi Mkuu 2025 na kuhamasisha umma kununua barakoa za kuzuia mabomu ya machozi kutoka dukani kwake.

View attachment 3498536

Orodha nyingine:
View attachment 3498542
View attachment 3498540
View attachment 3498537

Mashtaka yameambatanishwa chini:
Wasijali maana 9.12.2025 yaani Tisa December tutawatoa. Yaani tutaingia mpaka ikuli siku hiyo. Kazikazi, lazima tupate uhuru wa kweli
 
Mpumbavu na mshenzi huyo mtoto!! Alitafuta sifa kwa nguvu sana na umaarufu bila kujua wanaomtumia watakua wamwisho kuumia!! Nililiona anguko la Niffer kitambo sana maana hakua na utulivu wa akili wala nafsi! Inawezekana pia ana ukichaa!!
Uwe na akiba ya maneno pamoja hisia zako. Kila neno unalomsemea mwenzako jiweke nafsi yako kwanza. Kukaa kimnya nako ni busara. Ni hayo tu
 
"Walisema msimamo huu unaashiria uasi....., ni kweli, kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi.... hiyo ndiyo namna ya kupata mabadiliko, kwa hiyo tunaenda kukinukisha, sanasana huu uchaguzi tunaenda kuuvuruga kwelikweli, tunaenda kukinukisha vibaya"
Wavurugwe wao
 
Ujinga umemponza. Aliyoa tangazo Kwenye social media ya kuwa anauza barakoa ambazo ziko.suitable Kwa maandamano, zinaficha uso na zinafanya usipate athari ya mabomu. Na Kwa upofu zaidi alianzisha WhatsApp group kuratibu biashara yake huku hajui ya kuwa miongoni mwan group member ambao aliwa recruit wamo watu wa idara Maalim.
Sahivi awape na mbinu za kukaa jela
 
Sio rahisi hivyo ukiangalia wateja wake wengi wako Tanzania

Na unajua atachukua mda gani kukaa mahabusu anaweza akaa mahabusu mpaka kutoka biashara zake zimefilisika zote na itambidi aanze upya
Mkuu lini utakuja kuwa rais ukomeshe huu upuzi? Yani kila kukicha unazidi tu na huoneshi dailies ya kupungua.

Mwafrika is very primitive.
 
Kweni tafsiri ya UHAINI kwa mujibu wa KATIBA inasemaje kwa maana sasa watu wanagaiwa UHAINI kama karanga?.

Kuiba kura nako ni kosa gani kwa mujibu wa KATIBA.
 
Mimi nazidi kuwaasa vijana!
Msichokoze serikali,
Serikali ina mkono mrefu sanaa,
Hao huko Mtandaoni wanawashawishi mfanye vurugu ila hawapo wapo uko kwa mabwana zao,sasa nyie mtapoteza familia zenu zibaki zinawalilia!
Vijana jengeni nchi yenu acheni vurugu!
Mwenye masikio na asikie.!!
waijenge nchi kwanafasi gani wanazopewa?
 
Kwamba Niffer Kucheza kale Ka Clip ndo uhani? Aisee Hii nchi kuna shida kubwa sana

Hii mbinu ya kutisha watu kwa kuwapa mateso ili wanyamaze imeshashindwa, watafute mbinu mpya
 
Jeshi la polisi lime mbambikizia kesi ya uongo Niffer na heche sikuhizi unakamatwa tu bila maelezo kosa utalikuta polisi hii ni kinyume cha sheria

Heche wala niffer hawakukamatwa kwa makosa ya uhaini hii ni ubambikiaji wa kesi za uongo wazi wazi, aidha kuzuia uchaguzi au kuhamasisha mabadiliko kwa maandamano sio uhaini.
 
Ujinga umemponza. Aliyoa tangazo Kwenye social media ya kuwa anauza barakoa ambazo ziko.suitable Kwa maandamano, zinaficha uso na zinafanya usipate athari ya mabomu. Na Kwa upofu zaidi alianzisha WhatsApp group kuratibu biashara yake huku hajui ya kuwa miongoni mwan group member ambao aliwa recruit wamo watu wa idara Maalim.
Shida nayoiona, kuhamasisha maandano kitu kimoja ila kwa kilichotokea kwenye maandamano yaani uharibifu na mauaji, they could indeed fall into that convinction.

Chanzo na mchawi anatafutwa, hawa wapo katika nafasi ngumu kuliko Tundu Lissu.
 
Back
Top Bottom