GE2025 Niffer na wengine 97 wafunguliwa mashtaka, yakiwemo ya UHAINI kufuatia maandamano ya Oktoba 29, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hivi emmanuel mwita yupo humo??
 
Hii nchi ukiwa na akili timamu na unajitambua unaishi maisha magumu sana.
 
Utoto,ana miaka 26,akitoka ataiheshimu kweli serikali
 
Nilidhani ni kesi ya wizi na uharibifu wa mali.
 
Binti mjinga sana huyu. Alinusurika kesi ya uhujumu uchumi alivyochangisha michango kwenye janga la Kkoo. Nakumbuka hata baada ya speech ya waziri mkuu aliendelea kujigamba kwamba hajakamatwa na ana jeshi imara nyuma yake. Serikali ikatumia busara na kumwachia lakini ikaamua kumpotezea na kutomhusisha kwenye shughuli zake pamoja na za CCM. Ile kupotezewa ingemshtua kuwa serikali haimtaki na asije akajichanganya. Safari hii kajiingiza mwenyewe mtegoni. Tumuombee kabla ya miaka mitano awe ameachiwa.
 
Mbona wote wanashuka kwenye hilo Basi bila kua hata na viatu? Wote wako peku! Au ndio kanuni ya Magereza iko hivyo?
 

Kuna namna huyo Niffer wenu ameropoka kwa messages na calls, na kaingia kwenye 18, kama kweli alihamasisha watu waandamane na kununua barakoa kwake, atakaa ndani sana!
 
Nimenotice wengi wana majina ya kikristo. Interesting ila labda ni coincidence tu.
 
Kwa mahakama huru Hakuna uhaini hapa. Mshitakiwa hana kesi ya kujibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…