Nilichojifunza Uchaguzi wa Kenya: Tuwape nafasi Matajiri na Watafutaji

Nilichojifunza Uchaguzi wa Kenya: Tuwape nafasi Matajiri na Watafutaji

Inasikitisha sana mkuu eti nayo sehemu ya sifa ya kuwa kiongozi ni kuwa MASKINI haya ni maajabu kama ty mtu (mskini) ameshindwa kujisamamia mwenyewe kupata maendeleo yake binafsi ni Maendeleo ya Nchi ataweza kusimamia?
Maskini hawezi mletea maendeleo mtu kama hata yeye tu ameshindwa jiletea maendeleo
 
Kuna mawaziri vijana kwa sasa wanasaini mikataba ya akina mangungo na wanachofanya kupitia ofisi zao haina mguso kwenye jamii, wakipewa pesa na genge ya wahuni huko nje, kuna namna watatuongoza kutufikisha nchi ya ahadi au watalipa kwanza pesa za watu?

Fuatilia mtu anaitwa Lee Kuan Yew, mfuatilie David Bengurion, mfuatilie, Luiz Lula da Silva; wote hawa hawakutokea familia tajiri ila wamefanya mapinduzi makubwa sana kiuchumi na kijamii nchi mwao.

Uhuru Mwigai anatokea familia tajiri, yet kapiga deal nyingi Kenya ikiwamo SGR ya diezel na wachina yenye gharama kubwa kuliko sGR ya umeme wanayojenga Waturuki hapa nyumbani.

Kuna kiongozi mmoja mwaka 1995 alikuwa na ukwasi wa kutisha, Nyerere alihoji, huyo kijana anaweza ku-account huo utajiri kapataje wakati inafahamika ni public servant; Akahoji, je, analipa kodi, ikaonekana hata kodi za serikali halipi!
Mtu kama huyo akishika urais unategemea nini?

Anyway, kupanga ni kuchagua, kama tutataka matajiri kweli, basi tukawashawishi akina Elon Musk waje, ila kama ni matajiri kama yule wa timu ya mpira wa miguu ambae mpaka leo 20bn haijaweka kwenye acc, mkipa nchi mtu kama huyu mtalia sana.
Hata mimi napenda matajiri waongoze, ila ni matajiri kweli wenye uwazi kama akina mzee John Rupia au matajiri ambao baadhi yao wanafungamanishwa na wauza nganda?
Kikubwa matajiri ndo tuwape uongozi! Hawa makapuku hawana lolote ndo wanaturudisha nyuma huku wao wakijineemesha
 
Naona umetoa sababu nyepesi sana kwenye uzi wako.

Simply put, mfumo wa capitalism kule Kenya ndio umewafanya wakenya wakawa na mindset uliyotaja kuhusu matajiri.

Wakati sisi, mfumo wa ujamaa ndio umetufanya kuwa na mindset hii tuliyonayo, kuwaona matajiri ni kama maadui.

Japo naona with time tunaanza kubadilika, hao vigogo au watoto wao waliojipatia utajiri kwa kutumia uwepo wa wazazi wao muda mrefu kwenye siasa, ndio wanaanza kushika hatamu kwenye siasa zetu.

Hii ni kama ilivyokuwa kwa kina Uhuru na Odinga ambao wote wamerithi utajiri toka kwa wazazi wao waliokuwa wanasiasa kule Kenya.
Mfumo wa ujamaa kwa sasa Tanzania upo vitabuni tu tena kwenye vitabu vya zamani! Hakuna anaye practise ujamaa saivi
 
Kikubwa matajiri ndo tuwape uongozi! Hawa makapuku hawana lolote ndo wanaturudisha nyuma huku wao wakijineemesha
Kama wako tayari kwa public scrutiny ya chanzo cha utajiri wao na wanalipaje kodi, we may gamble to to try.
Ila kama ni aina ya matajiri kama yule wa club moja ya mpira ambae anasema club ina thamani ya 40bn na akaulizwa, amejuaje club ina value ya 40bn; hakutoa jibu.

Hakuna la maana alilofanya jimboni kwake.
Kuna bilionea mwingine aliachana na siasa uchwara, ukikagua toka kawa mbunge 1994 mpaka anatoka, ni aibu.

Kupanga ni kuchagua!
Tuna nafasi ya kupanga na kuchagua hatma ya nchi yetu ila sio ya expense ya matajiri 'wajanja-wajanja'
 
Mfumo wa ujamaa kwa sasa Tanzania upo vitabuni tu tena kwenye vitabu vya zamani! Hakuna anaye practise ujamaa saivi
Kama ungekuwepo vitabuni kama unavyoamini basi tusingehangaika kusema mimi sio fisadi kwenye kampeni kama ulivyoandika kule juu.
 
Siasa za Kenya sizitofautishi sana na siasa za Marekani! Wao wanaamini sana katika kumpa nafasi mtu anayeonesha ana uwezo wa kutafuta pesa na kupambana kupata pesa! Ndo mana inawezekana hata kiuchumi wako vizuri kuzidi sisi ingawa na sie tunajikongoja kuwafikia

Wakenya sio waumini sana wa ngonjera za sijui nichagueni mimi sio mwizi, mimi sio fisadi kwa sababu wanajua watu wanaopenda kujivika hizo sifa sio watu wenye akili za kimaendeleo na hawawezi kuhimiza vizuri maendeleo yao!

Kutoka kwa Jomo Kenyata mpaka kwa Daniel Arap Moi, kuja kwa Kibaki mpaka kwa Uhuru Kenyata na sasa naona Hustler William Ruto anaenda kubeba ndoo.

Wote ni watu wenye ukwasi ambao wako proud na ukwasi wao na wanatumia ukwasi wao kama njia ya ku motivate watu wengine kuwa na ukwasi.

Tanzania tujifunze hili kutoka Kenya mambo ya mtu kujisifia umaskini na kujiona ndo ticket k ya kuwa kiongozi tuachane nayo.

Kuanzia saivi tuanze kuangalia maisha ya mtu kama anajiweza kiuchumi vizuri, ana mali anazoziendesha vizuri, ana nyumba nzuri na ya kisasa na ana biashara nzuri ambayo ana imanage vizuri kama kigezo cha kumpa mtu uongozi.

Suala la kuteua sijui mtu hohehae asiye na mbele wala nyuma huku tukitegemea apandishe uchumi wetu liwe mwisho kuanzia leo.
Kuwa TAJIRI au MASKINI haipasi kuwa Qualification ya mtu kuchaguliwa kuwa Kiongozi.

Kiongozi wa watu ni zaidi ya hapo, maana TAJIRI hatakiwi kutumia pesa zake kuongoza, atazirudishaje?

By the way jajiri aache biashara zake akawe Rais Kwa mfano anataka nn?

Ikulu Pana biashara Gani Hadi matajiri wapakimbilie?
 
Akili zako sio tu za kimaskini ila ni za kijinga sana! Waislam na Wakristo tunasoma kuhusu habari ya male suleiman Mungu alimpa hekima na utajiri? Unajua kwa nini Mungu alimuongezea utajiri

Wewe na umaskini wako huwezi kuwaza sawa kama tajiri katika kuwaletea maendeleo wako! Tajiri from experience yake anaweza just afanye nini ili watu wake watajirike na wawe na maisha mazuri kiuchumi wewe na umaskini with no experience kwenye kutafuta pesa kwa mafanikio utawezea wapi?
 
Kama ungekuwepo vitabuni kama unavyoamini basi tusingehangaika kusema mimi sio fisadi kwenye kampeni kama ulivyoandika kule juu.
Kuongea kwenye kampeni hayo ni ujinga tu
 
Kama wako tayari kwa public scrutiny ya chanzo cha utajiri wao na wanalipaje kodi, we may gamble to to try.
Ila kama ni aina ya matajiri kama yule wa club moja ya mpira ambae anasema club ina thamani ya 40bn na akaulizwa, amejuaje club ina value ya 40bn; hakutoa jibu.

Hakuna la maana alilofanya jimboni kwake.
Kuna bilionea mwingine aliachana na siasa uchwara, ukikagua toka kawa mbunge 1994 mpaka anatoka, ni aibu.

Kupanga ni kuchagua!
Tuna nafasi ya kupanga na kuchagua hatma ya nchi yetu ila sio ya expense ya matajiri 'wajanja-wajanja'
Huyo bilionea uchwara aliyeachana na siasa uchwara kama hujui ndo muanzilishi wa mfumo wa bima ya afya ambapo serikali ya mkapa walicopy kutoka kwake na hadi leo watumishi wa umma wanautumia na kufaidika nao. Alianzisha mfumo huu jimboni kwake igunga mwaka 1995

Pia ndo amejenga kituo cha polisi kizuri zaidi Tanzania cha Oysterbay ambacho wanigeria wanakijadili uzuri wake kulinganisha na vituo vyao vya polisi
 
Kituo Cha oysterbay hakijajengwa na tajiri yoyote, kimejengwa Kama hospital,madarasa na Majengo mengineya serikali yanavyojengwa.

Wewe ni zaidi ya mpumbavu
 
Napendekeza waziri wa sekta fulani angalau awe na degree au masters inayohusiana na sekta anayoisimamia!
Waziri hatakiwi kuwa Mbunge, anatakiwa ateuliwe kutoka sekta inayohusika na Wizara husika
 
Kuna tofauti kati ya kupambana ku-build wealth na kuiba, Matajiri wa Tanzania ni wezi, tajiri aliyepambana alikuwa Mengi tu, wengine wote wezi!
Una akili za kimasikini sana
 
Waziri hatakiwi kuwa Mbunge, anatakiwa ateuliwe kutoka sekta inayohusika na Wizara husika
Haya mapendekezo nayakubali sana! Nakumbuka kwenye rasimu ya mzee warioba nililionaga hili
 
Kituo Cha oysterbay hakijajengwa na tajiri yoyote, kimejengwa Kama hospital,madarasa na Majengo mengineya serikali yanavyojengwa.

Wewe ni zaidi ya mpumbavu
Hujui Caspian ndo wamejenga kile kituo pamoja na nyumba za Polisi za Mikocheni Tanesco na Kunduchi? Unajua Caspian ni kampuni ya nani?

Basi nikusaidie maana inaonekana unapenda kupayuka tu bila kujua vitu! Caspian ni kampuni ya Rostam Aziz

Embu punguza kujianika uzumbukuku wako hapa
 
Kwa kenya wote aliowataja utajiri wao wameupata kwenye uongozi serikalini!!
Wameiibia Nchi !! Hata mkuu wao anamtuhumu mgombea mmoja kwamba ni fisadi mkubwa !! Kwahiyo kwa mawazo ya mtoa mada Viongozi wenye kujua kutafuta pesa kwa njia yeyote hata ya ufisadi ndio watakaotuletea maendeleo ya haraka hapa Tz !! Kweli ukistaajabu ya musa utayaona ya Jf !!
 
Wameiibiaje nchi?
 
Kuwa TAJIRI au MASKINI haipasi kuwa Qualification ya mtu kuchaguliwa kuwa Kiongozi.

Kiongozi wa watu ni zaidi ya hapo, maana TAJIRI hatakiwi kutumia pesa zake kuongoza, atazirudishaje?

By the way jajiri aache biashara zake akawe Rais Kwa mfano anataka nn?

Ikulu Pana biashara Gani Hadi matajiri wapakimbilie?
Suleiman mfalme hakuwa TAJIRI aliingia kuwa mfalme akiwa kijana mdogo tena mtoto wa Suria au nyumba ndogo. Hakuna aliye mjua.

Utajiri wake ulikuja baada kuomba HEKIMA na maarifa Kutoka Kwa Mungu. AKAPEWA ndo Dunia nzima AKAITAWALA.

Daudi babaye Suleiman alikuwa MCHUNGAKONDOO, alipakwa mafuta alitokea mbugani akaacha mifugo, alitokea familia ya Yese maskini kabisa.

We usitetee wezi, wauza dawa za kulevya wanayotaka kutakatisha fedha kuukwaa urais watuuze.

Nasisitiza TAJIRI au MASKINI haitoshi kuwa Qualification kuwa KIONGOZI.

Ni zaidi ya hapo.

Ameeeen.
 
Umesema suleiman hakuwa Tajiri alafu unasema alikuwa mtoto wa Mfalme Daudi!

Kuna mfalme mwenye mtoto maskini?

Alafu kwa nini Mungu alipompa ufalme alimuongezea na utajiri? Hujifunzi kitu hapo kuwa huwezi kuwa kiongozi mzuri kama sio tajiri?
 
Back
Top Bottom