Kuna mawaziri vijana kwa sasa wanasaini mikataba ya akina mangungo na wanachofanya kupitia ofisi zao haina mguso kwenye jamii, wakipewa pesa na genge ya wahuni huko nje, kuna namna watatuongoza kutufikisha nchi ya ahadi au watalipa kwanza pesa za watu?
Fuatilia mtu anaitwa Lee Kuan Yew, mfuatilie David Bengurion, mfuatilie, Luiz Lula da Silva; wote hawa hawakutokea familia tajiri ila wamefanya mapinduzi makubwa sana kiuchumi na kijamii nchi mwao.
Uhuru Mwigai anatokea familia tajiri, yet kapiga deal nyingi Kenya ikiwamo SGR ya diezel na wachina yenye gharama kubwa kuliko sGR ya umeme wanayojenga Waturuki hapa nyumbani.
Kuna kiongozi mmoja mwaka 1995 alikuwa na ukwasi wa kutisha, Nyerere alihoji, huyo kijana anaweza ku-account huo utajiri kapataje wakati inafahamika ni public servant; Akahoji, je, analipa kodi, ikaonekana hata kodi za serikali halipi!
Mtu kama huyo akishika urais unategemea nini?
Anyway, kupanga ni kuchagua, kama tutataka matajiri kweli, basi tukawashawishi akina Elon Musk waje, ila kama ni matajiri kama yule wa timu ya mpira wa miguu ambae mpaka leo 20bn haijaweka kwenye acc, mkipa nchi mtu kama huyu mtalia sana.
Hata mimi napenda matajiri waongoze, ila ni matajiri kweli wenye uwazi kama akina mzee John Rupia au matajiri ambao baadhi yao wanafungamanishwa na wauza nganda?