Nilipata fursa ya kutembelea Australia na New Zealand nilichojifunza ni hiki

Nilipata fursa ya kutembelea Australia na New Zealand nilichojifunza ni hiki

Watu weupe walishajijengea Misingi na Mitizamo mizuri tokea zamani. Sababu walishajua maendeleo kwa sekta yeyote msingi mkuu ni Mtoto, Inatakiwa akazaniwe tokea udogoni, afundishwe kua Disciplined.

Mtoto anayezaliwa Australia hata kama ni Poor family utakuta anafundishwa kustaarabika toka akiwa mdogo hivyo anakua Mentallity perfect, Ijapo sio wote ila walau 7 ya 10.

Mentallity ya kijana wa miaka 25 Australia huwezi ukaifananisha na ya mzabzab zee la papuchi au Poor Brain mzee wa Action first maneno baadaye.

😂!
 
Wakuu, mnamo mwezi wa 7 mwaka 2023 nilipata fursa ya kutembelea Australia na baadaye New Zealand, kwakifupi NILIKATA TAMAA.

1. Hakuna namna Tanzania tunaweza kuwafikia hata wakiamua kutusubiri kwa miaka 100.

2. Niliona kabisa kuwa Waafrika wengi ni kama hatuna akili hasa tunapokuwa katika ardhi yetu.

3. Upende usipende, Wazungu wametuzidi akili na maarifa ukitaka kujua hilo, tembelea mgodi wa GGM tu uone trailer, sasa Australia kuna migodi niliingia nikaishia kusema tu aaaah kmmk walai.

4. Mwisho kabisa naamini haikuwa sahihi kwa mwajiri kutupeleka Australia kujifunza, pale alipoteza gharama zake bure, sisi hatujafikia wala sioni tukifikia huko ila asanteni kwa exposure.

5. Operators wa mitambo ya migodini tembeleeni seek.com.au tafuteni deals japo si rahisi ila ukipata unaenda kuishi dunia nyingine kabisa kmmk.

6. NYERERE ASINGEWAFUKUZA WAZUNGU TUNGEKUWA MBALI SANA, KISWAHILI KIKATUZIKA KABISA.
NI NCHI IPI AMBAYO WAZUNGU WAMEISHI KAMA WAKOLONI ILIENDELEA? HIZO ZILIZOKALIWA MOJA KWA MOJA NAO NDIO WAMEZIENDELEZA VINGINEVYO NI KUVUNA NA KUPELEKA KINGI KWAO NA KUBAKIZA KIDOGO KUENDELEZA NCHI.
 
Ukweli mchungu,ingawa Nyerere kuwaondoa wazungu bado alikuwa sahihi,shida ni ulafi wa viongozi wetu,wanataka kuwa viongozi ili washibishe matumbo yao na sio kuendeleza nchi....
"The concept of primitive accumulation of wealth refers to the historical process by which wealth and capital were initially concentrated in the hands of a few"

Kwa wenzetu hiyo akili ya kujilimbikizia mali walikua nayo kuanzia karne ya 5 kabla ya Kristo mpaka kwenye karne ya 9 hivi baada ya Kristo. Sisi ndio saa izi akili zetu zipo huko.
 
Wakuu, mnamo mwezi wa 7 mwaka 2023 nilipata fursa ya kutembelea Australia na baadaye New Zealand, kwakifupi NILIKATA TAMAA.

1. Hakuna namna Tanzania tunaweza kuwafikia hata wakiamua kutusubiri kwa miaka 100.

2. Niliona kabisa kuwa Waafrika wengi ni kama hatuna akili hasa tunapokuwa katika ardhi yetu.

3. Upende usipende, Wazungu wametuzidi akili na maarifa ukitaka kujua hilo, tembelea mgodi wa GGM tu uone trailer, sasa Australia kuna migodi niliingia nikaishia kusema tu aaaah kmmk walai.

4. Mwisho kabisa naamini haikuwa sahihi kwa mwajiri kutupeleka Australia kujifunza, pale alipoteza gharama zake bure, sisi hatujafikia wala sioni tukifikia huko ila asanteni kwa exposure.

5. Operators wa mitambo ya migodini tembeleeni seek.com.au tafuteni deals japo si rahisi ila ukipata unaenda kuishi dunia nyingine kabisa kmmk.

6. NYERERE ASINGEWAFUKUZA WAZUNGU TUNGEKUWA MBALI SANA, KISWAHILI KIKATUZIKA KABISA.
Ebu tupia tupicha hapa
 
Ukifika nchi kama Kanada utasema nini mwanangu? Huna haja ya kutudhalilisha kwa ushamba wako. Waafrika tuna akili ila ukoloni ulituchelewesha. Kuna siku tutawafikia tutakapopata viongozi na si chawa na wafuga chawa. Ulishafika Dubai au Sharjah, Manama na kwingineko au China? Hawa nao ni wazungu au ujinga na kutokujiamini kwako? Kifupi, tutakapoacha kushobokea ujinga kama dini na mila za kigeni, tutawakamata haraka tu.
Mkuu na wewe naona umejibu kwa jazba tuu,sasa hapo dini imeingiaje?
Hao china ,japan wana dini zao ila wameendelea,je dini zimewakwamisha?
Canada,USA, UK wana dini na wengi ni wakristo wanamaendeleo hapo sijazitaja sweden,Norway n.k.
Nimeona umegusia point moja ambayo ni ya msingi,kukosa viongozi wenye moyo wa kujenga nchi/Afrika
na sisi tumeishia kumsifia anayekuibia kisha akakupa pombe na biscuit. Tukivuka hatua hii tutashinda pakubwa.
 
Nakazia hapo kwa nyerere, aliwakosea mno watanganyika kuwafukuza wakoloni kwa haraka na kutuunganisha na wanyonyanyi wakizenji. Ilipaswa tukae na wakoloni hadi miaka ya themanini mwishoni. Nchi ingefunguka kama kwa madiba.
 
Mkuu na wewe naona umejibu kwa jazba tuu,sasa hapo dini imeingiaje?
Hao china ,japan wana dini zao ila wameendelea,je dini zimewakwamisha?
Canada,USA, UK wana dini na wengi ni wakristo wanamaendeleo hapo sijazitaja sweden,Norway n.k.
Nimeona umegusia point moja ambayo ni ya msingi,kukosa viongozi wenye moyo wa kujenga nchi/Afrika
na sisi tumeishia kumsifia anayekuibia kisha akakupa pombe na biscuit. Tukivuka hatua hii tutashinda pakubwa.
Ukifikiri vizuri unakuja kugundua kua hiyo sababu ya dini ni ya uongo, dini tunaisingizia tu.

Kila nchi raia wake wana dini, nchi nyingine ndo zinaendeshwa kwa misingi ya dini 99%, nchi nyingine dini dominant ndo inaamua hata baadhi ya mambo ya kiserikali.

Ni akili zetu tu kutaka kujilimbikizia mali(ubinafsi uliokubuhu).
 
Lugha hua mnaisema bure na kuisema lugha kuwa ni chanza cha wewe kuwa nyuma huo ni uzwazwa!, nchi ngapi zinazungumza lugha zao na kiuchumi zipo juu..?
hivi unafahamu hata hawa jirani zetu kenya wanatamani Kiswahili kingekuwa chakwao..?
unajua ni faida kiasi gani wanaipata kwa kitumia Kiswahili..?
sema wabongo tumelala usingizi wa pono si kuisema lugha!.

kuna mataifa kibao English hawajui na raia wake hata hawajivunii kutokujua English lkn bado wapo vizuri kiuchumi na nyanja nyengine!.. hatujaamua tu kuwa serious ila Kiswahili sio sababu ya kurudi nyuma!.
 
Ana haki ya kushangaa ila amekosea kututukana wafrika. Kikweli wenzetu wanaenda mbele ss tunarudi nyuma halafu visingizio kibao afrika watu wenye akili wameandamwa sana afrika hawatakiwi sasa tunategemea nn Angekuwa Elon Musk yupo afrika ungekuta either marehem au maskini watawala wetu hawapendi wt wenye akili hata kidogo
 
Afrika matumizi ya akili ni madogo mno. vitu vidogo vinatushinda. mtaani hakuna maji lakini ajabu DAWASA wamejenga jengo la mabilioni ya fedha badala ya kuwekeza kwenye uzalishaji na usambazaji wa maji
 
Miaka 400 juzi tu? Sisi tuko nyuma miaka 1500+ sema kinachotusaidia ni huu muingiliano na wazungu kutuletea teknolojia na miundombinu. Kiakili bado tuko zama za mawe za kale..!
Nilikua naongea na Mzungu mmoja alisema ninyi mna bandari harafu Nchi zote zinazowazungukq zinategemea bandari yenu ila Trucks kuingia Tanzania ni kama nayo ni bidhaa hiyo kodi yake pamoja na bara bara ndogo na mbovu kutoka Daslm mpaka Tunduma akili yenu imedumaa sana...yaani vile vitu vinavyotakiwa kuwasaidia Nchi ipate pesa ninyi ndio mnavipa kodi ya hatari wakati hivyo vitu vikiwepo mapato yatapatikana kwa kutoa mizigo mingi huko Bandarini na kwa wakati nikabaki kusema sawa tu..
 
Ukifika nchi kama Kanada utasema nini mwanangu? Huna haja ya kutudhalilisha kwa ushamba wako. Waafrika tuna akili ila ukoloni ulituchelewesha. Kuna siku tutawafikia tutakapopata viongozi na si chawa na wafuga chawa. Ulishafika Dubai au Sharjah, Manama na kwingineko au China? Hawa nao ni wazungu au ujinga na kutokujiamini kwako? Kifupi, tutakapoacha kushobokea ujinga kama dini na mila za kigeni, tutawakamata haraka tu.
Kwa akili zipi tulizonazo mkuu? Tuache kutafuta kichaka cha kujificha, hatuna uwezo wala akili za kuwafikia, hatuna innovation yoyote ya kutufanya tuwafikie na hata tuachwe tujitafute for 100yrs hatuna huo uwezo. Labda tuwe land-locked, kissingie chochote kwa namna yoyote, huenda ndio tutaamka usingizi wa pono.
 
Umeandika ulichojifunza Ila sijaiona Kama umejifunza chochote zaidi ya kulalamika.
Ziara Kama hizo zinawafaa wenye akili na sio kilaza Kama wewe, wenye akili wakitoka huko wanakaa chini na kujiuliza sisi tumekwama wapi na tufanyeje ili tujikwamue SEMA wewe ulienda kushangaa.
 
Swala ni kuwajibika kikamilifu katika nafasi yako uliyonayo.
Jitahidi sana kuwa na bidii sana katika kile unachokifanya
Ondoa mawazo ya HAIWEZEKANI kabisa kwenye akili yako.
Ishi na wapumbavu kama vile hawapo,waelimishe na kuwasaidia wajinga wenye kiu ya maarifa.
Ondoa kabisa ubinafsi nafsini mwako.
Jenge tabia ya kujitolea pale unapoweza kufanya unachokiweza kwa kuwa kinakuhusu wewe.(Chanzo cha uchawi ni kuchungulia sahani ya mwenzako)
Mafanikio ni maisha ya uwajibikaji katika utendaji zaidi ya propaganda ambazo ndio zimejaa kwenye vichwa vya wengi.
 
Back
Top Bottom