Niliwahi kumwambia Hayati Magufuli, leo narudia kwa Rais Samia ili asipoteze muda wake

Mkuu k
Huko Marekani sera za Bush Jr. na Obama zilikuwa zinafanana?
Kuna kitu ambacho hukijui kuhusu Marekani. Chochote kinachofanywa na Marekani au Rais wa Marekani ni kwa maslahi ya kiulinzi na kiuchumi kwa ajili ya Marekani.Hakuna Rais wa marekani anafanya jambo kwa ajili ya legacy yake km kiongozi bali ni maslahi ya marekani na Taifa linataka Nini.

Marekani akipigana Vita leo siyo mpango wa mwaka mmoja au mawazo ya kimaamuzi ya Rais yeye km yeye Bali Ni mpango wa muda mrefu wa vyombo vya kiintelijensia kukusanya taarifa.

Marekani kila kitu kipo ktk misingi ya kikatiba.Hebu angalia tarehe yao ya KUPIGA KURA ktk uchaguzi mkuu ipo ktk katiba.

Marekani Rais hawezi kuibuka leo anapeleka miswada bungeni kipuuzi puuzi tu kwa maslahi yake .

Mfano Rais yyte wa marekani anayeingia madarakani kwa Sasa anaikuta mezani Kwamba threat ya kiuchumi kwa marekani kwa Sasa ni nchi ya China.Na inaenda hivyo.

Hawabahatishi, consistency yao ni Kwamba Hakuna mtu anaweza kugusa misingi ya taifa sembuse katiba yenyewe.Sera yao ya kiuchumi,kijeshi nk Ni ya kitaifa siyo utashi wa Rais.Wanatembea kwenye mstari japo pengine wew unaweza usione.
 
Sawa mkuu JF kuna ndugu zetu wa kila namna. Ngoja twende nao hivyo hivyo tu.
 
Alikuwa mgonjwa sana watu walikuwa hawajui tu!! Ndio maana alikuwa anazungumzia kifo sana.
Tofauti na kuropoka. Lakini ni raisi alieleta impact kubwa sana in a long run. Spirit na discipline mindset alio iacha kwa watanzania na waafrika ni kubwa mno. Watanzania ni warahisi sana kuyumbishwa. Mtu akijua tu kupangilia maneno mnamuamini.
 
Naam mkuu
 
Uchambuzi mzuri sio haba
You are mis guided brother. True liberation haiitaji kubembelezana. Angalia true liberators wote kina gadafi, lumumba, kwame. Ni watu agressive lakini at the same time
Walikua na akili. Huyu jamaa inaonekana ana standard yake mwenyewe ya kupima intelligence ya mtu. Intelligence ya mtu haipimwi hivo. Inapimwa kwa output impact. Jpm amesababisha impact kubaa sana ndani na nje ya africa. Lakini jamaa anataka ku ignore kila alichokiwekea effort jpm.
 
Tanzania tuna kasumba ya kusapoti viongozi kuwa ndo uzalendo na kupinga sio uzalendo ,viongozi wa nchii hii mpaka wananchi hawajui wanataka nini kutwa nzima kulalamika tu
 
Mbona kuna baadhi ya vitu ametoa pongezi mkuu
 
Jiwe angejua nchi inahitaji zaidi Helicopter za ambulance kuliko uwanja wa chato na mabombadia yake huenda ndugu yako bado angekuwa na mtoto wake mpaka leo.
Kuna ndugu yangu aliwahi kupoteza mtoto katika foleni ya ubungo wakati akiwa anampeleka hospitali. Jamaa ana pesa nzuri tu (maendeleo ya watu) lakini miundombinu mibovu (maendeleo ya vitu) ilifanya apoteze mtoto.
 
Na mabalozi wake wangetumuliwa pia, lakini hata kwa Kiduku Kim Jong wa Korea bado kuna mabalozi wa nchi nyingi tu za Ulaya.
Angekuwa hawapendi wazungu, angewafukuza mabalozi basi mkuu. JPM alikuwa anataka fair play kati ya Tanzania na nchi zingine.
 
Gaddafi na Kwame Nkurumah walikuwa madikteta na wote waliondolewa kwa aibu katika nchi zao.
 
JPM hakuwa malaika yule. Yeye pia ni mwanadamu na ana mapungufu yake mengi tu.

Ww ndio unasema, dhalimu alikuwa anajiona kama masiha wa nchi hii. Wajinga, wasomi uchwara, wajasiriatumbo na makatili walikuwa wanamsifia ile mbaya. Na alishurutisha kuonekana kuwa ni mzalendo wa kweli, kumbe jizi la kura na ibilisi tu.
 
Angekuwa hawapendi wazungu, angewafukuza mabalozi basi mkuu. JPM alikuwa anataka fair play kati ya Tanzania na nchi zingine.
Hakuwa na uwezo huo. Hata wazungu walijua he was just stupid with no impact.

Na kuthibitisha hilo, Tundu Lissu ( Mwanasiasa ambaye Magufuli alimchukia to the moon ) alihifadhiwa kwenye ubalozi wa Ujerumani na badaye wazungu wakamsindikiza kwenda Airport kupanda ndege mchana kweupeee huku akihitajika mahakamani.

Hao wazungu baada ya kumsindikiza wakarudi ubalozi na wako hapa hapa na hakuna kitu Magu angeweza kuwafanya.
 
Hapa nakataa mkuu. Jpm alikua anataka fair business kati ya tanzania na nchi nyingine. Alitaka wananchi wawe na thamani sawa na foreigners. Na kutoa dhana ya cheap labour.
 
Tanzania tuna kasumba ya kusapoti viongozi kuwa ndo uzalendo na kupinga sio uzalendo ,viongozi wa nchii hii mpaka wananchi hawajui wanataka nini kutwa nzima kulalamika tu
Jpm was in a right direction. Kubali tu mkuu. Hata kama hakua smart jinsi ulivotaka ww. Tofautisha kuwa evil smart na kua mzalendo. Its better kua mzalendo. No matter how much upo smart. Lakini kama una misguide wananchi bado hai count.at the end of the day wananchi watakudai basic needs, justice, employment, land
 
Nilikuwa nakusoma Sana Ila ulipotea kwa ghafla mpaka nikadhani pengine ile timu ya Mwendazake ya WASIOJULIKANA imekupoteza. Karibu Sana ROBERT HERIEL
 
Tajiri muungwana kama MO Dewji au mzee Reginald Mengi wakianguki mimi masikini siwezi kufurahi hata kidogo.
Unesahau ile kauli "... matajiri wataishi kama mashetani ilivyowafurahisha maskini?" Umesahau waliokuwa wafanyakazi wa QG walivyoshangilia anguko la tajiri yao? Leo wengi wanalia na kusaga meno maana Bwana yule alifunga biashara zake na wao wakapoteza ajira... wengi wao wanapanga bidhaa barabarani siku hizi ili wajikimu...
 
Gaddafi na Kwame Nkurumah walikuwa madikteta na wote waliondolewa kwa aibu katika nchi zao.
waliondolewa kwa kupigania wananchi wao, je huo ni uovu? Kama fight against corruption and african enemies ni uovu then wema ni upi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…