Kwanini, mbona masufi wako poa sana.
Sema kuna vikundi vya kisufi, mimi xivielewi elewi, Inabidi niviuliziee sana. Isipokua vingine navielewa sana.
Niliwahi kumuuliza babu yangu, yeye Wareika ipi? Akacheka sana, akanambia, bwana mkubwa, mimi tariqa zote, mradi wansema La ilaha ila Allah, mimmi nipo nao.
Sema babu yangu nae alikua ni mtu wa uradi sana, kuna nyiradi nyingi kanifundisha lakini fupi fupi sana. sema za muda mrefu. Nakumbuka alikua anasema usiewe na haraka unapotaka haja yako kwa Mungu, mrasi usichoke kumtukuza na kumtaja.
Nikamwambia mbona mamkuu, yaani binti yake, ana tasbihi kubwa boksi zima. Huyo mamkuu ni mazowea tu kumwita ma mkuu, lakini ni shangazi yangu, baba mmoja mma mmoja na babangu. Mie toaka mdogo naona kila mtu anamwita mamkuu. Nikajua ukubwani, walikua wa kike wengi upande wao na yeye ndio dada yao kina babu yangu na wapo wengi kweli, babake alijua kuzaa, wapo jumla 28 kwa wake wanne, huyo mamkuu ndio wa kwanza kuzaliwa katika matumbo yote manne.
Ndugu zake wa kike nao wamezaa sana, basi watoto wote wanamwita mamkuu, mpaka majirani. Ukienda Usagara tanga, mpaka leo ukiuliza kwa mamkuu wapi utaoneshwa, ndio bado nyumba ya marehemu babu ipo hapo. Mamkuu alikuaAlikua ananipenda sana mimi, mwenyewe alikua utotoni namsikia akisema, huyu msimpeke kulelewa kwa mama zake, huko watamfundisha uchawi na wanga waoi wale. Nilikua sielewi ana maanisha nini, siku hizi nafahamu, mawifi hua picha haziendi. Alikua poa sana lakini, nimekula sana shilingi shilingi zake. Mqwnywei Mungu amehemu.
Huwa tunamtania babu, tunamuuliza tasbihi la dadako umelirithi wewe nini? Anasema wamerithi wanawe, wanaligombania hilo utafikiri la dhahabu, kumbe hawajui nimetengenezea mimi, sema ile nimeichonga kwa kiini cha mizizi ya misandali, haiozi na inanukia mpoaka leo. Nakumbuka kweli boksi lake la mamkuu la tasnihi lilikua linanukia, nikijua analitia mafuta mazuri kumbe ni msandali. Kwa watu wa Tanga misandali wanaijua inavyonukia, ipo kwa baba yangu shamba, marufuku kabisa kuikata, hio, toka mwenyewe yupo hai. Anasema msiikate hii, ina wenyewe. Sijawaju mpaka leo hao wenyewe, ipo mitatu mikubwa sana.