Nimeangusha pesa ya rambirambi 300,000/= cash mchana huu

Wakuu, mchana huu mida ya saa saba nimeangusha Wallet ikiwa na pesa kiasi cha 300,000/= cash. Daaah, roho imeniuma sana aisee na haya maisha yalivyo magumu siku hizi huku mitaani.

Alafu ni mchango wa rambirambi ya msiba wa ndugu yetu aliyefariki kule Bagamoyo, watu 6 wamechangia ambapo kila mmoja alitoa 50,000/= na mimi nikiwa ni mmoja wao. Nikijiondoa mimi hapo ninabaki na deni la 250,000/=

Huu si ndio mwanzo wa kuonekana tapeli aisee? Wakuu, naombeni msaada wenu wa mawazo nifanyaje ili nirejeshe hizi pesa za watu?
Pole sana
 
Jamani
Pole sana

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kwanza poleee..
Ukifanikiwa kutoa hayo maelezo kwa wabongo na wakakuamini bila dot ya shaka...
Utakua nabii asiyejijua

Hata marehemu hawezi kuamini, akisikia hayo maneno atafumbua mdomo,

kwa ufupi hata ungesema umeangusha hio 50k yako tuu hamna atakae amini, sio tu hivyo, hata ambaye hajatoa mchango ni ngumu kuamini.

Mbaya uwe na ka sura ka kisanii sanii kama ka Mtanga, huchomoi...
Na kwenye msiba watu wasiposhiba, utaona vifungu vifungu vya watu vikikuangalia na kuoneshana kwa misunyo.
[emoji2][emoji2][emoji2]
 
Back
Top Bottom