Wakuu, mchana huu mida ya saa saba nimeangusha Wallet ikiwa na pesa kiasi cha 300,000/= cash. Daaah, roho imeniuma sana aisee na haya maisha yalivyo magumu siku hizi huku mitaani.
Alafu ni mchango wa rambirambi ya msiba wa ndugu yetu aliyefariki kule Bagamoyo, watu 6 wamechangia ambapo kila mmoja alitoa 50,000/= na mimi nikiwa ni mmoja wao. Nikijiondoa mimi hapo ninabaki na deni la 250,000/=
Huu si ndio mwanzo wa kuonekana tapeli aisee? Wakuu, naombeni msaada wenu wa mawazo nifanyaje ili nirejeshe hizi pesa za watu?