funzadume ushauri wako una maana kubwa na mafunzo juu. Dah
Ngoja nikueleze kisa kimoja. Kuna siku moja alikuja kijana mmoja mwanafunzi wa chuo kikuu (jina kapuni) akija kuomba msaada wa nauli (kipindi vyuo vimefungwa kwa COVID - 19) na alikuwa anaenda kwao Bukoba. Kijana namjua kwani alikuwa amepanga jirani na kwangu na tulikuwa tunaonana juu kwa juu kwenye sehemu za starehe za kitaani na hata kwenye vibanda vya mpira ambako sometimes naenda ili kupata fleva za ushabiki wa kitaa. Alikuwa mjuaji sana kutokana na elimu yake (nilipenda hii confidence yake)
Sasa kuna siku akaja kugonga geti nyumbani (alikuwa hajui kama ni kwangu) na nadhani kwa elimu yake na ujanja ujanja wake wa kitaa alijua akija na sound zake za Covid 19 na chuo kufungwa ghafla na kutokana na aina ya nyumba basi ataonewa huruma na kupata nauli kirahisi.
Dogo akakaribishwa akaomba kuonana na mwenye nyumba nikaitwa kumsikiliza, alivyotoka na kuniona mimi alishtuka lakini easy akanieleza shida yake nikamwelewa. Alikuwa anataka kama elfu 80 hivi ili kufika mpaka kijijini kwao.
Nilichomwambia kulikuwa na kazi home ya kupandisha mchanga ulishuswa na fuso (mende) lilishindwa kuingia kwenye geti kutokana na ukubwa wake so ulikuwa mchanga mwingi huko nje ya geti kama (trip 3 za mende). So nikamuuliza dogo umepitia jeshini akasema ndio, nikaona huyu atanifaa nikamwambia nakuuzia hiyo kazi kwa 180,000/= ifanye ila wewe ndio uwe mtendaji mkuu na utatafuta vijana wa kufanya nao kazi. Hiyo kazi kwa ukubwa wake ni kama 200,000/= ilitakiwa na mie nilipanga nimpe hiyo kilo 2 ila nilitaka kumpima imani.
Dogo akaja na style ya kuleta wapiga kazi yeye awasimamie but wale jamaa walikuwa wakiona ile kazi na bei yake (maana alikuwa anatoa kwenye makubaliona 80,000/= ya nauli ya kwenda kwao) wanaikataa kwamba haina maslai. Dogo alihangaika kama siku 5 hivi kazi haijaanza na kila siku anakuja na sound kuwa ataifanya ile kazi na mimi nilikuwa nahofia mvua so nikawa namkazia kama hawezi niite vijana.
Mwisho to cut the story short dogo aliifanya ile kazi na vijana wengine wawili ila wote waliipiga asubuhi mpk jioni ndio kwa siku mbili nikawalipa 180,000/= na on top of that nikampa 80,000/= ya nauli aliyoniomba yeye kama yeye. Nilichomwambia ni kwamba kuna funzo kubwa sana nimekupa kwenye kufanya hii kazi lichukue na uishi nalo maisha yako yote hata ukija kupata madaraka au utajiri.
Dogo aliporudi vyuo vilipofunguliwa alikuja na kiroba cha maharage kama zawadi kutoka kwao na mpaka sasa amekuwa kama ndugu yangu
Nimeendika haya kwa kuwa kuna kitu umekiona cha ndani sana na nilitaka kumfanyia pia mleta mada kama angekuwa serious