Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 17,306
- 19,885
- Thread starter
-
- #121
Huyo jamaa yupo katika ignore list yangu kitambo sanaπ π π imagine huyu ndo angekuwa naye ni mmoja wa walio changa hiyo 50,000. Hapo lazima na wewe wangechanga ya kwako
Upo sahihi kabisa mzee baba. Hakuna anayetaka kunielewa katika hawa jamaa zangu 5, alafu ukiangali wote ni "agemate" hivyo wanajua tu huu ni usanii. Afadhali wangekuwa ni watu wazima kwangu wangeweza kuelewa hii situation.Hapo mzee baba kila mtu atakufikiria anavyojua yeye ila waeleze tu watakuelewa
[emoji23][emoji23][emoji23]Ponapona yako wewe jamaa ni ukifika uwambie uzikwe pamoja na marehemu ukiongea vinginevyo utarudi hapa kusimulia.
Ninaona kuna baadhi ya watu wanafanya masihara na hii changamoto yangu, ipo siku yatawakuta pia.[emoji23][emoji23][emoji23]
Unajua hata mimi bado ninawashangaa sana hawa jamaa? Labda wanatumia zile Wallets za vijana wadogo wa secondary.Hivi mko serious kwamba laki 3 haiwezi kukaa kwenye wallet?!
Wee acha tu mkuu. Inauma sana...Mkuu kweli leo umekumbwa,hata kuamkia umesahau.
Asante mkuu...pole sana mkuu
hakuna atakayekuelewa
DuhKama vipi njoo Goba uje uchimbe shimo dogo la chemba ya choo kuna nyumba ninajenga nataka kulitumia kuhifadhia maji nitakupa laki mbili na nusu. Kazi unaweza kuianza hata saa moja usiku mpaka saa kumi na mbili alfajiri nakulipa chako unaenda kusolve hilo soo
Ingekuwa mimi hapo wasingenielewaaa kbsaMchangie hata laki mbili basi mkuu
Lisu kakosa kura moja tayari
Mm Nna Tukio kama Hilo lako Sema mm nilifanyagaUpo sahihi kabisa mzee baba. Hakuna anayetaka kunielewa katika hawa jamaa zangu 5, alafu ukiangali wote ni "agemate" hivyo wanajua tu huu ni usanii. Afadhali wangekuwa ni watu wazima kwangu wangeweza kuelewa hii situation.
Wallet I nakaa mpaka milion bwana Hawa vpUnajua hata mimi bado ninawashangaa sana hawa jamaa? Labda wanatumia zile Wallets za vijana wadogo wa secondary.
Ngoja nikueleze kisa kimoja. Kuna siku moja alikuja kijana mmoja mwanafunzi wa chuo kikuu (jina kapuni) akija kuomba msaada wa nauli (kipindi vyuo vimefungwa kwa COVID - 19) na alikuwa anaenda kwao Bukoba. Kijana namjua kwani alikuwa amepanga jirani na kwangu na tulikuwa tunaonana juu kwa juu kwenye sehemu za starehe za kitaani na hata kwenye vibanda vya mpira ambako sometimes naenda ili kupata fleva za ushabiki wa kitaa. Alikuwa mjuaji sana kutokana na elimu yake (nilipenda hii confidence yake)funzadume ushauri wako una maana kubwa na mafunzo juu. Dah
Pole sana mkuuMkuu, mimi ni kijana mmoja wa kawaida sana. Sema tu mimi ni mdadisi, ninasoma sana vitabu ndio maana ninajua mambo kadhaa hapa duniani hususan kuhusiana na siasa za kimataifa.
Asante sana mkuu, asante kwa kuweka nilichokiona kwenye comment yako ya awaliNgoja nikueleze kisa kimoja. Kuna siku moja alikuja kijana mmoja mwanafunzi wa chuo kikuu (jina kapuni) akija kuomba msaada wa nauli (kipindi vyuo vimefungwa kwa COVID - 19) na alikuwa anaenda kwao Bukoba. Kijana namjua kwani alikuwa amepanga jirani na kwangu na tulikuwa tunaonana juu kwa juu kwenye sehemu za starehe za kitaani na hata kwenye vibanda vya mpira ambako sometimes naenda ili kupata fleva za ushabiki wa kitaa. Alikuwa mjuaji sana kutokana na elimu yake (nilipenda hii confidence yake)
Sasa kuna siku akaja kugonga geti nyumbani (alikuwa hajui kama ni kwangu) na nadhani kwa elimu yake na ujanja ujanja wake wa kitaa alijua akija na sound zake za Covid 19 na chuo kufungwa ghafla na kutokana na aina ya nyumba basi ataonewa huruma na kupata nauli kirahisi.
Dogo akakaribishwa akaomba kuonana na mwenye nyumba nikaitwa kumsikiliza, alivyotoka na kuniona mimi alishtuka lakini easy akanieleza shida yake nikamwelewa. Alikuwa anataka kama elfu 80 hivi ili kufika mpaka kijijini kwao.
Nilichomwambia kulikuwa na kazi home ya kupandisha mchanga ulishuswa na fuso (mende) lilishindwa kuingia kwenye geti kutokana na ukubwa wake so ulikuwa mchanga mwingi huko nje ya geti kama (trip 3 za mende). So nikamuuliza dogo umepitia jeshini akasema ndio, nikaona huyu atanifaa nikamwambia nakuuzia hiyo kazi kwa 180,000/= ifanye ila wewe ndio uwe mtendaji mkuu na utatafuta vijana wa kufanya nao kazi. Hiyo kazi kwa ukubwa wake ni kama 200,000/= ilitakiwa na mie nilipanga nimpe hiyo kilo 2 ila nilitaka kumpima imani.
Dogo akaja na style ya kuleta wapiga kazi yeye awasimamie but wale jamaa walikuwa wakiona ile kazi na bei yake (maana alikuwa anatoa kwenye makubaliona 80,000/= ya nauli ya kwenda kwao) wanaikataa kwamba haina maslai. Dogo alihangaika kama siku 5 hivi kazi haijaanza na kila siku anakuja na sound kuwa ataifanya ile kazi na mimi nilikuwa nahofia mvua so nikawa namkazia kama hawezi niite vijana.
Mwisho to cut the story short dogo aliifanya ile kazi na vijana wengine wawili ila wote waliipiga asubuhi mpk jioni ndio kwa siku mbili nikawalipa 180,000/= na on top of that nikampa 80,000/= ya nauli aliyoniomba yeye kama yeye. Nilichomwambia ni kwamba kuna funzo kubwa sana nimekupa kwenye kufanya hii kazi lichukue na uishi nalo maisha yako yote hata ukija kupata madaraka au utajiri.
Dogo aliporudi vyuo vilipofunguliwa alikuja na kiroba cha maharage kama zawadi kutoka kwao na mpaka sasa amekuwa kama ndugu yangu
Nimeendika haya kwa kuwa kuna kitu umekiona cha ndani sana na nilitaka kumfanyia pia mleta mada kama angekuwa serious
Una akili sana na nimeliona hilo ndio maana nikahadithia hicho kisa ili wengine waone na kujifunza kituAsante sana mkuu, asante kwa kuweka nilichokiona kwenye comment yako ya awali
NOTHING IS GIVEN EVERYTHING IS EARNED!