Nimechoka na matusi ya huyu kaka yangu mwenyewe Miaka zaidi ya 40

Umemaliza Sina cha kuongeza.
 
Ndio kaitwa kwa mjumbe kapiga bangi kwanza. Na pombe kawashA kiredio anaelekea huko tunAsikiliza wataamua nini

Maana majirani wamemshitaki usiku hawalali kwa ajili yake
Huko Mirembe atatulia tuu!
 
Huwezi zima moto kwakuwasha moto
 
Si mpk apimwe mkuu au unampeleka hivyohivyo
Kuna ndugu yetu Tulimpeleka hivyohivyo hatukumwambia Sasa hivi Katulia,shika maneno yangu,sio mzoefu ila ukichaa una stage Nyingi na majina ya kizungu mengia(Dementia,nk)Ulizia madokta watakupa ushauri!
 
Mu-mlete huku tarime hata wiki moja2 alaf alete vag akutane na wakurya walio vurugwa.
 
Suluhu ni nini
Mtu mzima asemeshwi wala hafokewi. Wewe muacheni wala msimsemeshe chochote, akikutukana amka hapo ulipo na uwondoke zako, chochote anachofanya msioonge nae Chochote.

Ukimya wenu ndio ushindii pekee kwenu. Mabaya yake wala msiyatangaze, chochote kuhusu yeye kiwe siri yenu. Mkiweza kuwa wakimya hakika na yeye atabadilika.

Ushauri huu waweza kuwa wakijinga kwako, au kwenu ila ndio majibu ya maswali yenu.
 
Mpelekeni sober
Au mpelekeni Mirembe la sivyo atakuja kuleta madhara makubwa hapo ndani.
Muda mwingine ana matatizo ya saikolojia.
 
Mpaka siku awakate masikio ndiyo mtapata ufumbuzi
 
Mwisho wa siku ndugu tunaonekana tuna Roho mbaya tukimfunga daah ila lazima iwe hivyo
Achana na hao ndugu uhai ni zaidi ya undugu.Bangi ni mbaya sana.Likitokea la kutokea hata serikali itawashangaa kwanini hamkuchukua hatua mapema.

Nishawahi kuweka ndani mtoto wa bamdogo baada ya kuvuta bangi akataka kumkata mapanga mama na baba.Kakaa zero miaka 2 karud amenyooka na saivi ni Raia mwema ni rafiki yangu na ananishukuru
 
Hatujakataa ila sasa vipi akiua mtu ama akija kumuua yeye mwenyewe maana kashasema atakuja kuchoma kiberiti nyumba atuue wote
Hilo ni takwa la kiserikali haamna viongozi wa Serikali hapo mnapoishi wakawasaidia? Mpelekeni ngazi za Serikali kuna mjumbe au balozi wa nyumba 10, mtendaji mpaka mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wenu watamchukulia hatuaa km nyinyi mmemshindwa au km kuna ndugu yenu mkubwa km mjomba aua mtu yoyote anaeweza kumuonya muiteni aje amuonye na kumsikiliza yeye anataka nini
 
Usiseme hivyo mkuu

Hata hivyo hapa anapokaa ni kwetu sisi ni kwa baba yetu na ni nyumba ya Mzee ambayo alishaacha urithi kwa ajili ya sisi watoto zake hivyo share yake haipo

Hapa anakaa tu kwasababu ya mama na ni ndugu yetu hatuwezi kumfukuza
ATAWAUA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…