Damu ni nzito kuliko maji amueni kilicho bora, maana huyo ameshaathirika kisaikolojia , na siyo rahisi kumrejesha katika hali yake , ushauri wangu ingieni kwenye maombi ,pia mchukulieni hatua kali zakupeleka akafungwe huko.
huwenda atajifunza na akirudi mfukuzeni hapo nyumbani asikae na asiruhusiwe ili Dunia imfunze .
Nina ndugu yangu ambaye kitabia tulimhangaikia kila akifanya timbwili tulimuokoa ila tuliponyoosha magoti tuliachana nae , alifanya kosa sehemu akawekwa ndani kwa miezi kama miwili , alitoka kule anajutia ,akakaa kaa mtaani kama miezi 5 akarudia tena sehemu alipopewa afanye kazi akauza mifuko minne ya cement , akauza godoro ⅚ qfl ambalo alipewa alalie , akauza bati 5 zilizokuwamle ndani , akaanza kusakwa sasa akawa amekimbilia mbali.
Kwa kuogopa kuswekwa ndani mpaka sasa nasikia yuko dar na huko akiendeleza ujinga wake ataishia huko maana hana ndugu wala mtu wakumsaidia wala kumshika mkono, kiufupi sisi kama wanafamilia na wanaukoo tuliamua kumuacha ili afanye anachokitaka siku MUNGU akimrejesha katika hali yake basi tutashukuru , kibaya zaidi huyu ndugu yangu ni mtu wa pombe na Kichwa cha pombe hana , na akichanganya wanawake ndo huchanganyikiwa zaidi , na amejaaliwa uongo uongo mwingi mpaka unajiuliza tabia hiyo kaitoa wapi ? Kiukweli ndugu wa namna hiyo hawafai .
Poleni kwa changamoto hiyo , na huo ni mtihani Mwenyezi Mungu aliwapatia lakini nawasihi msimfumbie macho ,kumfunga magereza siyo rahisi akienda kule mtahisi anateseka ila sasa mkimuacha pia kuna siku nzengwe itampeleka au itamuua na mtamkosa .