Nimeguswa na wale wananchi waliookoa watu ajali ya ndege

Ndio maana nilisema katika mazingira ya Bukoba ndege haikuwa mbali, ni mita 200 kwa taarifa za awali.

First responder maana yake siyo mtaalamu . Mathalani Polisi wangapi wana utaalamu wa mambo ya majini?

Hivi yule Polisi aliyesimama hata kuvuta kamba hakusaidia ndio first responder!

Haya mambo unayosoma ni vizuri, lakini ukiyasoma jaribu kuyaelewa yanafanyaje kazi
 
Ulikuwepo ukaona ndege ilijipigiza mbele? Ilijipigiza wapi kiasi cha kufanya hewa iingie ndani..

We ulikuwepo ukaona haijajipigiza? Mkuu ebu punguza izo mambo... hii ni issue serious sana kwenye ichi yetu waliotoa msaada wapongezwe sana wamefanya kazi nzuri yofauti na ivyo hakuna mtu angepona...!!! Hao wataalamu ndo wakina nani?
 
Huo ubishani wa nani ni nani, kafanya nini..ni non issues, uwe na amani na kile unajua wewe, that's all.
 
Kama hujaelewa nilichosema mwanzo tena kwa lugha nyepesi ni tatizo la uelewa kwako mwenyewe..ninaelewa zaidi yako juu ya mv bukoba, wala sina haja kubishana ubishani wa mitaani kama unavyotaka wewe..baki na unachojua, that's all.
Ulitaka kupotosha watu kwamba wavuvi ndio walitoboa meli ya MV Bukoba! Ni uongo!
 
Mkuu wale wananchi utawalaumu bure tu,ukwa kutegemea kuwa wanaufahamu wowote ule wa kutoa msaada wa huduma ya kwanza!!kwenye huduma ya kwanza kuna kitu kinaitwa DRs ABC.
Sio rahisi kwa kila mtu kukifahamu,ukizingatia na aina ya ajali na sehemu ilipotokea,ni kweli kabisa unaweza ukaona kuwa unafanya uokozi kumbe ndio una zidisha athari kwa muhusika,na kwako pia,vile vile hata na eneo la ajali kulifanya liwe hatarishi zaidi.
Mfano leo umeona kuna baadhi ya askari polisi,zimamoto,jwtz wako pembeni kabisa,ambao kulingana na kazi zao,utoaji wa huduma ya kwanza ni kitu ambacho ni lazima,kama sala ya baba yetu(kwa wa kristo)hawafanyi,wananchi wa kawaida ndio wanachakalika kwenye uokozi!!Japo wanaeeza leta madhara lakini heri nusu shari kuliko shari kamili.
 

..Uko sahihi.

..tatizo linaanza na wanaohusika na wenye utaalamu wa uokoaji kutofika kwa wakati eneo la ajali.

..wataalamu na wanausalama kutokufika ndani ya muda mfupi ktk eneo la ajali, ndio kunasababisha wananchi kujiongeza wenyewe na kusaidia, na matokeo yake yanaweza kuwa mazuri au mabaya.

Cc Nguruvi3
 
Yaani wavuvi inaonekana wana akili na msaada mkubwa kwa umma kuliko viongozi wa Serikali.

Shame to you all government officials. Hamna msaada wa maana kwa umma.
Kiongozi anakwenda kuokoa watu waliozama majini ana mwamvuli?
 
Watanzania ndiyo Jadi yetu kupendana ila kuna watu wachache kwa faida zao wanazozijua wenyewe wanajaribu kuondoa hali hiyo lakini leo imejidhihirisha kuwa hawataweza.
 
Hapo hao wenye utaalamu walifika baada ya muda gani?
 
Leo hii wavuvi wamefanya kitu cha kupongezwa na kila mtu mwenye akili timamu watakuja hapa wataalam walio kalili madesa na nadharia zao uchwara za uokozi ambazo hata kuzifanyia kazi haja wahi na bla bla.

Mtu anasema walitakiwa kusubili kikosi Cha uokozi ambacho hakija wahi kuwepo Sasa sijui huyu mtu anazungumzia kikosi gani?

Kesho utasikia wale wapiga makofi wasio jitambua na kauli za pole
 

..kila kunapokuwa na sherehe za kitaifa huwa kuna ' show ' ya maaskari wanaopasua matofali kwa kichwa, kukunja nondo kwa meno, misafara ya silaha nzito-nzito, magari ya deraya, etc etc.

..ungetegemea ktk matukio ya ajali kama hii ya Bukoba vyombo vyetu vitakuwa tayari na msaada utakuwa wa haraka. Lakini leo tumeshuhudia ni kinyume chake.
 
Mkuu Truevote naomba baadhi ya fact uziweke sawa maana kuna mfano unarudia katika kujenga hoja zako

Ebu tuambie nani alitoboa meli ya Mv Bukoba na kwa amri ya nani ?

Na tuambie ni kikosi gani kilifika leo kufanya uokozi nje na wavuvi ?
 
Heshima kwako mkuu Jokakuu kwenye sherehe za kitaifa zile huwa show off za askari wetu ila katika muktadha wa kuwajibika pale panapo tokea majanga huwa kinyume na matarajio ya walio wengi kilicho tokea leo Bukoba kina tukumbusha uzembe wa idara zetu za majanga na namna tulivyo na watu wasio na weledi katika kutimiza wajibu wao bado hatuja sahau tukio la Moto la soko kuu la karia Koo na kituko Cha jeshi letu la zimamoto.

Hili taifa linahitaji mageuzi ya kiutendaji na kiutawala ndo njia pekee iliyo baki
 
Kuna matatizo mengine

Hatuna disaster preparedness hakuna response nzuri yakitokea majanga. Hatuna contingency plan kwasababu viongozi ni myopic, kwamba hatuwezi ku foresee majanga! Tunamsinginzia Mungu! aah hiyo ni kazi ya mungu!

Ofisi ya Waziri mkuu ina idara ya maafa! idara lazima iwe na uwezo wa kutazama uwezekano wa maafa, kwa namna gani na wapi halafu namna ya ku -respond kwa wakati na kwa nyenzo gani.

Ipo katika vitabu tena vimeandikwa na wenzetu sisi tunasoma tu bure! hatuna vyetu

Kwetu, Idara ya maafa inatumika maafa yakitokea kama kuhifadhi miili, kusafirisha n.k.
Hiyo ni sehemu tu lakini si jukumu la kwanza la idara ya maafa

Idara ya maafa katika ofisi ya Waziri mkuu si sahihi, ni mwendelezo tu wa bureacracy
Hivi kweli hakuna boti ya ku patrol ikijiandaa ikiwa kuna tatizo!
Ofisi ya PM haijui kilichotokea ziwa Victoria si mara moja bali mara kadhaa
Hatujifunzi nini kilitokea bahari ya Hindi mara kadhaa

Kwanini tunaweza kuwa na mfuko wa Jimbo na kila Mbunge anapewa mipesa, halafu mkoa hauna kikosi cha uokoaji! Kwani airport ya Bukoba, Musoma au Mwanza si zinajulikana zipo karibu na Ziwa! Fire brigade za maeneo hayo zina vifaa vya kutosha zikiwemo Boat?

Haya mambo ya kuvunja matofali kwa vichwa au kuvuta magari tuyaache, tufikirie namna bora za kujiandaa na maafa! Hili la Bukoba linatuonyesha tusivyo na vipaumbele.

Waziri mkuu, rambi rambi hadi lini? Tunadhani kwa hili la maafa umeshindwa!
 
Ni aibu sana mijiviongozi yetu inatembelea v8 halafu vifaa vya uokozi hamna.
 
Mkuu Truevote naomba baadhi ya fact uziweke sawa maana kuna mfano unarudia katika kujenga hoja zako

Ebu tuambie nani alitoboa meli ya Mv Bukoba na kwa amri ya nani ?

Na tuambie ni kikosi gani kilifika leo kufanya uokozi nje na wavuvi ?
Hakuna mtaalam wa uokozi majini bongo hii anayewazidi utaalam wavuvi. Huyo anayetaka wavuvi wasubiri wataalam hajui uhalisia wa mambo.
 
Ajali zinapotokea zinataka utulivu na subra kidogo ili uokozi ufanyike pasi na kuleta madhara zaidi..papara na haraka haraka mara nyingi zinaongeza madhara.

Uko kinadharia zaidi. Ww ni wale wasomi msio na tija kwenye nchi hii. Ww ni mmoja kati ya wasomi wengi wanaodhidi kuifanya nchi hii kuwa masikini. Hii ndio sababu serikali yetu imebaki kuwa na milolongo isiyo na tija kwa maelezo ya aina hii. Inasikitisha kuwa na wasomi wa aina yako.
 
Aisee Una matatizo Mkuu, Yaani ajali itokee watu washindwe kuokoa wasubiri dk 20 wataalam waje? Are you serious? Hivi unajua changamoto ya miundombinu tuliyonayo?

Sidhani Kama ulishawah kupata ajali hapa Bongo.

Huyu jamaa ndio aina ya watunga sera wetu wengi. Wao wako ofisini hawana uelewa wowote wa uhalisia, bali wamejaa nadharia pekee walizokariri humo madarasani. Matokeo yake wamekuwa wakifunga sera, sheria na miongozo isiyotekelezeka na kuifanya nchi kuwa masikini, huku wakijilipa fedha nyingi katika ya umasikini wetu.
 

Huyo jamaa hizo ndio akili za viongozi wanaonunua maVX na kuweka ulinzi wa kutisha wa viongozi, kisha wanajaza misururu ya magari kwenda kufungua vyumba vitatu vya madarasa! Ni wale wanaotengeneza milolongo kwenye huduma za umma, kwa kisingizio cha kufanya mambo kitaalamu. Hii ndio picha halisi ya watu wanaoitwa wataalamu huko serekalini. Yaani mimi nikishasikia mtu anaitwa msomi na yuko Serekalini, huwa napata kinyaa mara moja.
 
Mkichagu kuongozwa na wanafiki ndo matokeo yake haya.Airport inakosa mkakati wa uokoaji wa majini.Kwa kweli Bukoba Airport wamefeli vibaya.Sasa Emergence kwao ni kuzima moto tu?

Kwa taarifa yako hata ingetokea moto bado wasingezima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…