Nimejiuzulu rasmi nafasi yangu ya Ujumbe wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

Nimejiuzulu rasmi nafasi yangu ya Ujumbe wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

Kuweka rekodi sawa

Next time andika na sababu za kujihudhuru kwako.

Huu ni wakati tunaweka rekodi sawa ya watu wote waliosimama imara dhidi ya udhalimu ili wakati ukifika tuwavike Mataji ya Ushindi.

Kumbuka anaishi Tanzania mkuu. Hapo ataambiwa mchochezi na hatua kubwa zaidi wanaweza kumchukulia hao wanamtandao.
 
Sharp guy!

Acha hao wanaosema maadili yanavunjwa ila wizi ndio maadili kwao.
 
....tangu Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) itangaze kusitisha kwa muda wa siku tisini leseni ya huduma za maudhui mtandaoni iliyotolewa kwa taasisi yake aanayoiongoza ya Vapper Tech Limited (Jamii Forums)...
Aisee pole sana Ndugu WanaJF na Maxence Melo na timu yako kwa kadhia hii. Tupo pamoja.
===
Naomba taarifa rasmi ya TCRA nione hivyo vifungu vilivyokiukwa na JF.
 
Pole sana kwa yote haya JF inapitia na wewe kama Mkurugenzi wake.

It's so sad nchi inapita katika hii trajectory upande wa uhuru wa habari, Haki, usawa wa kidemokrasia nk.

We encourage you to stay focused while at the same time take all precaution about your safety, it's a matter of time everything will be fine.

Nyakati ngumu hazidumu hata kidogo, tutatoka tukiwa washindi hata kama ni kwa maumivu makubwa na kupoteza sana.
 
Jf nashauri iwe registered nje ya nchi,hapa ndani mtasumbuliwa sana
Ni uzalendo na nia njema JF kuwepo hapa nchini walipe kodi Watanzania wapate ajira. Hakuna lisilowezekana wakiamua, kama serikali ya Rais samia itaendelea kuziba masikio na huu uvamizi wa vyombo vya habari hasa JF.
 
Naomba nieleweshwe taratibu jf kupokonywa leseni, yaani itakua haipatikani kabisaa(kufutwa) au tutakua tunaipata ki magendo (vpn)
Maana kichwa kinanizunguka kweli kweli!

Wameipiga pini kama walivyofanya kwa Twitter(X) isipatikane mjini ila kufuta hawawezi! Uzuri JF inapatikana kwa .COM , kama ingekuwa inapatikana kwa .CO.TZ au .TZ hapo sasa kingewaramba!
 
  • Thanks
Reactions: naa
Jf kwangu ni zaidi ya nyumbani kama ikifungiwa siku 90's itakua ni maumivu kwa familia nzima ya watu AMBAO usiku na mchana tumekua humu ndani kama familia tukicheka,elimishana, burudishana, tukipeana pole, tukihabarishana, tukitaniana, tukisaidiana na kuijenga tanzania moja.

NB. Swali linalo bakia kwenye viunga vya akili yangu ni lini wale watu wanao SIFIA SANAAAAAA MPAKA KUPOTOSHA KULAGHAI , KATUFANYIA BULLYING WATANZANIA KWA PROPAGANDA, KEBEHI, DHARAU,DHIHAKA, UFEDHULI KAMA KINA THLAATLAH, CHIEMBE, LUCAS MWASHAMBWA,LUCHA, MTOTO WA SHULE , THE BIG SHOW na wengine wengi ambao huamua kwa makusudiiiii kuponda na kuchafua taswira ya Wana mabadiliko/ mageuzi hata viongozii wa chadema na tundu lissu aliye gerezani kwa uhaini wa mchongo JE kufanya hivyo kwao ni sawa?!

Namalizia na hii nahau ya wahenga wa zamanii.
Mkuki kwa nguruwe kwa BINADAMU MCHUNGUU.
Hayo uliyoyataja aya ya pili ndio maadili kwa mujibu wa akili za akina Msigwa.
 
Max alikosea kupokea uteuzi wa ujumbe wa bodi za kipuuzi, kuna kitu gani anakosa! Hakupaswa kufanya hivyo. Wamemtumia tuu na wala huo ulinzi hautakuwepo ila kwao tuu. Ulinzi upo kwenye maslahi yao sio ya jamii, hawamananishi kama Max alivyofikiri itakuwa. Ni mazingaombwe tuu.

Max amesahau kwamba hii nchi inaendeshwa kwa utashi wa kisiasa "political will" na maslahi ya chama kilichopo madarakani. Ukiyagusa wanakugusa.

Wamemtumia Max kama mtaalam "expert" wakikijua kipaji na exposure yake, huku wanamchora, wamemtumia na huku hawapendi na jukwaa lake hili ambalo, dhima yake inakinzana nao.

Max ameshindwa walau kujua kwamba CCM, hawana rafiki wa kudumu ila wana maslahi ya kudumu na kwakua kagusa maslahi yao na watu wao "wezi wenzao", wamemuadhibu.

Ushauri wangu: Max endelea na initiatives zako, nyakati zinakuja na kupotea, lakini haitakuja nyakati dola ikapenda unachokifanya, ukosoaji, uhuru wa maoni. Haitakuja kutokea kamwe.

Umepoteza hela, nguvu kazi na muda. Muda ambao ungekaa na watoto wako mkacheza uwanjani. Na kama katika ushiriki wako huko rasilimali za JamiiForums zilitumika, basi ulizitumia ndivyo sivyo. Hawana shukrani hao jamaa, ni wanafiki, machawa na wajinga.

Jikite kuijenga JF. Usipeleke nguvu sehemu usiyothaminiwa. Jionee wivu, umetoka mbali, una kila sababu ya kukataa unafiki na viini macho. Wamekuteua wakitaka kuvuna ujuzi na utaalamu wako, na watabaki nao kwenye makaratasi, it will never happen.

Pole sana mkuu, jiandae washapewa maelekezo ya kukudhibiti hao hao, uliokaa nao kitako kwenye matume ya kijinga mkigonga glasi na kucheka.

Chivundu.
 
Back
Top Bottom