Nimejiuzulu rasmi nafasi yangu ya Ujumbe wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

Nimejiuzulu rasmi nafasi yangu ya Ujumbe wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

Wamekuwa wakikanusha uwongo , tena wana sub platform ya jamii check, wamekuwa wakicheki kama. Ni uwongo au ni kweli
Walitakiwa kubana kabisa post kabl ya kwenda public
..Wanakuja kukanusha zaidi ya mwezi huko.
 

Leo, Septemba 06, 2025 nimemuandikia rasmi Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari juu ya uamuzi wangu kujiuzulu ujumbe wa Bodi katika Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Niliteuliwa Disemba 18, 2023 na nimehudumu kikamilifu majukumu yangu. Natoa shukrani nyingi kwa Wizara, Tume, na wajumbe wenzangu kwa ushirikiano mzuri walionipa katika kipindi chote.

Aidha, naishukuru Taasisi yangu na Bodi ya Wakurugenzi kwa kulipa gharama zote za ushiriki wangu katika vikao vyote na shughuli za Tume kwa takribani miaka miwili.
💪🙌
 
Kuweka rekodi sawa

Next time andika na sababu za kujihudhuru kwako.

Huu ni wakati tunaweka rekodi sawa ya watu wote waliosimama imara dhidi ya udhalimu ili wakati ukifika tuwavike Mataji ya Ushindi.
Sababu ni zilezile za polepole
 
Aidha, naishukuru Taasisi yangu na Bodi ya Wakurugenzi kwa kulipa gharama zote za ushiriki wangu katika vikao vyote na shughuli za Tume kwa takribani miaka miwili
Hii spana nimeielewa 🤗
 
Kwa hiyo ukijitoa kwenye bodi ya ulinzi wa taarifa binafsi maana yake sasa hakuta kuwa na ulinzi tena wa taatifa binafsi?au
Pole sana Ndugu Maxence Melo kwa misukosuko uliotokea Jana. Pia nakupongeza kwa uamuzi uliochukua nikiamini umefanya hivyo Kwa msingi wa 'WIN-WIN' kwa pande zote mbili. Kwa maana upande wako ambao sisi,Wana JF, pamoja na wewe tupo hatutathirika na uamuzi huu pia na upande mwingine wa Bodi utaendelea kutekeleza majukumu yake.

Wakati Nawaza, swali kama hilo alilouliza Ndugu chararaa nikaona kwanza nilielewa hii bodi uanzishwaji wake na majukumu yake.

Katika kutafuta taarifa za Bodi ndipo nikakutana hii sheria "SHERIA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI, 2022". Sheria imefafanua uanzishwaji wa Tume ya ulinzi wa taarifa binafsi na majukumu yake pia na uanzishwaji wa bodi na majukumu yake na namna wajumbe wa Bodi wanavyopatikana. Pia nimepitia website ya Tume ni mekosa taarifa nyingi nilizokuwa nahitaji hasa ripoti za mwaka na kadhalika.

Kwa msingi huu nashauri wanaJF wote tusome Sheria hii na matakwa yake na utaratibu unaotumika kukusanya taarifa binafsi kihalali kwa muhusika aliye ndani ya nchi na yule aliye Nje ya Nchi.
 

Leo, Septemba 06, 2025 nimemuandikia rasmi Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari juu ya uamuzi wangu kujiuzulu ujumbe wa Bodi katika Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Niliteuliwa Disemba 18, 2023 na nimehudumu kikamilifu majukumu yangu. Natoa shukrani nyingi kwa Wizara, Tume, na wajumbe wenzangu kwa ushirikiano mzuri walionipa katika kipindi chote.

Aidha, naishukuru Taasisi yangu na Bodi ya Wakurugenzi kwa kulipa gharama zote za ushiriki wangu katika vikao vyote na shughuli za Tume kwa takribani miaka miwili.
Umechukua uamuzi sahihi katika wakati sahihi. Hatua ingependeza zaidi hata kwa media kususia kuandika habari za upande wao ikiwezekana hata kususia mikutano yao wabaki wao na kenge wao.
 
Back
Top Bottom