Wakuu
de Gunner denoo G Titicomb Natafuta Ajira, my golden brother
Robert Heriel Mtibeli na shostie
binti kiziwi naomba tufunge mada yetu kwa nyie kunielewesha tena kuhusu suala la hisia.
Hivi hisia si ndio feelings?
Hapa si ndio kuna mambo ya emotions, ma mood swings na ma stress eeh?
Na wote si tunakubali kuwa hormone imbalance ina affect hisia za binadamu eeh?
Sasa naona wengi wamekubaliana na Robert kuwa kwenye hisia wote tuko sawa ila mimi bado akili yangu imegoma kuona usawa ktk hili sababu
1)Katika siku 30 za mwezi hormones huzigawanya siku za mwanamke kwenye mafungu ya hisia tofauti tofauti.
Siku ya 1-5 hapa tunakua mwezini.Kwa wanawake wengi hizi ni siku za mawenge na hisia za huzuni na hasira.Tumbo,mgongo,kichwa vinauma kizunguzungu no appetite.Binafsi huwa sijisikii kuongea na mtu.
Siku ya 6-13 hapa tunakua kawaida tu.Hormone zinakua vile zinapaswa kuwa.Tunakua na hisia zisizosukumwa na hormones.
Siku ya 14-17 mwanamke huwa na hisia za furaha.Furaha itokanayo na kuongezeka kwa hormone ya estrogene na testosterone.Hapa migenye kama yote.Hisia za migenye pia ni matokeo ya kuongezeka kwa hizo hormones.Utelezi kama wote.Ni kipindi cha ovulation.Ni siku za mahaba.Siku za mood nzuri.Unakua mchangamfu na kind kwa kila mtu.Hapa baba na watoto wote wanamfurahia mama.Hichi kipindi kama baba ni
min -me utaona ananywea mbege zake nyumbani chini ya mti wake wa mparachichi huku akiangalia kahawa na migomba yake kwa mbali.
Siku ya 18-28 siku za karibu na hedhi.Hizi siku asilimia kubwa ya wanawake(sio wote) wanakua na hasira za karibu.Mistress kama yote.Hizi ni siku ambazo baba na watoto kuna ki sauti huwa kiinawaambia(ga) This woman is from hell😃 na kama baba ni
min -me hizi siku atakaa bar hadi afukuzwe na akifika tu home pombe yote inakata na anaingia chumbani kwa kunyata.
Tuachane na jinsi menstrual circle inayumbisha hisia zetu.Tuje kwenye ujauzito.Hormones zinaweza kubadilisha kabisa hisia za mwanamke.Mwanamke anaweza kumchukia mumewe au mwanae fulani na kumpenda mchunga ng'ombe wao kuanzia mimba inatunga hadi anqjifungua.Tukiwa preggo tunakua veery sensitive na harufu.Kitunguu kinaweza kaangwa mtaa wa 3 mimi nikatapika huku.Naweza kupenda au kuchukia jasho la mume wangu.Ikitokea nimelichukia sitatamani kabisa uniguse na 'shetani' /hormone zinaweza fanya nivutiwe na harufu ya shamba boi wetu.Ikitokea hivyo nitakua natamani awe karibu yangu sbb harufu yake inafanya nijisikie vizuri.Inanipa hisia za furaha.
Tukiachana na hayo mjamzito anakua very emotional.Kulia na kufurahia vitu vya kijinga ni kawaida.Wakati niko preggo nilikua nalia kila nikisikia Jotta akiimba ule wimbo wa Worthy is the lamb.Mr. wangu alikua akiusikia tu alikua ananyanyuka anaondoka zake coz alikua akinibembeleza ndo hisia za kulia zilikua zinazidi😃
Baada ya kujifungua kuna wanawake wanapata post natal depression kwa kama miezi sita hivi.
Kumbuka mwanamke atapitia vipindi hivi vya kumyumbisha kihisia kila baadhi ya siku za mwezi na kila miezi 9 ya kila mimba atakayobeba na kila post natal ya kila mimba atakazobeba na hapo bado mazingira ya kumyumbisha kihisia hayajaisha kuna kuzimu ya menopause inamsubiri.
Wote tunajua jinsi menopause inavuruga wanawake kihisia.Mwanamke anakua very unstable emotionally.Anakua mbogo.Hataki kuguswa.Anaweza hata kuhama zake chumba aepuke 'kero' za night vigil na morning glory.Na hapa kama mume ni
min -me hichi ndo kipindi atahamia zake kwenye vilabu vya mbege.Nyumbani atarudi tu kubadili nguo.
Wapendwa wangu niliowakwoti ninawaheshimu na sina shaka na uwezo wa vichwa vyenu hivyo ninaomba mnieleweshe kwa lugha nyepesi bila kutumia viingereza vyenu vigumu vyenye terminologies za havard na university of Massachusetts.Bear in mind mimi ni mwalimu wa chekechea tu hivyo naomba nieleweshwe.
1)Mwanaume ana siku ngapi ambazo naturally tu inatokea zinayumbisha hisia zake ambazo tunaweza kuziilinganisha na siku za za kuyumba kihisia za mzunguko wa hedhi wa mwanamke.?
2)Najua mwanaume habebi mimba ila naomba kujuzwa katika baiolojia ya mwanaume ni kipindi gani maumbile yake naturally tu huvuruga hormones zake na kuvuruga hisia zake kwa miezi 9 au inayokaribia na hiyo.
3)Ni kipindi gani ktk mabadiliko ya mwili wa kiume mwanaume na yeye hupata kitu kinachofanana na post natal depression?
4)Ni kipindi gani mwanaume na yeye huwa unstable and weak kihisia kama awavyo mwanamke aliyeko kwenye menopause.?
Asanteni