Nimekwazwa na bandiko la Robert Mtibeli linalosema eti 'Wanaume na Wanawake wako sawa kiakili', - Siyo kweli

Nimekwazwa na bandiko la Robert Mtibeli linalosema eti 'Wanaume na Wanawake wako sawa kiakili', - Siyo kweli

Mkuu nafikiri unajua kwamba tunawasilisha hoja kwa kufanya generalization sio kuangalia kesi moja moja. In general mwanaume ni jasiri zaidi ya mwanamke, ingawa wanawake majasiri kwa viwango vya wanaume wapo lakini ni wachache sana. There is exception in everything but exceptionality don't count when we generalize.

That's what am talking about
Period
Na hawa jamaa bado wanataka kwenda kwenye angle ya individual..

We are right all along. 💯
 
Mbona hukuviainisha katika bandiko lako la mwanzo?

Ulijua point yako itakuwa na ukakasi kiasi gani kama usonge ainisha hizoo

Sikuwa na hiyo haja.
Hoja ya kibaolojia ameileta prida ndio maana nikaizungumzia mara hii.

Nikisema niandike kila kitu ninachokijua kuhusu mada hiihii pekee ninaweza kujaza Biblia hata tatu
 
Sikuwa na hiyo haja.
Hoja ya kibaolojia ameileta prida ndio maana nikaizungumzia mara hii.

Nikisema niandike kila kitu ninachokijua kuhusu mada hiihii pekee ninaweza kujaza Biblia hata tatu
Sasa mkuu utakuwa unakosea sana

Lazima uangalie mapokeo ya hoja zako, lasivyo utakuwa manipulator
 
Period
Na hawa jamaa bado wanataka kwenda kwenye angle ya individual..

We are right all along. 💯
Kuna swali nimeuliza uko juu, hili kuthibitisha madai kwamba kiakili mwanaume na mwanamke wapo sawa, ni nyanja ipi mwanaume na mwanamke kiwastani wanalingana(let alone mwanamke kumzidi mwanaume). Biashara, teknolojia, sayansi n.k? Hakuna aliejitokeza kuleta jibu.
 
Their ego won't let them...
 
Feminism imeleta hitalafu mpaka kwenye akili za baadhi ya wanaume. Hoja ya bwana mtibeli ni muendelezo ule ule wa kumuuzia mwanamke fantasy ili ajisikie vizuri au ajione na yeye ana umuhimu.

Haina tofauti sana na zile blah blah za "kwenye mafanikio ya mwanaume nyuma kuna mwanamke". Halafu wanaume wanaofanikiwa ni wachavhe sana ukilinganisha na wanaofeli. Sasa hawa wengi wanaofeli nyuma yao kuna nani?

At the end of the day, we realize that dad was right. Hata feminist wenyewe wanampongeza baba yao kwa malezi bora, alaf wakiingia mtaani wanamwita mwanaume Mbwa, Daah hii dunia
 
Wakuu de Gunner denoo G Titicomb Natafuta Ajira, my golden brother Robert Heriel Mtibeli na shostie binti kiziwi naomba tufunge mada yetu kwa nyie kunielewesha tena kuhusu suala la hisia.

Hivi hisia si ndio feelings?
Hapa si ndio kuna mambo ya emotions, ma mood swings na ma stress eeh?
Na wote si tunakubali kuwa hormone imbalance ina affect hisia za binadamu eeh?

Sasa naona wengi wamekubaliana na Robert kuwa kwenye hisia wote tuko sawa ila mimi bado akili yangu imegoma kuona usawa ktk hili sababu

1)Katika siku 30 za mwezi hormones huzigawanya siku za mwanamke kwenye mafungu ya hisia tofauti tofauti.

Siku ya 1-5 hapa tunakua mwezini.Kwa wanawake wengi hizi ni siku za mawenge na hisia za huzuni na hasira.Tumbo,mgongo,kichwa vinauma kizunguzungu no appetite.Binafsi huwa sijisikii kuongea na mtu.

Siku ya 6-13 hapa tunakua kawaida tu.Hormone zinakua vile zinapaswa kuwa.Tunakua na hisia zisizosukumwa na hormones.

Siku ya 14-17 mwanamke huwa na hisia za furaha.Furaha itokanayo na kuongezeka kwa hormone ya estrogene na testosterone.Hapa migenye kama yote.Hisia za migenye pia ni matokeo ya kuongezeka kwa hizo hormones.Utelezi kama wote.Ni kipindi cha ovulation.Ni siku za mahaba.Siku za mood nzuri.Unakua mchangamfu na kind kwa kila mtu.Hapa baba na watoto wote wanamfurahia mama.Hichi kipindi kama baba ni min -me utaona ananywea mbege zake nyumbani chini ya mti wake wa mparachichi huku akiangalia kahawa na migomba yake kwa mbali.

Siku ya 18-28 siku za karibu na hedhi.Hizi siku asilimia kubwa ya wanawake(sio wote) wanakua na hasira za karibu.Mistress kama yote.Hizi ni siku ambazo baba na watoto kuna ki sauti huwa kiinawaambia(ga) This woman is from hell😃 na kama baba ni min -me hizi siku atakaa bar hadi afukuzwe na akifika tu home pombe yote inakata na anaingia chumbani kwa kunyata.

Tuachane na jinsi menstrual circle inayumbisha hisia zetu.Tuje kwenye ujauzito.Hormones zinaweza kubadilisha kabisa hisia za mwanamke.Mwanamke anaweza kumchukia mumewe au mwanae fulani na kumpenda mchunga ng'ombe wao kuanzia mimba inatunga hadi anqjifungua.Tukiwa preggo tunakua veery sensitive na harufu.Kitunguu kinaweza kaangwa mtaa wa 3 mimi nikatapika huku.Naweza kupenda au kuchukia jasho la mume wangu.Ikitokea nimelichukia sitatamani kabisa uniguse na 'shetani' /hormone zinaweza fanya nivutiwe na harufu ya shamba boi wetu.Ikitokea hivyo nitakua natamani awe karibu yangu sbb harufu yake inafanya nijisikie vizuri.Inanipa hisia za furaha.

Tukiachana na hayo mjamzito anakua very emotional.Kulia na kufurahia vitu vya kijinga ni kawaida.Wakati niko preggo nilikua nalia kila nikisikia Jotta akiimba ule wimbo wa Worthy is the lamb.Mr. wangu alikua akiusikia tu alikua ananyanyuka anaondoka zake coz alikua akinibembeleza ndo hisia za kulia zilikua zinazidi😃

Baada ya kujifungua kuna wanawake wanapata post natal depression kwa kama miezi sita hivi.

Kumbuka mwanamke atapitia vipindi hivi vya kumyumbisha kihisia kila baadhi ya siku za mwezi na kila miezi 9 ya kila mimba atakayobeba na kila post natal ya kila mimba atakazobeba na hapo bado mazingira ya kumyumbisha kihisia hayajaisha kuna kuzimu ya menopause inamsubiri.

Wote tunajua jinsi menopause inavuruga wanawake kihisia.Mwanamke anakua very unstable emotionally.Anakua mbogo.Hataki kuguswa.Anaweza hata kuhama zake chumba aepuke 'kero' za night vigil na morning glory.Na hapa kama mume ni min -me hichi ndo kipindi atahamia zake kwenye vilabu vya mbege.Nyumbani atarudi tu kubadili nguo.

Wapendwa wangu niliowakwoti ninawaheshimu na sina shaka na uwezo wa vichwa vyenu hivyo ninaomba mnieleweshe kwa lugha nyepesi bila kutumia viingereza vyenu vigumu vyenye terminologies za havard na university of Massachusetts.Bear in mind mimi ni mwalimu wa chekechea tu hivyo naomba nieleweshwe.

1)Mwanaume ana siku ngapi ambazo naturally tu inatokea zinayumbisha hisia zake ambazo tunaweza kuziilinganisha na siku za za kuyumba kihisia za mzunguko wa hedhi wa mwanamke.?

2)Najua mwanaume habebi mimba ila naomba kujuzwa katika baiolojia ya mwanaume ni kipindi gani maumbile yake naturally tu huvuruga hormones zake na kuvuruga hisia zake kwa miezi 9 au inayokaribia na hiyo.

3)Ni kipindi gani ktk mabadiliko ya mwili wa kiume mwanaume na yeye hupata kitu kinachofanana na post natal depression?

4)Ni kipindi gani mwanaume na yeye huwa unstable and weak kihisia kama awavyo mwanamke aliyeko kwenye menopause.?

Asanteni🙏
Mada yako niliisoma vizuri tu, nikahitimisha ulikuwa sahihi kwenye maeneo yote uliyozungumzia.

Hata kwenye suala la hisia ulivyozungumzia hapa, na ulivyozungumzia mwanzo wa mada yako, kote naendelea kuona upo sahihi.

Suala la hisia kwa mwnaume lipo kama lilivyo kwa mtoto wa kike, tofauti kubwa inayokuja kwa pande hizi mbili kuhusu hisia ni chanzo na muda wa kukaa na hisia tofauti {mood swing}.

Wakati kwa upande wa wanawake, yapo mambo ya kibiolojia kama ulivyoandika hapo juu yanayoweza kumfanya hisia zake zikabadilika kwa muda mrefu, mfano pregnancy.

Hivyo basi, kwa upande wa mwanamke, hisia zake zaidi hubadilishwa na mambo yanayotokea ndani ya mwili wake, mambo ambayo humchukua muda mrefu mpaka aje kukaa sawa.

Lakini, kwa upande wa mwanaume, jibu ni simple tu, opposite ya kile kinachotokea kwa mwanamke, ndicho kinachotokea kwa mwanaume.

Maana yangu ni hii, wakati kwa mwanamke mabadiliko ya kihisia mostly husababishwa na mambo yanayotokea ndani ya mwili wake, lakini kwa mwanaume husababishwa na yanayotokea nje ya mwili wake.

Hii zaidi ni kwa sababu ya tofauti ya kimaumbile; wanaume hatuna period, hatubebi mimba, wala hatuna matatizo yoyote yanayotukuta baada ya kujifungua. Hivyo muda ambao mood ya mwanaume ina badilika ni mfupi zaidi ya muda ambao mood ya mwanamke hubadilika.

Mfano, mimi kama mwanaume, mood yangu mostly huwa inabadilika endapo "nitafulia", hili nimesha prove mara nyingi sana, nina ushahidi wa kutosha.

Pale ambapo nakosa hela nakuwa sijiamini, nina hasira, akili haijatulia muda wote, hii ni kwasababu nature yetu ni kutoa kwa ajili ya mahitaji ya nyumbani. Sasa itakuwa vipi nyumbani wakitaka halafu wewe mtoaji huna?!

Lakini basi, kama itatokea nikawa stable financially kwa muda mrefu, basi mimi muda mwingi hata miezi nane mfululizo nakuwa mtu wa kawaida tu, labda itokee kuvurugwa nyumbani au kazini ambapo hata hivyo hasira zake huchukua muda mfupi sana naendelea na mizuka yangu, ukinitibua home naenda bar kupata sina habari.

Lastly prida nakubaliana nawe ulipompinga @ mtibeli aliposema hisia za mwanaume na mwanamke ziko sawa, hapana alikosea, hisia za mwanamke zinayumba yumba kama mawimbi ya bahari ukilinganisha na hisia za mwanaume, hii ni fact worldwide.
 
Mkuu Prida, binti Mrembo.

Huu mjadala uliouleta umekuwa mzuri sana. Na ninachoshukuru Matusi hayakupewa nafasi kubwa.

Kimsingi mimi ni wale watu ninaopenda kujadili jambo kwa hoja.
Napenda hoja kwa sababu inapanua ubongo.

Tukirudi kwenye uzi wetu;

Moja ya makosa makubwa yanayofanywa na watu wengi ni kujadili jambo katika angle moja. Kutafsiri jambo katika muktadha mmoja.
Mfano, mtu anaelezea hisia au akili katika angle ya kifalsafa basi anafikiri akili kifalsafa ni sawa na akili kisaikolojia au kibaolojia. Hili ni kosa kubwa.

Kwa upande wako, nakubaliana na sehemu moja muhimu uliyosema: kweli mwili wa mwanamke una vipindi vingi vya mabadiliko ya homoni ambavyo vinaweza kuathiri hisia. Hili halina ubishi. Hedhi, ujauzito, baada ya kujifungua na menopause vinaweza kuleta mabadiliko makubwa ya kihisia.
Lakini hapa ndipo tofauti yetu ilipo. Hoja yangu haikuwa kwamba mwanaume na mwanamke wanapitia mabadiliko ya mwili yanayofanana. Hapana. Kibiolojia kuna tofauti kubwa. Hoja yangu ilikuwa kuhusu uwezo wa hisia na akili(saikolojia).

Hisia siyo tu kubadilika kwa mood kwa sababu ya hormones. Hisia ni uwezo wa kuhisi furaha, huzuni, upendo, huruma, hofu, maumivu, wivu, huruma kwa wengine na kuathirika na mazingira. Hapa mwanaume na mwanamke wote wana mfumo wa ubongo unaoweza kufanya hayo.

Mfano rahisi: Mwanamke anaweza kulia kwa sababu ya mabadiliko ya homoni, lakini mwanaume anaweza kulia kwa sababu ya msiba, kupoteza mtoto, kuvunjika moyo au presha ya maisha kama kukosa pesa. Tofauti inaweza kuwa namna wanavyoonyesha hisia, si kwamba mmoja ana hisia na mwingine hana.

Pia mwanaume ana hormones zake. Testosterone, cortisol na mabadiliko ya maisha yanaweza kuathiri mood, hasira, msongo wa mawazo na nguvu za kihisia. Tatizo ni kwamba jamii nyingi zimemfundisha mwanaume kuficha hisia zake, hivyo tunaweza kudhani hana hisia nyingi.
Pia jamii kuna maeneo zimemfundisha mwanamke kuficha hisia zake kama vile mwanamke anatamani na anamtaka mwanaume fulani lakini ataambiwa hatakiwi kumtongoza au kueleza hisia zake kwa kuitwa malaya. Lakini sio kwamba wanawake hawana hisia na hawawezi kutongoza.

Kuhusu swali la siku 30 za mwanaume: mwanaume hana mzunguko wa hedhi kama mwanamke, hivyo huwezi kuweka kalenda inayofanana. Lakini kutokuwepo kwa mzunguko huo hakumaanishi hana mabadiliko ya kihisia.

Kuhusu ujauzito na postnatal depression, ni kweli mwanamke hubeba mzigo mkubwa wa kibaiolojia ambao mwanaume hana uzoefu nao kwani wanaume sisi hatuzai watoto. Hapo mwanamke ana changamoto za kipekee. Lakini tunapozungumzia uwezo wa akili na hisia kwa ujumla, hatuwezi kusema mmoja ameumbwa juu kuliko mwingine.

Kwa kifupi: mwanaume na mwanamke wote wana uwezo sawa wa kuhisi, kufikiri na kuathirika kihisia. Tofauti kubwa ipo kwenye namna miili yao inavyofanya kazi na namna jamii inavyowafundisha kuonyesha hisia.

Nafikiri nimeeleza katika kiwango chakueleweka
Niwe tu mkweli.
Hujanipa majibu ya maswali yangu.
Unanichanganya kwa kuandika vitu vingi vinavyonichanganya tu na pia hata wewe vinakuchanganya coz kuna saa paragrafu zako zinapingana na kuna saa unataja vitu ambavyo havifit maswal yangu.Halafu kuna saa nahisi una lines zako ni kama kila ukinijibu ni lazima uzitumie hata kama hazifit.Sasa hiyo line yako ya kusema "jamii ina imani potofu kuwa mwanaume hatakiwi kulia".

Sasa hiyo inafit vipi maswali yangu?Au kisa mie madam wa day care ndo unanipa customized lines unaniwekea kila ukinikwoti.

Umekubaliana na mimi kuwa mwili wa mwanamke una mabadiliko mengi yanayoathiri hisia zake kulinganisha na mwanaume ila paragrqfu yako ya mwisho umeimaliza kwa kusema pamoja na yote hayo wako sawa kihisia.Inawezakanaje sasa?

Kwani we mpare ukikubali tu kuwa umechemsha kuwa mwanamke na mwanaume hawako sawa kiakili wala kihisia utapigwa ban ya kula makande?😃
 
Kuna swali nimeuliza uko juu, hili kuthibitisha madai kwamba kiakili mwanaume na mwanamke wapo sawa, ni nyanja ipi mwanaume na mwanamke kiwastani wanalingana(let alone mwanamke kumzidi mwanaume). Biashara, teknolojia, sayansi n.k? Hakuna aliejitokeza kuleta jibu.
Hawajajitokeza kwa sbbu hawapo. Mfano hai. Kipindi tuko chuo zamani sana huko. Hostel za wasichana zilikuwa mbili wakati za wanaume zilikuwa sita. Na wanaume wanabebana wakati wanawake wengi hawabebani. So ukiangalia kwa harakaharaka mfumo wa elimu ya juu tayari una shortage ya wanawake.
 
Mada yako niliisoma vizuri tu, nikahitimisha ulikuwa sahihi kwenye maeneo yote uliyozungumzia.

Hata kwenye suala la hisia ulivyozungumzia hapa, na ulivyozungumzia mwanzo wa mada yako, kote naendelea kuona upo sahihi.

Suala la hisia kwa mwnaume lipo kama lilivyo kwa mtoto wa kike, tofauti kubwa inayokuja kwa pande hizi mbili kuhusu hisia ni chanzo na muda wa kukaa na hisia tofauti {mood swing}.

Wakati kwa upande wa wanawake, yapo mambo ya kibiolojia kama ulivyoandika hapo juu yanayoweza kumfanya hisia zake zikabadilika kwa muda mrefu, mfano pregnancy.

Hivyo basi, kwa upande wa mwanamke, hisia zake zaidi hubadilishwa na mambo yanayotokea ndani ya mwili wake, mambo ambayo humchukua muda mrefu mpaka aje kukaa sawa.

Lakini, kwa upande wa mwanaume, jibu ni simple tu, opposite ya kile kinachotokea kwa mwanamke, ndicho kinachotokea kwa mwanaume.

Maana yangu ni hii, wakati kwa mwanamke mabadiliko ya kihisia mostly husababishwa na mambo yanayotokea ndani ya mwili wake, lakini kwa mwanaume husababishwa na yanayotokea nje ya mwili wake.

Hii ni kwa sababu wanaume hatuna period, hatubebi mimba, wala hatuna matatizo yoyote yanayotukuta baada ya kujifungua. Hivyo muda ambao mood ya mwanaume ina badilika ni mfupi zaidi ya muda ambao mood ya mwanamke hubadilika.

Mfano, mimi kama mwanaume, mood yangu mostly huwa inabadilika endapo "nitafulia", hili nimesha prove mara nyingi sana, nina ushahidi wa kutosha.

Pale ambapo nakosa hela nakuwa sijiamini, nina hasira, akili haijatulia muda wote, hii ni kwasababu nature yetu ni kutoa kwa ajili ya mahitaji ya nyumbani. Sasa itakuwa vipi nyumbani wakitaka halafu wewe mtoaji huna?!

Lakini basi, kama itatokea nikawa stable financially kwa muda mrefu, basi mimi muda mwingi hata miezi nane mfululizo nakuwa mtu wa kawaida tu, labda itokee kuvurugwa nyumbani au kazini ambapo hata hivyo hasira zake huchukua muda mfupi sana naendelea na mizuka yangu, ukinitibua home naenda bar kupata sina habari.

Lastly prida nakubaliana nawe ulipompinga @ mtibeli aliposema hisia za mwanaume na mwanamke ziko sawa, hapana alikosea, hisia za mwanamke zinayumba yumba kama mawimbi ya bahari ukilinganisha na hisia za mwanaume, hii ni fact worldwide.
asante sana nafurahi sana kuona mpo mlionielewa.Hivyo ndivyo haswa nilichomaanisha.

Na tukija kwenye factors za kuyumbisha hisia za mwanaume ambazo umesema zinatokea nje ya mwili wake yaani sio za kibaiolojia cha kusikitisha ni kwamba factors hizo humyumbisha mwanamke pia.Mkuu mimi nikifulia hata nikipaka lipstic haikai vizuri.😃.

BTW:Nina uhakika hapo ulipo "hujafulia" coz kichwa kilichowaza haya uloyaandika kinaonekana kiko ktk utulivu mkubwa na ndo mana nimeghairi kukutumia japo ya ka bia😃na niseme tu kwa reply yako hii nimejua walionielewa wamenielewa na ambao hawajanielewa sina cha kuongeza wanielewe🙏
 
Maelezo yako ni marefu lakini unajipinga wewe mwenyewe. Tuseme tu ukweli umekataa kukubali kwamba haupo sahihi. Kilichobaki kwako ni kufanya siasa tu hapa.

Kiakili na kihisia mwanaume na mwanamke wana tofauti kubwa sana, mfano kwanini mwanaume ni jasiri na mwanamke ni muoga? kwa sababu kihisia na kiakili wametofautiana. Wangefanana kwenye hivyo vitu viwili basi wote wangekua majasiri au wangekua waoga
Nahisi hii style ya maelezo marefu yasiyofit hoja ni kama mbinu ya mtibel ya kumchanganya mpinzani wake.

Binafsi naona hanipi majibu yangu ananichanganya tu.
 
Mkuu nafikiri unajua kwamba tunawasilisha hoja kwa kufanya generalization sio kuangalia kesi moja moja. In general mwanaume ni jasiri zaidi ya mwanamke, ingawa wanawake majasiri kwa viwango vya wanaume wapo lakini ni wachache sana. There is exception in everything but exceptionality don't count when we generalize.

That's what am talking about
Naam.
Asante mkuu🙏
 
Sikuwa na hiyo haja.
Hoja ya kibaolojia ameileta prida ndio maana nikaizungumzia mara hii.

Nikisema niandike kila kitu ninachokijua kuhusu mada hiihii pekee ninaweza kujaza Biblia hata tatu
Hoja ya kibaiolojia isingeweza kukwepeka kaka.
 
asante sana nafurahi sana kuona mpo mlionielewa.Hivyo ndivyo haswa nilichomaanisha.

Na tukija kwenye factors za kuyumbisha hisia za mwanaume ambazo umesema zinatokea nje ya mwili wake yaani sio za kibaiolojia cha kusikitisha ni kwamba factors hizo humyumbisha mwanamke pia.Mkuu mimi nikifulia hata nikipaka lipstic haikai vizuri.😃.

BTW:Nina uhakika hapo ulipo "hujafulia" coz kichwa kilichowaza haya uloyaandika kinaonekana kiko ktk utulivu mkubwa na ndo mana nimeghairi kukutumia japo ya ka bia😃na niseme tu kwa reply yako hii nimejua walionielewa wamenielewa na ambao hawajanielewa sina cha kuongeza wanielewe🙏
Dah, kweli kumbe na nyie mnafulia pia!.

Ndio maana huwa nawashangaa wanaume wanaojibizana na wanawake.
 
Hawajajitokeza kwa sbbu hawapo. Mfano hai. Kipindi tuko chuo zamani sana huko. Hostel za wasichana zilikuwa mbili wakati za wanaume zilikuwa sita. Na wanaume wanabebana wakati wanawake wengi hawabebani. So ukiangalia kwa harakaharaka mfumo wa elimu ya juu tayari una shortage ya wanawake.
na kwanini kuwe na shortage ya wanawake katika nyakati za usawa wa kijinsia? na hata ukiangalia population ya wanawake na wanaume ni almost inalingana. Sensa ya mwisho tuliambiwa wanawake wapo wengi zaidi Tanzania.

Ukweli ni kwamba tunachokiita shortage, sio shortage bali ni disqualification. Tunavyo-adress suala la ubaguzi wa kijinsia kuna eneo tunaliluka. Tunashindwa kutofautisha descrimination na disqualification.

Mfano, Tanzania hakuna mfumo uliowekwa kumzuia mwanamke kuwa dokta, injinia au computer scientist, lakini kuna wanawake wachache sana kwenye hizo nyanja. Kwanini? Kwa sababu wengi wao uwezo wao wa kitaaluma hawauwezi ule mziki wa PCM na PCB. Sasa hiyo sio descrimination, ni disqualification.

Tukitaka kulazimisha namba za wanaume na wanawake ziwe sawa, ndipo tunalazimika kulegeza vigezo upande wa mwanamke(ndicho kinchofanyika kwa sasa na kuitwa usawa wa kijinsia) . Matokeo yake tunapata wanawake wengi ambao ni incompetence. Hata kwenye nyanja nyingine ni hivyo hivyo. Women became too empowered, and that have ruined society.
 
Back
Top Bottom