Nimemfumania mchumba wangu je nimsamehe niendelee na mipango ya ndoa?

Hapo kweli nilikosea hila alikataa sio yeye baadae akakubali ndio akasema yule shemeji yake alikua nae
Huyo Muongo kama kweli alikua shemeji yake ulivyosema uliwaona angekuuliza kwanini hujaenda kuwasalimia na ujapiga simu, na kabla ya kwenda huko angekupa taarifa kama ataenda sehemu A na kama upo karibu mkutane.
 
ningekuwa karibu na wewe yaani ningekuchapa vibao fulani kwanza,,, pyumbafu wewe, miezi 7 hujadunga sindano, eti nipo njia panda,,,, ya wapi himo au madale???....eti namhudumia... we ni babake???, muoe akunyoroshe vizuri ndezi wewe............tumia mbinu ugonge angalau ufaidi huduma zako,,, then sepa......
 
Mwanetu miezi saba hujala kamdinyo😅😅😅🙌
Bwege mtozeni wewe ngoja unyooshwe..
 
hapana kaka ndio maana nimeomba ushauri
Mkuu kwani una mpenzi mmoja tu?
Ninavyojua Sisi Wanaume tukitaka kuoa tunakua na Top ten zetu kwahiyo namba moja ikizingua unaondoka na namba mbili, kwa jinsi aliilivyo unatakiwa undone na Mwingine huyo mteme
 
What if wakati unamtongoza alikuwa ndio jamaa yake? Maana sidhan kama alikuwa anakusubiri wewe hapo nilazima anatafuta mbinu za kumwacha jaama yake taratibu 🤣🤣🚴🏻‍♀️🚴🏻‍♀️
Hili nalo neno
 
Siku ya barua, mwambie dada yake aje na huyo mume wake au akupe namba ya dada umuulize kuhusu yeye kuwa na mume wa dada yake kwenye siku husiks😛😛😛
Mkuu Dada yake anaweza kuja na huyo Bwana aliyemkuta na Mpenzi wake unajua wanaweza kupanga vizuri, We unajua kama lazima huyo Dada yake wanajuana vizuri na huyo Mwanaume inawezekana hata huyo Mwanaume ndiyo anakubalika na anapendwa na shemeji zake kuliko huyo mtoa posa.
 
Tumia akili kama mwanaume na si mvulana
 
Mchumba ni mwekezaji huwa hafumaniwi mpaka siki ya harusi, kipindi hiki nyie wote ni wazinzi mnastahili kubondwa mawe mpaka mfe.
Hivi sasa wewe una my sweetie, my gf, my wife, mshikaji wangu na makolokolo mengine halafu unatuambia eti umemfumania! Utoto huo.
 
hapana alikua na mwanaume mwengine mazingira yanaonyesha ni bwanake
dada yake nnamfaamu hila hajaolewa inamaana km shemeji yake ni boyfriend wa dada yake
Once a cheater always a cheater.
Unaelekea kuyakanyaga ukisamehe haraka haraka.

Hapo cha msingi tangaza kusitisha mchakato kwa muda.

Kama huyo mwamba ni boyfriend wa dadaake kweli utajua kwa uhakika, maana wote pamoja na huyo jamaa, dada, mama, nk wataandamana kuja kwako kufunguka kila kitu.. Wakishindwa kukushawishi piga chini mazima. Bora lawama kuliko fedheha
 
Pole sana kwa kuumizwa kimapenzi. Angekuwa mkweli angekujulisha kuwa hamtaonana kwa sababu ana miadi ya kukutana na Shemeji yake (Mpenzi/Mume wa Dada yake). Lakini kwa maneno yake amekudanganya. Hivyo. muache haraka ili waendelee kuyajenga na Shemeji yake.
 
Pole sana kwa kutapeliwa.

Huyo mchumba wako ni tapeli wa mapenzi
 
Zamani tulikuwa tunawaita washika pembe,

Endelea kushika pembe, wengine waendelee kukamua
 
Ukisikia watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri ni pamoja na wewe, umeona red flag zote tena mapema kabla hujaingia kwenye ndoa halafu unakuja kuomba ushauri , wewe bado hujawa na sifa za kuwa mwanaume,
 
Avhana naye kabla ujatoa kilio kama ambulance ya halmashauri ya mpanda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…