Nimempiga mke wangu milioni 2 kizembe sana

Kijana una muibia vipi mtu ambaye unamlisha, unamvisha, una muhudumia, unamsimamia na yasiyo kuwa hayo ? Au mkeo ndiyo muendesha nyumba ?
 
Yani haya maishaa ya wanaume tuna changamoto sana ila inabdi tuwaelewa tu wanawake...!! Kama akiwa na hela ukikwama anakusaidia bhasi huyo ni mkeee pia hata ukimdanganya akukopee lakini Hajawahii kuidai hiyo helaa bhasi Muoeee...!!
 
Ila binafsi utegemezi pesa ya mtu sijui naonaje tena mwanamke
Naona kuliko nimwombe pesa mwanamke kama shida kweli imenibana ni bora nimwombe mzazi wangu anisaidie
Bhasi hujapata mwanamke sahihi badooo...!!
 
Ngoja uje uletewe taarifa mkeo kajenga nyumba kisiri utuletee mrejesho.
Wanawake ni wasiri sana na wanapotoshana sana wakikutana tegemea chochote kutoka kwao.
Hawana siri lakini hawana uwezo wa kuficha siri pia
 
Mbona ulivyompa hio idea alitoa hela? Au ukimuuliza huwa anasema hana hela? Kukubali kutoa hela yake kununua shamba ameonesha Hana issue.
 
Yani haya maishaa ya wanaume tuna changamoto sana ila inabdi tuwaelewa tu wanawake...!! Kama akiwa na hela ukikwama anakusaidia bhasi huyo ni mkeee pia hata ukimdanganya akukopee lakini Hajawahii kuidai hiyo helaa bhasi Muoeee...!!
Na pale niliamua nimuombe ili kumpima tu imani baada ya kugundua anapesa nyingi, ingetokea akaninyima ningesononeka sana kujua hanijali.
 
Yaani tatizo Ni kubwa,,kuishi na mwizi ndani Ni Bora kuficha tu hiyo laki mwizi ajue Kuna sabini tu.
Shenzee kabisa Joannah Ahahahahahahaaaa..!! Kwani huwa mnaogopa kuibiwa? Wala si kuibiwa, nyie hata LUKU ikiisha na upo nyumbani, kutoa hela yako kununu LUKU ni shida. Utampigia simu mtu yupo safarini hukoo anunue LUKU
 
Shenzee kabisa Joannah Ahahahahahahaaaa..!! Kwani huwa mnaogopa kuibiwa? Wala si kuibiwa, nyie hata LUKU ikiisha na upo nyumbani, kutoa hela yako kununu LUKU ni shida. Utampigia simu mtu yupo safarini hukoo anunue LUKU
Mwanamke anaweza kukuomba umnunulie vocha na kwenye simu yake ana salio la tigopesa au mpesa..
 
Nyakati na zama zimebadilika....hatuwezi kuishi kwenye zama hizi tukiwa na fikra na mawazo ya zama za mawe.....

Zama hizi jukumu la utafutaji lipo kwa wote na sio mwanaume peke yake hivyo basi kama kila mmoja anaingiza kipato hivyo anawajibika kwenye Ujenzi wa familia kwa Hali na Mali...kama mwanamke anaingiza kipato basi anawajibika kumsaidia mumewe baadhi ya majukumu hii inaleta mshikamano na kuongeza upendo ndani ya familia........

Zamani mwanamke alikuwa hana kipato hivyo jukumu la kuhudumia familia linabakia kuwa la mwanaume lakini sio kwa zama hizi ambapo jamii inatoa fursa sawa kwa jinsia zote mbili.......

Ukiona mkeo anajiweka kando kwenye mambo yanayojumuisha muskatabali mzima wa familia yenu basi ujue huyo mkeo mpo naye kimwili tu na sio kiroho na kiupendo.......

Mwanamke akiwa kama mwenza wa familia sio mpaka umuambie namna ya kiwajibika kwani anaona na anakujua mumewe hivyo sehemu unayokwama anaweza kutatua bila hata ya kumuuliza....ubinafsi ni dalili ya anguko la ndoa....... kwenye ndoa wote mnatakiwa muwe na dira na lengo moja.........

Kuishi na mwenza mbinafsi ni hatari sana

NB;
Wanaume tunapaswa tuweke mbele uwazi ili kuwa mfano kwa Wenzetu........
 
shida wanaume hatuwi wawazii mkuu mtu unajua kabisa hela ushatumia kwenye mambo ya kifamiliaa sijui kulipa kodi mara adaa lakini unashindwa kummwambia mwenzio nimekwamaa... mwanamke nae akikuomba hela unaona bora ukope umridhishe yeye kuliko kusema ukweli hela hunaa
 
Mimi ninachojua mama lazima uwe na bajeti siku vimebuma kabisa kabisa nitatoa kama hapo kaumwa umemtumia 2 m it's okay si ilikuwepo? Otherwise front seat tunaominya Hela mpambane Tu msitupigie mahesabu.
 
nitarejesha vipi hela ambayo imetumika kwenye matumizi halali ya familia
Suala siyo kurejesha suala ni kumuibia unae mlisha, ndiyo maana nimekuuliza au mkeo ndiyo muendesha nyumba. Kama msimamizi ni yeye hapo sawa, lakini kama msimamizi ni wewe hapo umejipiga mwenyewe na hujampiga mkeo.
 
Maisha hayakuchapa ipasavyo. Siku yakikuchapa ipasavyo lazima utajiuliza maswali kwanini mali za mkeo si sehemu ya mali za familia, na utastaajabu sana jinsi mfumo haupo fair.

Unamuuguza, unakopa hadi unaweka bond nyumba lkn yeye kakalia 5M hata hakwambiii! Imagine this situation! Mnaosema hamuwezi tamani vipato vyao, hilo ni kweli kama tu una kipato kikubwa sana na maisha yapo smooth. Kwa mazingira hayo huwezi fikiria hata kidogo alichonacho mkeo. But when things goes the other way around lazima utarudi kwenye akiba za mkeo...
 
Acha mawazo ya kizamani. Zama hizi zimebadilika, mambo ni 50 kwa 50. Wanawake ni wabunge, ni majenerali ni ma rais. Mwanamke si yule kiumbe dhaifu uliyemfahamu hapo zamani. Hizi si zama za mwanamke anakaa nyumbani kulea watoto na kuangalia nyumba halafu mwanaume anaenda kutafuta kwa ajili yake na familia. Hizi ni zama ambazo asubuhi mke na mume mnatoka mnamwacha dada wa kazi na watoto mnaenda kazini! Hivyo, kama wote mnatafuta, basi jua wote mnawajibika. Nyakati zimebadilika, Usikariri

Kwa kuongezea, mwanamke anayekupenda na mwenye nia ya kujenga familia nawewe mpaka kufa, lazima atashiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa familia.
 
Mwanamke anayekupenda na mwenye nia ya dhati ya kuijenga taasisi ya familia na wewe hamuwezi kufikia huko kwani hilo jambo linajadiliwa kwa upana na kufikiwa muafaka mapema kabisa....na kila linaloendelea litakuwa kwenye mpango kazi mliojiwekea.......nasisitiza tena uwazi ni jambo la msingi sana kwenye ndoa.......huwezi kumhukumu mkeo kwa jambo ambalo hata wewe hulifanyi......wakati mwingine ubinafsi sisi ndio tuwafundisha wanawake kwa matendo yetu..... wakati mwingine anachohitaji mwanamke ni kuhakikishiwa tu uhakika wa kujenga familia na wewe kupitia matendo yako.........Imani hiyo inapotea na kuisha kutokana na mtiririko wa matukio yaliyokithiri ya uzinzi na uasherati.....hali hiyo inamfanya mwanamke ajiondoe kwako taratibu kimipango na kujijengea yeye mwenyewe kwa manufaa ya watoto wake.........anaweza kujituma kujijenga na wewe alafu wakaja watoto saba wa nje nao wakidai mgao......
 
Mi nashangaa watu wanaongea habari za moral authority lkn wengi wao wana michepuko au wamewahi kuwa na michepuko. Hivi mnajua huo nao ni wizi? Ni sawa na umeiba penzi la mkeo na kupeleka kwengineko. Hivyo, mnavozungumza hapa muhakikishe mpo clean dhidi ya makandokando.

NB. Sitetei wizi. Jamaa aliatakiwa amchane mke wake kuwa kwanini anaficha pesa yeye anahangaika kukopa huku na kule kwa ajili ya ugonjwa wake mwenyewe. (Binafsi mimi mke wangu, hana hata chembe ya ubinafsi kwenye maswala ya pesa)
 
Fact
 
Kama mwanamke unafanya kazi halafu hela zako hazichangii kwenye ustawi wa familia yako ni bora ukae nyumbani tu. Wengine tuko proud kabisa kuchangia maendeleo ya familia. Kila siku unaenda kazini kufanya nini sasa. Wanawake tuache ubinafsi . Mtu unashindwa kununua hata umeme au kulipia maji. Sisi tumezaliwa kijijini huko lakini baba na mama walishirikiana kutulea sisi mpaka tukasoma vizuri. Ingekuwa baba anabeba majukumu yote sijui kama tungefika hapa tulipo. Na waliisha pamoja mpaka kifo kikawatenganisha. Dada zangu wote pia nimeona walivyo bega kwa bega na waume zao na unaweza kuona jinsi maisha yao yalivyo mazuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…