Nimempinga Godbless Lema ila sasa Natubu

Lema anaongea mambo mazito sana ambayo hayawezi kuhimilika kwa watu mediocres
 
Hapo kwenye exposure ndipo kwenye point zake zote Lema zilipo, mambo ya ugali,boda boda ni mifano,anataka kutufungu akili kwa mifano rahisi,kwa mtanzania mwenye upeo hawezi kuona bodaboda kama kazi ya kudumu hata kama muhusika analisha familia, tunaangalia productivity nationwide...je baadaya miaka mitano tutapiga hatua zipi kwa kutegemea bodaboda?
 
Lema anaongea mambo mazito sana ambayo hayawezi kuhimilika kwa watu mediocres
Tuletee cv ya Lema hapa then we will be in a position to know who is really a mediocre
 
Tupe hoja nzuri moja tu ya Lema
Hoja moja,Lema anajaribu kutuonyesha sisi ni masikini wa kipato, kufikiri,anatuamsha tuamke tutoke nje ya box tuwaze, anajaribu kuonyesha bodaboda sio kazi ya katika nchi zilizoendelea na zinazotaka kuendelea,lazima kama nchi tutafute ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la ajira.
 
Kwa hiyo boda boda ndio kilaza Lema kaona ndio shughuli kuu wafanyayo watanzania sio
 
Yeye kama Lema aliweza fanya nini kwa kufikiri na kuweza kujikwamua kimaisha kama ambavyo kuna wafanya biashara ambao wanatoa wasifu wao njia walizopitia hadi kutoboa .Huyu mwamba feki yeye analaumu kwa kwenda mbele.Brother mawzo mmbadal sio kulaumu bali ninkutoa mbinu za nini kifanyike.
 
Tuletee utajiri wa Lema hapa na elimu yake pia ili tuweze kudadavua vizuri aisee
Hoja sio utajiri wa Lema wala Elimu yake, tunazungumzia Taifa kwa ujumla.
Labda uniambie wewe je Tanzania ni nchi masikini au tajiri,na je asilimia kuwa ya watanzia ni masikini au matajiri?
 
Jamaa utakuwa mwl maana unajua kuelimisha!! Hakika huwezi ku transform uchumi wa nchi ushindane duniani kwa kuwadump vijana katika ubodaboda na vikoba kumfanyia kazi muhindi
 
Hoja sio utajiri wa Lema wala Elimu yake, tunazungumzia Taifa kwa ujumla.
Labda uniambie wewe je Tanzania ni nchi masikini au tajiri,na je asilimia kuwa ya watanzia ni masikini au matajiri?
Je kenya na uganda ni matajiri?
 
hoja sio tatizo utekelezaji upo...? Kwani lema si alikuwa Mbunge au ? Amefanya kipi?
 
Maskini wtz bado tunawaza takataka za uchaguzi!! Wee ni chata halisi ya mtu mweusi ebu kuwa serious yaani huoni Lema katuamsha!? Acha ulafi kufikiria uchaguzi mzee hapa ndipo tunakwama.
Huyo anawakilisha uhalisia wa akili za hao "maafisa usafirishaji" waliosemwa na bwana mdogo Lema.

Wanafikiria uchaguzi tu ili wapate kujaziwa mafuta pikipiki zao na kupewa elfu kumi kumi tu.

Huyu jamaa ndiyo mojawapo ya wale ambao ndugu Lema amewaongelea.
 
Lema ametoka kimaisha? Unadhania angekuwa ametoka kimaisha angeendelea kupigwa jua ili aweze tu kupata kipato kupitia siasa?
Achana na Maisha ya Lema yeye analizungumzia Taifa na watanzania wote,hata kama yeye ni masikini wa kipato,lakini hoja zake zina maana,anaonyesha kabisa kwamba sisi kama Taifa ni lazima tupambane tutoke hapa tulipo kwenye hali ya umasikini
 
Tati
Hoja sio utajiri wa Lema wala Elimu yake, tunazungumzia Taifa kwa ujumla.
Labda uniambie wewe je Tanzania ni nchi masikini au tajiri,na je asilimia kuwa ya watanzia ni masikini au matajiri?
Tatizo watu wanapeleka chuki zao binafsi kwa Lema wanaacha kuona ukweli wa hoja za mujarabu kabisaaa na kazileta wakati muhafaka ila walafi hawataki watu wafunguke akili
 
Achana na Maisha ya Lema yeye analizungumzia Taifa na watanzania wote,hata kama yeye ni masikini wa kipato,lakini hoja zake zina maana,anaonyesha kabisa kwamba sisi kama Taifa ni lazima tupambane tutoke hapa tulipo kwenye hali ya umasikini
Yeye ameshaweza kupambana na kutoka kimaisha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…